Huu haukuwa muda muafaka wa Rais Samia kutembelea Marekani: Amejiweka kwenye Shinikizo la kulazimishwa kuilaani Urusi

Huu haukuwa muda muafaka wa Rais Samia kutembelea Marekani: Amejiweka kwenye Shinikizo la kulazimishwa kuilaani Urusi

Marekani sio rafiki kwani wamekataza Raia wao kuja hapa.

Rais wetu anakwenda huko kufanya nini??

View attachment 2186624
Kwani uongo, wewe huwa unajiona Salama mtaani kule Tabata au Mwenge usiku? Hata ukilala itabidi uweke komeo na lango la chuma. Ukiwa na gari nzuri hapo ni balaaa. Hata mimi naogopa si uongo. Umeshawahi kukaa Ulaya, marekani, Canada, Singapore au hata China tu?
 
Kwa taarifa yako hakuna taifa loliloua watu wengi duniani kama marekani!! Huko Iraq, Syria, Afghanistan na funga kazi ni huko Japan alikopiga Bomu la nyuklia.
Kwa hiyo kwa Logic yako, kama Marekani aliua watu Iraq, Afghan, Japan etc etc basi Russia naye aue tu?
Hao unaosema waliuawa na marekani walitaka wenyewe na wakaonywa ingawa sikushabikia hizo vita:
== Bila ya Japan kupigwa mabomu kwenye vita ya pili ya dunia Uharibifu mkubwa ungetokea - jiulize kule Pearl Harbour kilitokea nini, Japani walifanya nini. Musolin, Hitler ndiyo walikuwa partner wao.
  • Iraq - Kwanza Sadam aliteka Kuwait akasema nchi yake, akaja Bush mkubwa akamtoa kwa sababu alivamia nchi huru. Baada ya kutolewa akaanza fujo kuwa yeye ana nuclear, chemical weapons, akawa anazuia UN wasikague, kumbe masikini ilikuwa hana chochote, akapigwa utamlaumu nani hapo? Kwanza kapiga Kuwait, Kanyanyasa watu wake, halafu kaanza kutishia kuwa ana silha. Wakati Huo ndiyo imepita 9/11 au hukumbuki?
  • Afghanistani Walimweka (walimhifandhi) Bin Laden Osama, aliyetuhumiwa kuwa ni Terrorist mkubwa aliyeplan ku bomu World Trade Center 9/11, sasa wewe umeumizwa kiasi hicho utafanya nini?

I am not pro USA, laikini huwezi kulinganisha hii vita na Ukraine. Ukraine ni Nchi Huru wala siyo provocative Russia anataka wawe kwenye himaya yake, ati usijiunge na EU, usiwe na Silaha fulani, usijiunge na NATO,
 
Wasaidizi wa Rais Samia Suluhu Hassan wametenda kosa kubwa sana kwa kutokumshauri Rais kuwa huu haukuwa muda muafaka wa yeye kutembelea Marekani.

Marekani Ina hasira na Nchi nyingi duniani kwa kutokuiunga mkono katika harakati zake za kuitenga Urusi katika jamii ya kimataifa. Tanzania tumeamua kuwa neutral/kutokuwa na upande katika mzozo wa Urusi na Ukraine.!
Kama mko neutral si ndo mkaitangazie dunia yote ielewe?!
Alafu hii tabia ya kuwa neutral wakati mwenzako anadhulumiwa ni unafiki, woga uliopitiliza. What if wakati wako utafika na wewe uanze kudhulumiwa??

Kingine ninachoamini kwa Samia... Hapendi uonevu. Ana hofu ya Allah... Na kama mwana ccm mzalendo... Atasema na kusimamia ukweli!

Lakini si majuzi tu hapa mlifurahia Samia kukaa karibu na Biden kwenye majukwaa ya kimataifa? Lazima walijenga urafiki.

NB: Putin ni vampire!
 
Fikra za utegemezi hazitatuondolea kero za maendeleo. Swali la msingi tangu tumepata uhuru tumekuwa tukitegemea na kupewa misaada, je, imetuondolea umaskini?
Umaskini uondolewa na watu wenyewe...
Sisi tumechagua maendeleo ya vitu badala ya watu!
Mkipewa misaada mnajenga madaraja na matumbo yenu mnashindwa kuwaendeleza watu wenu hilo kosa la nani??
 
Wasaidizi wa Rais Samia Suluhu Hassan wametenda kosa kubwa sana kwa kutokumshauri Rais kuwa huu haukuwa muda muafaka wa yeye kutembelea Marekani.

Marekani Ina hasira na Nchi nyingi duniani kwa kutokuiunga mkono katika harakati zake za kuitenga Urusi katika jamii ya kimataifa. Tanzania tumeamua kuwa neutral/kutokuwa na upande katika mzozo wa Urusi na Ukraine.

Kwa Marekani ukiamua kutokuwa na upande unahesabika kuwa uko upande wa Urusi, na inafanya Kila jitihada kuyatisha mataifa yenye msimamo huo Ili yailaani Urusi! Kwa hiyo ukiandaa mazingira ya kukutana na Marekani kwa Sasa lazima ikushinikize kuilaani Urusi.

Sidhani Kama mama atakuwa na ubavu wa kuhimili shinikizo la Marekani katika jambo hili. Anaweza kujikuta amesema jambo ambalo hakutegemea akiwa chini ya shinikizo. Sidhani kama ataweza kuhimili Kama India na Afrika ya kusini zilivyoweza kuhimili.

Afrika hatuwezi kulaani Nchi ya Urusi iliyokuwa mstari wa mbele Sana kwenye harakati za upatikanaji wa uhuru kusini mwa afrika-(Zimbambwe, Msumbiji, Botswana, Angola, Namibia na Afrika ya kusini).

Wakati huo wapigania uhuru akiwemo Mandera walikuwa wanaitwa magaidi na Marekani!! Chonde chonde Samia Mungu akutie nguvu uwatolee nje mabeberu huko Marekani!
Wewe toka upigwe ban kukanyaga marekani kwa tuhuma zako za kudhulumu uhai wa watu bado unatapa tapa sana bashite.
Hebu tulia hangaika kwanza na mashoga wenzako wanaotaka kukuua maana unawapora waume zao
 
Yaani usifanye mambo yako kisa mtu mmoja tu aliyeamua kumvamia mwingine kwa ajili ya ego yake?
Ndio maana mtoa post kashauri kuwa sio wakati mzuri kwake kwenda Marekani. Yaani uende ugenini kwa mtu halafu useme unafanya yako? We Mtanzania kweli?
 
Eti Russia maskini wa kutupwa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] ingekua hivo basi hao unaowashobokea wasingetumia nguvu kubwa kumdhoofisha kiuchumi kupitia vikwazo,,,Russia sio zimbabwe na wala usiifananishe na Tzn hatuifikii,,View attachment 2186719
Wanatumia akili sio nguvu za vita kama anavyofanya huyo Maskini unaemshobokea..

Daima nitasimama na beberu
 
Kama ungeorodhesha ambayo unaamini kwa muda wa miaka 6 angeyakamilisha, hoja yako ingekuwa na uzito. Lakoni ukweli ni kwamba alishughulikia miradi ya kimkakati, naamini usingetegemea ikamilike ndani ya muda mfupi, na akaboresha na kupanua huduma za jamii (elimu na afya)
Mbona mnahangaika na Samia aikamilishe Kwa mwaka mmja? Mwaka 1 vs miaka 6 upi ni mda mfupi?

Good enough saizi tunaenda Kwa speed kuliko hapo awali,sio tuu Kwa speed bali na mambo mengine ya msingi yanaenda kinyume na visingizio vya kijinga vya Mwendazake eti tunajenga miradi Ili kuficha udhaifu wa kushinda kukuza Uchumi wa Nchi..

In fact mimi siungi mkono mradi Hata mmja wa ndenge,sgr wala Bwawa la Umeme Kwa sababu Tulikuwa na options za maana kuliko hivyo vinavyofanyika kwa Sababu miradi mingi kama sgr ni white elephant..

Pesa iliyoingizwa kwenye sgr ingeingizwa kwenye Barabara Leo tungekuwa mbali Sana kiuchumi.
 
Huu uzi una walakini, kwani unawasemea viongozi wetu wakati hatujui maudhui wa ziara hii. Ila ndio fursa za kutoa mawazo.
 
Agenda ya kuhitaj misaada haikwepeki! Pia mzungu sio mjinga eti umkwepe kwa kukaa ndan kwako unless otherwise usimtegemee kwa chochote! Baki kwako usiende kwao lkn agenda zao watakutupia mezan na uzifanyie kaz.
Unajua kuna watu hapa JF wanadhani mambo ya mahusiano ya kimataifa yanaendeshwa kama wanavyofikiria wao. Huyu mama kwenye diplomasia ya uchumi amefaulu sana kwa mazingira ya sasa
 
Kinana na tuhuma zote hizo bado unamfagilia,are you crazy!Oh,my God,tumekwisha kwa mitizamo hii,Watanzania kushnei.
Kwenye utawala wa sheria tuhuma haimzuii mtuhumiwa kupumua, ushahidi unahitajika kumshughulikia kisheria vinginevyo utaumia rohoni kwa kusubiri matokeo unayoyafikiria ambayo hayatatokea
 
Kwenye utawala wa sheria tuhuma haimzuii mtuhumiwa kupumua, ushahidi unahitajika kumshughulikia kisheria vinginevyo utaumia rohoni kwa kusubiri matokeo unayoyafikiria ambayo hayatatokea
Kiongozi kuto-watendea haki unao-waongoza na wao hatimaye wakanung'unika inatosha wewe kiongozi Mungu kukuwajibisha.Samia awe makini sana,yapo maandishi tayari ukutani👇

images.jpeg
 
Hiyo ni dharau!! Nampongeza Magufuli kukaa zaidi ya miaka 5 bila kupiga hodi kwenye mlango wa beberu yeyote!
Watanzania hatuihitaju Marekani, tunamhitaji Mungu!!
🤣🤣🤣 sasa yule mshamba angeweza kwenda nchi gani, Samia ni level nyengine hata kabla ya kuwa rais, waulize wanaomjua
 
Back
Top Bottom