Huu umilikishwaji wa vitega uchumi muhimu vya nchi kwa waarabu, ni uwekezaji au uvunaji?

Hiyo Heathrow walipewa bure kama sisi tunavyo gawa hizi za kwetu? Maana DPW mpaka sasa hajaweka hata shillingi moja ila amepewa bandari na anaanza kula hela bora wale wachina + Quatar waliokuwa wanakuja na hela zao kujenga Bagamoyo na viwanda vyake tungepata hata ajira sio hii ya DPW.
Hujui unaloliongea.
 
Umeona mikataba ya hizo ports zaidi ya 70?
Nazo ziliandikwa kienyejically kama huu wa kwetu?

Kwanza katika hayo mataifa makubwa yote, hakuna hata nchi moja ambayo DPW imepewa bandari mama. Inapewa kuendesha bandari za huko pembeni. Na mikataba yao ni tofauti kabisa, siyo wa kishenzi kama huu wa kwetu ambako amepewa bandari mama.
 
Kenya sio kwamba mafara na mm naona wakenya bado hawajafanya kweli yaan ilitakiwa wachome mali zote za mafisadi wawapige ua kabisa hao mbwa ....inaumiza sana kuona nchi yetu inawasomi wa kila kada ila kila sehem tunashindwa kuwapa ukiangalia kwa undani ufisadi tu umetawala ni bora tufunge shule na vyuo ziwe guest house za malaya tu.

Sasa tunasomesha ili waje wafanye nn km rasimali zetu wanapewa wageni tu angalia barabara asilimia 80 ama 90 wakandarasi ni wageni hata kwenye majengo na sehem kibao.Natamani nitukanee niandamane Maana siioni kesho ya wanangu kabisa
Kuna mbwa bado unakuta zinajisifia tunaupiga mwingi fuken kabisa mwingi upi ....nitatukana tu maana inaumaaaa sana🥶
Waswahili tunapopewa tunaiba na kufilisi, tunakuwa maadui namba moja wa kilichowekezwa.

Kwanza tuondokane na huu ulemavu wetu wa fikra kila tunapoajiriwa na haya makampuni makubwa.
 
Yule hajapewa kitu

Kanunua
Dangote na twyford, wale wamewekeza, wamejenga viwanda vyao, siyo waporaji kama hawa waarabu wanaochukua tulivyokwishavijenga.
 
Unaona mkuu Bams, wajinga niliowasema ndo Hawa

Yeye anaona ufaharibkuibwa na kunyonywa na mwabu badala ya mzungu

Wako wengi misikitini Wana fundishana ujinga

Tunasema hatufungamani na mwekezajin myonyaji awe mzungu awe mwarabu
Wote ni adui kwetu
Mwafrika kashindwa kuendesha mashirika yaliyoanzishwa na mwalimuu Nyerere awamu ya kwanza.

Kabla hujaja na lawama kwa Samia rudi nyuma utazame namna Mkapa alivyouza mashirika na alikuwa ni mkristo mwenzetu.

Blame Game haina faida kwetu na tusipobadilika tutapelekeshwa na wageni mpaka mwisho wa dunia.
 
We unaejua tuambie
Makelele tu, ufanisi wetu huko katika uendeshaji wa mashirika ni mdogo. Elimu inabadilika kwa kasi na unakuwa ni mzigo ule uongozi usio na njia za kisasa za kuendesha mashirika.

Wizi wa kila aina na ubadhirifu ni sifa nyingine mbaya ya uendeshaji wa kizalendo, tunataka kuishi juu ya kile kipato chetu halisi.
 
Kwani mkataba wetu una shida gani? Au bado umekaririshwa maneno machafu ya Dr Slaa na Mwabukusi?

Kama huwezi kuona ubovu wa ile IGA ya kishenzi, ambayo kupitia hiyo, ndiyo kumetengenezwa HIGA ya bandari, basi utakuwa mtupu sana kichwani.

IGA bado inatamka kuwa:

1) nchi hairuhusiwi kumtafuta mwekezaji mwingine yeyote kwaajili ya bandari yoyote iwe kwenye bahari, ziwa au mto ndani ya Tanganyika bila kwanza kuwataarifa DPW, na wao kuridhia.

2) DPW wakitaka arhi yoyote ile, eneo lolote lile, Serikali inalazimika kuwahamisha wanaotumia eneo hilo ambalo DPW wanataka, na Serikali italazimika kuwalipa fidia hao waliohamishwa.

3) DPW hawalazimiki kulipa kodi za nchi kama sheria inavyotaka.

Hiyo ni mifano midogo tu ya uhovyo wa ile IGA. Na hakuna kipengere hata kimoja, mpaka sasa kilichobadilishwa kwenye IGA.
 
Wengi wanaishia kua bodaboda,machinga huku kuna watu wanakuja tu na briefcase na makaratasi kibao wanapewa miradi wazawa wanabaki kua machawa.Kuna faida gani sasa ya kusoma yaan mwanangu asome leo kesho aje kua anasifie watu.
Nataka nifanye maamuzi magumu sana mwanagu akimaliza la saba tu namuingiza kwenye biashara zangu tu ajue abc..mapema kuliko kwenda kujaza ujinga shuleni.Mm naona watoto wetu wanaenda kujazwa ujinga maana km wanasoma na hiyo elimu haiwakwamui inafaida gani ni upuuzi.

Muache mtoto asome mpka mwisho.
 
Kwanza katika hayo mataifa makubwa yote, hakuna hata nchi moja ambayo DPW imepewa bandari mama. Inapewa kuendesha bandari za huko pembeni. Na mikataba yao ni tofauti kabisa, siyo wa kishenzi kama huu wa kwetu ambako amepewa bandari mama.
Hiyo bandari mama ya Tanzania inategemea kusafirisha mzigo wa DRC, Rwanda, Zambia, na Uganda utakaoletwa na SGR. Ungependa uone mambo yale yale ya wateja kukimbilia bandari ya Mombasa yakijirudia tena muda huu katika ushindani mkubwa wa shoroba uliyopo?.
 
Kama huwezi kuona ubovu wa ile IGA ya kishenzi, ambayo kupitia hiyo, ndiyo kumetengenezwa HIGA ya bandari, basi utakuwa mtupu sana kichwani.

IGA bado inatamka kuwa:

1) nchi hairuhusiwi kumtafuta mwekezaji mwingine yeyote kwaajili ya bandari yoyote iwe kwenye bahari, ziwa au mto ndani ya Tanganyika bila kwanza kuwataarifa DPW, na wao kuridhia.

2) DPW wakitaka arhi yoyote ile, eneo lolote lile, Serikali inalazimika kuwahamisha wanaotumia eneo hilo ambalo DPW wanataka, na Serikali italazimika kuwalipa fidia hao waliohamishwa.

3) DPW hawalazimiki kulipa kodi za nchi kama sheria inavyotaka.

Hiyo ni mifano midogo tu ya uhovyo wa ile IGA. Na hakuna kipengere hata kimoja, mpaka sasa kilichobadilishwa kwenye IGA.
Upuuzi mtupu umeandika kuhusu DPW, ufafanuzi wa kila namna na wa kina ulishatolewa na hauwezi tena ukawa unarudiwarudiwa kutolewa.

Hiyo IGA inazuia vipi uwekezaji wa mwekezaji mwingine wa sekta bandari?. Mbona pale TPA keshakuja mwekezaji mwingine mhindi na IGA haijazuia chochote kufanyika?.

Utawapata wajinga wajinga lakini wenye kujielewa wanakusoma na kukuona ni wale wale tu walalamikaji.
 
Bams amekariri anataka mambo ya hovyo yaenedelee kutokea TPA wakati tunapoteza mapato
 
Ndugu mbona umepitwa na wakati? Yote hayo uliyandika siyo kweli. Mbona kuna mwekezaji toka India anaitwa Adani Group lachukua berth 8, 9, 10 & 11.

Halafu kuna ubaya gani DP WORLD akichukua eneo jingine kwa ajili ya kuleta ufanisi. Kwani wale watu wa Kurasini hadi Kilwa Road Police wafididiwa fedha na Serikali ikawapa eneo jingine wewe unaumia nini?

Hilo la kutokulipa kodi za nchi ni UWONGO, kajipange upya
 
Nadhani serikali ijikite kutoa elimu kwa wananachi wapate kujua maana ya uwekezaji! Vinginevyo itaendelea kulaumiwa mpaka basi.
 
Bams amekariri anataka mambo ya hovyo yaenedelee kutokea TPA wakati tunapoteza mapato
Kila kitu anakiangalia katika mtazamo wa kisiasa hapotezi hata muda kuutazama uhalisia wa kiuchumi.

Baba Askofu Kitima alishawishi kanisa zima likausoma waraka ndani ya ibada baada ya muda wakajitokeza hawa wahindi kutaka kuwekeza na wakakubaliwa. Mmoja wa maaskofu akampigia simu Hamza Johari kumueleza mshangao wake wa TPA kutangaza tender wakati IGA ya DPW ilikuwa inadaiwa kuwa hairuhusu mwekezaji mwingine yoyote kufanya biashara na Tanzania!.

Siku ya kusaini hiyo mikataba pale ikulu akawepo Baba Askofu Kitima katika sehemu ya wageni waalikwa. Tunalo tatizo la ujuaji na ni la kitaifa. Unapoongea sana ukiwa huna maarifa ya kutosha unazidi kuuanika ujinga wako.
 
Upuuzi mtupu umeandika kuhusu DPW, ufafanuzi wa kila namna na wa kina ulishatolewa na hauwezi tena ukawa unarudiwarudiwa kutolewa.

Hiyo IGA inazuia vipi uwekezaji wa mwekezaji mwingine wa sekta bandari?. Mbona pale TPA keshakuja mwekezaji mwingine mhindi na IGA haijazuia chochote kufanyika?.

Utawapata wajinga wajinga lakini wenye kujielewa wanakusoma na kukuona ni wale wale tu walalamikaji.

Wewe hakika ni punguani.

Kitu kikishawekwa kwenye mkataba, wahusika wa kwenye mkataba, yeyote miongoni, akiwa na dhamura mbaya, akitaka anaweza kupuuza kufuatilia kipengere fulani ili wewe uhadaike. Siku akitaka kukufix, atafanya hivyo bila shida kwa kuutumia mkataba ambao wewe uliusaini.

Ungekuwa na akiki lapo kidogo ungejiuliza kwa nini waarabu hawataki kuviondoa hivyo vipengere tata kwenye IGA.

Fuatilia uone yaliyowatokea Dgibout, ambao wameamriwa na mahakama kuwalipa DPW zaidi ya dola milioni 700.

Kama DPW hawana dhamira mbaya, waambie waondoe hivyo vipengere kwenye IGA, uone kama watakubali. Pamoja na kila mwenye akili na weledi, kuanzia chama cha wanasheria Tanganyika mpaka wasomi wabobezi, kulaani vipengere hivyo, waarabu wamegoma kabisa kubadilisha badala yake wakaendelea na vikao vya siri na watawala ili kukubaluana namna ya kuwapumbaza Watanganyika, lakini siyo kubadilisha kipengere chochote.
 
Punguani ni wewe unayerudia habari iliyokwisha kutolewa ufafanuzi tena na mwanasheria mbobezi wa hayo masuala ya IGA.

Kuwepo kwa hivyo vipengele kunaziua vipi kampuni ya Adani kumiliki magati namba 8-11?.

Kuwepo kwa IGA na vipengele vyake kunazuia vipi uwekezaji kufanyika katika bandari zetu nyingine?.

Kwa taarifa yako kuna mikataba mingine itaingiwa kati ya serikali na waendelezaji wenye uzoefu wa masuala ya bandari katika kipindi kijacho kuhusiana na bandari zetu nyingine na hakutakuwa na lolote litakalofanywa na hao DPW.

Usilete maongezi ya kwenye viti virefu vya Bar humu kwenye jukwaa lenye watu wenye uelewa mpana wa kinachofanyika pale TPA.

Usilete story za kwenye ulevi mbele ya watu wenye kuelewa kwa kina Serikali ya awamu ya sita inafanya nini na ina mpango gani wa kutimiza hicho inachokifanya.
 
Back
Top Bottom