Huu Utitiri wa Maofisa wa Serikali kwenda Hanang, Wanaenda Kufanya Uokoaji au Kuonekana?

Huu Utitiri wa Maofisa wa Serikali kwenda Hanang, Wanaenda Kufanya Uokoaji au Kuonekana?

Itifaki lazima izingatiwe...uliona wapi waziri mkuu anapanda daladala ktk shughuli zake za kiserikali?
 
Elewa mantiki ya Uzi acha kukurupuka kama chawa
Acha mantiki za kishamba wewe unafikiri gari linaweza kuzuia janga kama hilo, na ulitaka waje kuwaona watanzania wenzao kwa punda. Yaani ufikiri kitendezi watu wachangia na ujinga. Unajua ofisi ya waziri mkuu majukumu yake, kweli ?. Vijana fikra mgando na zitazidi kuganda
 
Wadau nimetizama msafara wa mawaziri, manaibu,Makatibu wakuu,wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama,wakuu wa mikoa mbalimbali,wakuu wa wilaya mkoa Manyara..... na wengine wengi.Ni kufuru mav8 yote hayo wakati wangeweza kupanda luxury bus Moja ama mbili the rest wakasaidia wahanga.Mungu turehemu waja wako....Tanzania bila ccm inawezekana.
Mafuta kwa siku lazima watumbue kama 5b za mafuta na perdiem
 
Wengi wenu hampajui hanang' na hamjawahi kufika huko katesh ndio maana mnaropoka baada ya kushiba kande zenu!! Yaani mnataka viongozi wa dola wapande daladala iwapitishe ktk milima ya mbulu hivi mko sawa kweli?
 
Watanzania ni wazee wa kulalamika ,ulitaka waende kartesh na punda au v8 linaweza kuzuia natural disasters like flood. Jamani vijana tunashindwa wapi kufikiri. Je, viongozi wasipoende kuwafariji ndugu zetu napo mtasema serikali imekaa dodoma wameshindwa kwenda kuona wahangaa .
Unajiona na ww umejibu kitu
 
Wadau nimetizama msafara wa mawaziri, manaibu,Makatibu wakuu,wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama,wakuu wa mikoa mbalimbali,wakuu wa wilaya mkoa Manyara..... na wengine wengi.Ni kufuru mav8 yote hayo wakati wangeweza kupanda luxury bus Moja ama mbili the rest wakasaidia wahanga.Mungu turehemu waja wako....Tanzania bila ccm inawezekana.
Viongozi wa Africa walipandishwa basi walipoenda UK kwenye mazishi waAfrica waliponda sana!
Ngoja watanue kwa Ma-v-eite!
 
Lwakwanza lamsingi wanapaswa kumobilize resources kusaidia wahanga, wataalamu kustudy kwa haraka nini kilichotokea na kuna uwezekano kikaendelea tena soon, Je maeneo mengine yanayofanana na hilo eneo na hizi mvua nini kifanyike haraka?

Kwasasa sio muda wa ziara, kutazama na kutoa pole...
 
Mnaliona na msafari tu safari za nje zinaharimu sana kuliko hii misafara.

Business class $4,000 mpaka $6,000
Hotel $200 mpaka 1,000 per night
Kula yao kila mmoja $100 mpaka $300
Usafiri wao $$$
 
Watanzania ni wazee wa kulalamika ,ulitaka waende kartesh na punda au v8 linaweza kuzuia natural disasters like flood. Jamani vijana tunashindwa wapi kufikiri. Je, viongozi wasipoende kuwafariji ndugu zetu napo mtasema serikali imekaa dodoma wameshindwa kwenda kuona wahangaa .
Ngoja nimsaidie mwanzisha siredi.
Hoja yake badala wa wakuu wa mikoa kadhaa kwenda na ndinga zao Kila mmoja.

Wangetumia bus kubwa ambalo lingeokoa gharama zifuatazo.
1. Muda wa wananchi na waokoaji kusubiria VIONGOZi wafike.
2. Mafuta,
3. Gharama nyinginezo za mapokezi.
 
Chaos at best

Madhara ambayo unatarajia kuona trained ‘emergency response team’ inayoongozwa labda na kikosi cha zimamoto (usually hilo ndio kundi ambalo linakuwa trained more than others kwenye ku deal na aftermath za natural disasters), unatarajia kuona fist aid responders kama medics wakiwa mstari wa mbele, ambulances na polisi wakilinda maeneo.

Tanzania polisi ndio wapo juu ya paa za watu badala ya zimamoto na viongozi wa serikali kwa mbali mikono kiunoni wakitoa porojo.

Hakuna kikosi cha fire wala ambulance, hakuna call for help ya fire services za mikoa mingine kwenda kuongeza nguvu za uokoaji kwenye kusaidia kudeal na situation.

Halafu wakienda huko kwenye COP meetings wanadai waongezewe hela za kukabiliana na natural disasters zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia za nchi, hizo hela wakipata wanaweka matumboni mwao tu maana clearly hakuna ‘emergency response team’ kwa kinachoonekana kule zaidi ya watu kwenda kutafuta posho za kazi tu.

What a pity
 
Vipo vifaa maalum vya auokozi vya kisasa ambavyo tulitarajia kuwaona watu wetu wakiwa navyo.

Kwa wale wenye mashaka na kutaka kujua vifaa gani basic tunazungumzia jaribuni kugoogle WATER, MUD AND ICE RESCUE.... mtaona nini tunamaanisha.

Mkoa wa Manyara uko karibu na Jiji la Arusha ambalo ni jiji linaloingiza pesa nyingi za utalii lakini pia kuna Mji wa Kilimanjaro wenye uwanja wa ndege wa kitaifa na ambao pia una mlima mrefu unaovutia watalii kila kukicha na maeneo mengine, tungetegemea kuona namna bora ya uokozi wa kisasa na utalaam hapo Manyara baadala ya njia zetu za kienyeji za kila siku.. HAPA NDIO TUNAPOSHANGAA VS MATUMIZI YA SERIKALI.
 
Hatujawahi kupata tatizo kama hili tangu Uhuru. Hivyo ni Kazima Waende Mawaziri WA Uchukuzi, Ujenzi, Mawasiliano, Afya, tanesco, Maji, n.k kujionea Maafa ya Sector zao.
 
Wengi wenu hampajui hanang' na hamjawahi kufika huko katesh ndio maana mnaropoka baada ya kushiba kande zenu!! Yaani mnataka viongozi wa dola wapande daladala iwapitishe ktk milima ya mbulu hivi mko sawa kweli?
HAPANA!
Weka hadhi pembeni leta gharama za hizo Ma-v-eite karibu.
Imagine kila kiongozi na lake! Bado posho! Yaani gharama ukijumlisha ni kubwa mara 💯 ya kinachowapeleka Hanang'
 
Unadhani kikiingia chama gani mambo yatabadilika??

Hizo ni akili za kiafrika na moja ya sababu ya hayo ni viongozi kuwahi kuishi kwenye umasikini. Tabia za maskini akipata si unazijua!?
 
Wadau nimetizama msafara wa Mawaziri, Manaibu, Makatibu wakuu, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, wakuu wa mikoa mbalimbali, wakuu wa wilaya mkoa Manyara na wengine wengi.

Ni kufuru mav8 yote hayo wakati wangeweza kupanda luxury bus Moja ama mbili the rest wakasaidia wahanga.

Mungu turehemu waja wako. Tanzania bila CCM inawezekana.
Halafu utakuta wote wakifika huko wanaangalia tu hakuna anayeshika hata beleshi!
 
Back
Top Bottom