Huu Utitiri wa Maofisa wa Serikali kwenda Hanang, Wanaenda Kufanya Uokoaji au Kuonekana?

Huu Utitiri wa Maofisa wa Serikali kwenda Hanang, Wanaenda Kufanya Uokoaji au Kuonekana?

Ngoma ya wazaramo "Mdundiko" inapopita mitaa ya uswahilini hukumba washabiki, wambea, wanafiki, malumpeni na mapashkuni ya kila aina. Hukusanya watu wa kila aina kama alivyofanya mpiga filimbi wa Hamelin!....
Taifa letu Lina Serikali inayozinduliwa na matukio zaidi kuliko mipango ya muda mrefu. Tukio la Hanang ni ushahidi wa kinachoendelea sasa.... 😢
 
Nimeiona video ambayo inaonyesha msafara wa kiongozi wa serikali kuingia Hanang kwenye maafa ya mafuriko.Msafara una Landcruiser LC 300 zaidi ya 15 ambazo zinakwama kupita kwenye lile tope zito .

Najiuliza msafara mkubwa vile na magari ya anasa unaenda kuwasadia nini watu wa Hanang?
 
Sijasema wakubwa wasiende ila napenda watakaokuwa front ndio watangulie plus Mahitaji ya Waathirika badala ya kwenda kuleta taharuki nyingine.

Huko PM yupo
Mkuu wa Majeshi yupo
Mawaziri wapo

Na wengine wanaendelea kumikinika ,Sasa sijajua Kama Kasi ya wakubwa kumikinika inaendana na Kasi ya Uokoaji.

Mlioko eneo la tukio tuambieni kama mnapata mahitaji stahiki kuanzia tiba,mahema,vyakula,maji,nk?

Pia soma > Manyara UPDATE: Waliofariki kwa Mafuriko Wilayani Hanang wafikia 49

---
PICHA: BAADHI YA VIONGOZI WALIOZULU HANANG

View attachment 2833818View attachment 2833819
Huyo dingi mwenye tshrt nyeusi imeandikwa Samia love kama namfananisha hivi ni nani huyu?
 
Iko hvi kwenye Hili janga lilio wapata watanzania wenzetu Kuna watu hawako serious kbsa na Bado wana fanya mambo ya kipuuz hadharani

Huyu Dr mollel amekuaje azunguke na chopa angani wkt kwa uhalisia yey alipazwa kuwa ground akifanya uokozi na kufunga watu vidonda na kuhakikisha vifaa Tiba na madawa vinavyo takiwa vinakuwepo kwa muda sahih Lkn ajabu yupo angani anazunguka kufanya survey wkt siyo kazi zake hizo

Anazunguka as if Ni mtaalamu wa wizara na consultant wa mambo ya Hali ya hewa na mazingira

Tunachotaka wale watu hawataki mzaha wana stressed hawajui hatma yao hawajui itakuje ,hawajui hatma nzima ya maisha Yao baada ya wanna siasa kuondoka pale

Imagine mtu kapoteza mke watoto ,nyumba ,ngombe zake HV watakuwa Hali gani ,alfu mtu anazunguka na chopa na kina bashungwa siku nzima

Nashauri wale watu watazamwe kwa jicho la tatu View attachment 2834477
IMG_20231206_112117.jpg
View attachment 2834478
 
Halafu tuwe na kumbukumbu.Malawi waliathiriwa na kimbunga, serikali yetu ilipeleka huko tani 90,000 za mahindi, mahema,mablanketi,gari ya wagonjwa,ambulance, karakana ya magari yanayotembea,malori na helikopta 2.
Huku tumeanza kuona viongozi wakienda kutoa pole ,sawa lakini wafanye zaidi maana tuliweza kuwasaidia malawi na uturuki tutashindwaje nyumbani?.
 
Huyo dingi mwenye tshrt nyeusi imeandikwa Samia love kama namfananisha hivi ni nani huyu?
Ukiona majitu ya hivyo, ujue ndiyo yale majitu yenye unafiki wa hali ya juu. Jitu la hivyo utakuta halijawahi kumwambia hata mama yake mzazi, mama nakupenda, halafu linataka kumpumbaza Rais aamini kuwa linampenda sana.
 
Wadau nawasabahi.Nimewaona VIONGOZI wetu wakimiminika kwa wingi kuelekea Hanang kuliko tokea Mafuriko ambayo mpaka sasa Watu 69 wamekwishafariki.Utitiri wa hawa VIONGOZI na uharaka walionao wa kwenda Hanang umekuwa mkubwa kiasi cha kutisha.Najaribu kujiuliza endapo kwa Mwitikio huu.

Je VIONGOZI hawa wangekuwa Wanaitikia kwa kasi hii kwenye Maeneo yao ya kazi hakika NCHI ingepata Maendeleo Makubwa.

Nawashauri hawa VIONGOZI Kasi hii ya kwenda HANANG isiishie Hanang bali WAONGEZA KASI HII kwenda kusimamia sehemu zao za kazi ili Nchi ipige hatua haraka za Maendeleo.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Kikubwa ninkuwa wamekwenda kushiriki kuokoa, japo yawezekana wako ambao wamekwenda kuonekana.
Anyways, je, wanashirihi kweli kuokoa au baadhi yao wanafanya kile ambacho wangeweza kufanya bila kuwapo kwenye eneo la tukio?
 
Cha kushangaza zaidi wameenda lakini maelekezo bado yanatoka kwa Rais!
Sasa why watumie gharama zote zile alafu hawana solutions??
Aibu!
Yaani viongozi wetu ni mambumbumbu sana na ndiyo maana hawachoki kurogana maana kila mmoja yuko incompetent, anaroga wenzie ili abakie yeye madarakani na kuendelea kuiba hela za umma
 
Kinachotakiwa ni utoaji wa misaada kwa haraka kuliko wao kwenda na kujiwekea mahema wao na kuanza kujadili nini cha kufanya wakiwa eneo la tukio badala ya kujadili kwanza ndio waende huko kuhakikisha utekelezaji wa mazungumzo yao kama unafanyiwa kazi.
 
Back
Top Bottom