Kwanza, poleni sana. Hali hiyo inaleta stress sana kwa wazazi, haswa mama.
Pili, walau ningeona hizo dawa ingetusaidia kutabiri alikuwa anaumwa nini. Hii ni muhimu sana, kama ingelikuwa ya magonjwa ya zinaa tungepata picha dogo kashaanza kuonja. Au ugonjwa mwingine wowote, tungeunganisha dots za hali anayopitia pamoja na ugonjwa na kupata picha ya haswa ya nini kinamsibu.
Tatu, unapaswa kuelewa kuwa huo upole aliokuwa nao ni upweke. Ukweli ni kuwa, watoto wa kiume wanapenda kuchangamana na wanaume wenzao. Bahati mbaya sana familia ina watoto wa kike pekee. Mwanaume aliyebaki ni baba ambaye naye yupo busy.
Nne, mnapaswa kufanya yafuatayo;
a)naamini ya kwamba ninyi ni waamini. Jambo la kwanza muombeeni. Kwa sababu mengine yote yanatimizwa kupitia maombi. Mungu ni Mkuu.
b)fanyeni upelelezi wa wapi anaposhinda na nani na wanachokifanya. Si lazima ninyi muende huko, rafiki zake mkikaa nao wanaweza kuwaletea majibu sahihi na hiyo itawapa picha kamili ya mabadiliko yake.
c)Mhimizeni mzee asipuuze mabadiliko ya dogo. Sawa, kuna mambo yanapaswa kupuuziwa ila si mabadiliko ya ghafla kama hayo. Au labda tayari mzee ana majibu tayari ya nini kinachoendelea. Ashajua huko dogo anafukunyua, kaamua kupiga kimya.
d)Sijafahamu kama huwa wazazi au dada zake mnampa hela. Lakini mpaka kaenda hospital ana hela. Kama hali nyumbani, maana yake ana hela za kula huko alipo. Sasa, sitisheni kumpa hela. Hiyo, itamshikisha adabu na kujirudi. Ataanza kula nyumbani.
e)Ukaguzi wa chumbani uwe wa kila leo. Hii itawasaidia sana kufahamu anachoingia nacho. Kama simu yake mna uwezo, pia ifatilieni (hack) kujua anachokifanya na anaowasiliana nao.
Kila la kheri.