Huwa mnawashughulikiaje watoto wanaokuwa na tabia kama hii?

Huwa mnawashughulikiaje watoto wanaokuwa na tabia kama hii?

Kabisa mkuu......kama mnamhurumia au mnaogopa tafuteni polisi pay him amshikishe adabu huko anakochelewaga......amin amin nakuambia msipomshughulikia now hamtaweza tena later....nina uzoefu na hilo
Sawa Asante kwa ushauri
 
Habari wanajamvi...

Nina imani humu kuna wazazi ambao walishawahi kua na watoto wenye tabia kama hizi naombeni msaada wenu wa mawazo na ushauri unisaidie na mimi.

Binafsi nina mdogo wangu aliyenifuata wa kiume, ana miaka 17...huyu mdogo wangu alikua ni mpole Sanaa, akiwa nyumbani ni mtu wa kushinda ndani mda wote ni kusoma kula na kulala, mara chache sana unaweza kumkuta anaangalia movie hata marafiki zake ni mpaka waje nyumbani kutembelea ndo apige nao story bila hivyo hatoi mguu nyumbani labda aagizwe mahali..

Shida kwamba sikuizi( yani miezi hii hapa miwili) amebadilika sana hadi tunaogopa,, amekua ni mtu wa kuondoka nyumbani bila kuaga na akiondoka asubuhi harudi nyumbani msipompigia simu anaweza asionekane kabisa hadi usiku,, sometimes tukimpigia simu anaweza akapokea halafu akajibu kwa ukali kua tusimfatilie na maisha yake, hataki kula chakula nyumbani, amekua ni mtu wa kufokafoka tu mda wote hadi mama akimuuliza kitu anajibu kwa kufoka tu sio kama alivyokua zamani.

Saizi amefikia hatua kwenda kanisani pamoja na sisi hataki anasema tumuache., alikua anaumwa hakutoa taarifa mpaka anapona na hatuelewi alikua anaumwa nini yani tumefanya tu kustukia kumwona anakunywa dawa, kuna mda alivyoondoka mama akaingia chumbani kwake kukagua akakuta dawa nyingi sana, hata hatuelewi zinatibu ugonjwa gani., baada ya mama kumuuliza alikua mkali sana na ametupigia marufuku kuingia chumbani kwake hata kama ni kufanya usafi.

Ajabu ni kwamba tukimuelezea baba tabia za huyu dogo sikuizi wala hata hatilii maanani anasema tu muacheni kama alivyowaambia mumuache...hasa tatizo ni lipo kwa mama amekua na wasiwasi sana na mabadiliko ya huyu mdogo wangu yani pressure inampanda mda wote, akijaribu hata kukaa nae chini kuongea nae dogo hataki kumskiliza yeyote zaidi ni anakua mkali ukimsogelea jirani anaweza akupige makofi...

Naombeni msaada wenu wa mawazo ili niweze kumsaidia huyu mdogo wangu maana napata shida sana kumuona mama akiwa na wasiwasi mda wote 🙏🏼

Umri huo asipopata mtu wa kumisimamia na kumuongoza ni hatari sana. Maisha yake yote yanawezaharibikia hapo

Jenga utafiki na ukaribu nae bila kumlazimisha akueleze shida zake. Ongea nae, mpe uhuru wa kutoa mawazo yake bila kumkatishakatisha, muonyeshe kwamba unamjali na una uwezo wa kumuelewa, mwache afanye mambo na umsikilize zaidi ya wewe kuongea...... utajua mengi
 
Dogo kaanza kuwa na misingi yake....

huyu asijekuwa anasoma vile vitabu vya GANGSTERZ
 
Hana tatizo muacheni aushi maisha yake.. yaan ni hivyo tu msimfanye km katoto hicho ndicho kinachomchukiza kwa hio mwacheni aishi anavyotaka
Sawa tutajaribu, ila ni uhakika kwamba tukimuacha kama alivyo ndo atabadilika?
 
Itabidi tufanye hivyo..shida ni nani sasa wakumpa hizo stiki maana baba naona kashajitoa hataki stress, mama ndo hawezi kabisa kuchapa mtu ,, labda police
Muache aishi maishi yake polisi kufanya nini? Wewe una miaka 21 yeye 17 mnapisha miaka 4 sasa shida ipo wapi kwani wewe huna anaekubandua nyinyi wanawake na watoto wa kike kufuatilia ndugu zenu wa kiume mnakuaje au unataka akubandue wewe?
 
Tatizo la kisaikolojia baada ya kunyanyaswa kijinsia yaani kuna mtu alitumia advantage ya upole wake na kumuingilia kinyume na maumbile sasa reaction ndio hiyo!!!

Hiyo baba wa nyumba ndio mshukiwa wa kwanza hawezi kuona kawaida kijana akiwa Katika hali hiyo!!!

Hiyo ni defensive mechanism!

Ipo SIKU atafunguka mkimpatia mwanasaikolojia mzuri!!!

Mawazo huru haya toka kwa fikra huru!

Sorry to write that!!
Asante kwa ushauri wako pia mkuu...
 
Umri huo asipopata mtu wa kumisimamia na kumuongoza ni hatari sana. Maisha yake yote yanawezaharibikia hapo

Jenga utafiki na ukaribu nae bila kumlazimisha akueleze shida zake. Ongea nae, mpe uhuru wa kutoa mawazo yake bila kumkatishakatisha, muonyeshe kwamba unamjali na una uwezo wa kumuelewa, mwache afanye mambo na umsikilize zaidi ya wewe kuongea...... utajua mengi
Sawa nitajaribu kufanya hivyo...shida ni kwamba hataki kuongea wala kumskiliza yeyote yule 🤔
 
Tatizo la kisaikolojia baada ya kunyanyaswa kijinsia yaani kuna mtu alitumia advantage ya upole wake na kumuingilia kinyume na maumbile sasa reaction ndio hiyo!!!

Hiyo baba wa nyumba ndio mshukiwa wa kwanza hawezi kuona kawaida kijana akiwa Katika hali hiyo!!!

Hiyo ni defensive mechanism!

Ipo SIKU atafunguka mkimpatia mwanasaikolojia mzuri!!!

Mawazo huru haya toka kwa fikra huru!

Sorry to write that!!
Muongo mkubwa alafu unachokiandika hapa umemtukania baba yake mzazi huyu mleta mada kwa kumuita mfiraji Jambo ambalo huna ukweli nalo, acha upotoshaji kijana
 
Naweza kukisia. Inaonekana alipokuwa anakaa nyumbani sana mlimwandama kwa masimango na kila aian ya kero kuwa ni kwa nini hatoki kama wanaume wengine. Sasa akaona atoke ili awaonyeshe kuwa na yeye amekua. All in all wewe na mama yako inaonekana ni wale wanawake wanaofuatilia mambo ya watoto wao wa kiume na kutaka kuwa-control. Hii inaonyesha hata ulivyosema mnaingia chumbani kwake. Mimi ni mwanaume na nilipokuwa kwenye huo umri nilipata kero kama hizi. Mama yangu na dada zangu wakawa kama wanataka kuingilia maisha yangu na kuniona kama bado ni mtoto wa chekechea. Tulikuwa tunagombana sana kwani mra nyingi nilikuwa nataka kuwaonyesha kuwa sitaki kuendeshwa kama gari bovu. Ushauri wangu ni kuwa achaneni na kutaka kum-control maisha yake. Wewe anakufuatilia? Komeni kabisa wewe na mama yako. Miaka 17 bado mnataka kumfanya kama mtoto wa chekechea?
Huu ushauri akiuona dogo, atakwambia uagize pepsi mahali atalipia na huu ndio ukweli.
 
Kwahiyo tumfanyaje ili akae sawa..au ndo tumuache tu atabadilika mwenyewe kama wengi wanavyosema🤔
Atabadirika mwenyewe kwani wewe ulizaliwa unatembea si ulianza kukaa au unataka aruke stage za ukuaji awe zuzu hapo nyumbani kwenu azeeke hapo hapo?
 
Muache aishi maishi yake polisi kufanya nini? Wewe una miaka 21 yeye 17 mnapisha miaka 4 sasa shida ipo wapi kwani wewe huna anaekubandua nyinyi wanawake na watoto wa kike kufuatilia ndugu zenu wa kiume mnakuaje au unataka akubandue wewe?
Jamani 😃😃😃, mbona unanifokea sasa🤨
 
ukiona mtoto ameanza kukujibu, jua kuna tabia mbaya ameanza kuifanya. na hapo sio kwamba tu anawezakuwa ana makundi mabaya, anaweza kuwa anavuta hadi bange, ndio maana haogopi. kwenye mabange ndiko kwenye mabasha na mashoga. haow avuta bange na unga wengi wakilewa huwa wanaingiliana wao kwa wao huko, kuweni makini. inakuwaje kijana wa umri huo anapotea asubuhi hadi jioni hamjui ameenda wapi? na ukimuuliza anajibu hivyo? au baba anajua wapi huwa anakuwa ameenda manake familia zingine huwa zinaoperate kiroho, si ukute kachawi bila ninyi kujua hako. watoto wengi tu wanaingiziwa uchawi na ushirikina kwa kupitia wenzao mashuleni nahuko wanakocheza.
 
Back
Top Bottom