Huyo mwamba alishawahi kuwa mnunua karanga Kahama leo ni Ltn Col wa RDF

Huyo mwamba alishawahi kuwa mnunua karanga Kahama leo ni Ltn Col wa RDF

Kwa wafanyabiashara wa karanga kutoka Kahama kwenda Rwanda, hakika watakuwa wanamfahamu mwamba huyo.

Nimeshangaa kumuona ndani ya vazi la kazi la jeshi la nchi fulani tena kama Lt Col!

Tunaposema miji kama Ngara, Nyakahura, Nyakanazi, Runzewe, Ushirombo, Kahama, Kagongwa, Isaka, Shinyanga, Mwanza, Tabora, Singida na karibia Nchi nzima wameenea, muwe mnatuelewa!

Ama kweli vita vya medani, ni hatari!

View attachment 2683680
Hilo halizuiliki na Wala sio ajabu duniani kote iko hivyo hata sisi tuna majasusi wengi Sana wako kwenye hizo inchi wanafanya yao na wengine Wana maduka kabisa kwa hiyo Hilo lisikuumize kichwa.hatuko kiboya Kama unavyofikiria
 
Kote huko na wapelelezi wengine hasa wanyarwanda ni madreva wa malori yaendayo bandarini kuchukua mizigo kutoa dar to rwanda, na wengine maspy wanapiga ruti za makaa ya mawe mbinga to kigali haya yote hufahamika muda mrefu sana , sema hua nikileta uzi hapa wanafuta faster kuna siku niliwasema sana uhamiaji hapa wakanipiga na ban
Wewe unafikiri mpaka umeyajua wewe idara zetu haiwajui haya hata ukimjua unamfanya nn?yuko na kifuniko
 
Usishangae hata risasi zilikua zinaingizwa kama mafuta ya kula, ndoo kubwakubwa za lita 20 , zinakua cleared kama mafuta yakula kumbe wazee wanasafirisha mizigo yao enzi hizo na mara nyingi ngoma zilisafirishwa kwa treni hadi isaka au kigoma ndio mizigo inasambazwa kwa wenyewe iwe waasi au vinginevo na agent aliekua anafanya clearance ya mizigo ya aina hiyo alilipwa pesa ndefu, dunia ina mambo sana hujiulizi waasi hupata wapi silaha nzito, na vifaa vya kijeshi?
Dili za wakubwa hizi
 
UVCCM na ndugu zao CCM wako busy kuhakikisha 2025 tunatoboa tena.

tuendelee kuishi kwa historia ya 1978 enzi za vita za ukombozi tu, kukicha watakuwa pale posta na maeneo ya Seaview wanatuchora tu.
Na kutishia watu nyau. Ukiwakosoa tu, basi utawaona wanavyotokwa na macho. Wenzao wako bisy na vita ya kiuchumi, wao wako busy kutishia watu nyau.

Hovyo kabisa ccm na watoto wao uvccm.
 
Kwa wafanyabiashara wa karanga kutoka Kahama kwenda Rwanda, hakika watakuwa wanamfahamu mwamba huyo.

Nimeshangaa kumuona ndani ya vazi la kazi la jeshi la nchi fulani tena kama Lt Col!

Tunaposema miji kama Ngara, Nyakahura, Nyakanazi, Runzewe, Ushirombo, Kahama, Kagongwa, Isaka, Shinyanga, Mwanza, Tabora, Singida na karibia Nchi nzima wameenea, muwe mnatuelewa!

Ama kweli vita vya medani, ni hatari!

View attachment 2683680
Paul Kagame kwenye masuala ya ujasusi ni mbobevu sana, ameiva haswa kwenye taaluma hiyo. Siyo mtu wa kumchezea hovyo hovyo, kwenye nchi yetu ana 'watu wake wengi sana'. Nchi pekee ndani ya Afrika Mashariki ambayo anaihofia kwamba inaweza kumharibia maslahi yake ni Tanzania, ndio maana amewekeza sana katika kuifanyia ujasusi, nchi zingine zilizobaki watawala wa huko ni rafiki zake, kwa hiyo hana hofu nazo sana.
 
Mimi nilimfahamu zamani kama mtu wa upelelezi wa Rwanda, na nilikua nakutana nae sana bijampora na moclay, na niliwahi kuleta uzi hapa jukwaani kua maspy wa Uganda, Rwanda hua wanaingia Tanzania kama wafanyabiashara, na niliwahi kutoa hadi ushahidi kua Rwanda, uganda na burundi serikali hutoa mamilioni ya pesa kwa baadhi ya wanausalama wao na kuingia nchini hadi vijijini kununua mazao hasa ya chakula ili kulinda usalama wa chakula kwenye nchi zao na kama ukiacha kahama wanausalama hao wako hadi ifakara, kasulu, mpanda, sumbawanga, kibondo, mpeta, mbeya, kibaigwa na maeneo mengine mengi lakini huingia kama wajasiliamali, huo ndio ukweli
Mpeta Wana Kijiji Kabisa
 
Tz is very known compared to them all ila ni kwel TZ tuna viongozi wapumbavu haswaaaa
Ilikuwa juu sana. Lakini sasa ni kama yatima. Viongozi na watanzania wengi wanathamini zaidi ulaji na kujineemesha kibinafsi kuliko kujishughulisha na mustakabali wa taifa.

Huko nje ni wazee hasa wenye kumbukumbu za Nyerere ndio wanaikumbuka Tanzania na kuithamini. Vijana wengi duniani hawaijui - hata ilipo kijiografia; wanazifahamu vizuri zaidi Kenya, Zanzibar na Rwanda. Tembea, ulizia usikilize majibu. Utashangaa.
 
Ndio dunia ilivo kuna mbinu nyingi za kufanya upelelezi kwa mfano ukiwa kigali kamwe huwezi kudivert call! Lakini ukiwa bongo divertion unafanya kama kawaida, ndio maana ulisikia magufuli hata samia wanawasifu ma IT wa Rwanda haikua bahati mbaya kabisa, kwenye teknolojia jamaa wako mbali, hata rekodi za mazungumzo ya simu ya viongozi wako yalichukuliwa kutokea Rwanda then magufuli akamwagiwa ndio akachanganyikiwa
Unawasifia kurekodi sauti kwa kutumia software za wa Israel?
Mbona hiyo mitambo na software zipo hapa nchini siyo habari ya kificho.
 
Kwa wafanyabiashara wa karanga kutoka Kahama kwenda Rwanda, hakika watakuwa wanamfahamu mwamba huyo.

Nimeshangaa kumuona ndani ya vazi la kazi la jeshi la nchi fulani tena kama Lt Col!

Tunaposema miji kama Ngara, Nyakahura, Nyakanazi, Runzewe, Ushirombo, Kahama, Kagongwa, Isaka, Shinyanga, Mwanza, Tabora, Singida na karibia Nchi nzima wameenea, muwe mnatuelewa!

Ama kweli vita vya medani, ni hatari!

View attachment 2683680
Hata sisi watu wetu wengi wametapakaa kwenye hizo nchi, ni wajasiriamali, ni maderva taxi, ni Mama Ntilie nk..ni kawaida nchi kupelezana
 
Asijali, hata hapo kwa PK wako kibao, ni vile tu sisi ni waoga waoga tu kwa kila kitu,
pale Simba Supermarket mbona wanakula bia daily, wagogo kibao wanaongea Kinywaranda pure na sura zilishaanza kufanana na kule

Arovera kua na amani mkuu, nchi iko salama
Ishu huyo spy yuko ktk misheni gani?
 
Back
Top Bottom