Huyu hakuwa raia mwema, haiwezekani umpige askari kwa teke na ngumi

Huyu hakuwa raia mwema, haiwezekani umpige askari kwa teke na ngumi

Bahati nzuri ipo video original ikionyesha tangu mwanzo wa tukio ila ajabu Muliro kachukua kipande kidogo tu na kusema askari kashambuliwa ila hawasemi wao ndio walianza kushambulia raia wasiokuwa na silaha.

Katika video ambazo Muliro hakuonyesha mojawapo ni ya yule kijana anaitwa Mahinyila huyu ni wakili na alikuwepo mahakamani ila video yake inaonyesha polisi watatu wasio na sare wamemvamia na wanataka kumkamata anapowahoji wao ni akina nani na wanamkamata kwanini hawajitambulishi bali wanazidisha kutumia nguvu je ni sawa mbona mleta mada analeta double standard?
Weka link mkuu
 
Unaongelea ulipoangukia sio ulipojikwaa.Umpige askari utegemee uachwe?Hata Marekani mshambulie askari uone utafanywa nini.
Hata huko Marekani askari akitumia nguvu kubwa kumdhibiti raia bado ni makosa.
 
Mahilinya alikuwa ana resist kuwa arrested.Hakuna double standard.Mahilinya aliwatusi askari na waliojaribu kumweka chini ya ulinzi akawa ana resist.
Ukienda kumfanyia mtu arrest kuna vitu vitatu unatakiwa kama polisi ufanye hakikisho.

1.Jitambulishe

2.Elezea sababu ya kumkamata mhusika.

3.Hakikisho la kupewa nafasi ya ndugu kujulishwa na kupata wakili.

je katika video hiyo hapo husikii wakili akiwauliza wao ni akina nani na wanamkamata kwa sababu gani?

Husikii hapo anawauliza mimi niko kazini kwangu sababu yeye ni wakili na yuko mahakamani wanamkamata kwa nini?


View: https://youtu.be/OoFs1hkQT0w?si=qpQk8z2fHa5mKDv8
Lema alijaribu kumuombea kwamba aachwe kwa hiyo ina maana Lema alikuwa anajua ni askari waliovaa kiraia.Alipoona jamaa hataki kuwa arrested akajiondokea zake.Mwisho akasarenda na kupelekwa Polisi.
Okay polisi wamesema kosa lake lilikuwa ni nini ?

Na kwanini Muliro alipotoa press hili tukio hakuliongelea badala yake akajificha kwenye kichaka kuwa wanachama wa CHADEMA walikuwa wanafanya vurugu?
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Nguvu kubwa ni kama hiyo hapo kwenye video ya huu uzi.
Na Marekani kufanya haimaanishi ndio sahihi, kwanini unaihusudu sana hiyo Marekani?
Si ndio mnapokimbilia mkidai mnaonewa.The land of the free.Leo hamupataki tena mkitolewa mifano kutoka huko.
 
Hata huko Marekani askari akitumia nguvu kubwa kumdhibiti raia bado ni makosa.
Na kwa kumsaidia tu huyo jamaa askari wa Marekani wanazo bodycam kwenye combat yao hii pia hurekodi tukio mwanzo hadi mwisho hivyo kama askari wa Tanzania angekuwa nayo tungeweza kusikia hadi walichokuwa wanazungumza hapo polisi muda wa tukio .

Uwepo wa bodycam ndio unafanya mtu atende haki na hawachukui rushwa maana anajua kila analofanya linarekodiwa na rekodi zote hutumwa kule kwenye kituo husika.

Mfano hili tukio ni la siku za karibuni tu na lilikuwa recorded na bodycam, siku polisi wa Tanzania wakiwa na hii itawasaidia kufanya kazi kwa uweledi.


View: https://youtu.be/qrBL_IAoPqk?si=NeLXY0tmLzZ-PbL7
 
Sawa mkuu, nimezicheki na pia nimeona kuna nyingine hii inaonesha angle nzuri zaidi na mtiririko mzuri


View: https://youtu.be/jrBaB65FuK4?si=4O7lX6mc0GO8b-9j

Naam, sasa hii video polisi hawataki kuionyesha wao wamekata kipande kidogo tu cha huyu jamaa kumpiga askari ilhali katika hiyo timua timua jamaa wala hakua na nia ya kushambulia bali alikuwa anarudi nyumba ghafla askari kamtandika.
 
Huyu jamaa anampiga Askari ni mwenzao wanataka tu kubalance unyama wao wa kupiga raia bila hatia
 
Jamaa aliponzwa na mob mentality.Akadanganyika na kelele za "Mtatuua mtatuua".Walipoambiwa watawanyike akabaki na kutupa teke ikabidi askari wajibu mashambulizi.Au wewe ulifikiri hivyo virungu ni mapambo?
 
Back
Top Bottom