Huyu hakuwa raia mwema, haiwezekani umpige askari kwa teke na ngumi

Huyu hakuwa raia mwema, haiwezekani umpige askari kwa teke na ngumi

Naam, sasa hii video polisi hawataki kuionyesha wao wamekata kipande kidogo tu cha huyu jamaa kumpiga askari ilhali katika hiyo timua timua jamaa wala hakua na nia ya kushambulia bali alikuwa anarudi nyumba ghafla askari kamtandika.
polisi wanatafita mbinu ya kujitetea japo mzani haupo upande wao
 
Bahati nzuri ipo video original ikionyesha tangu mwanzo wa tukio ila ajabu Muliro kachukua kipande kidogo tu na kusema askari kashambuliwa ila hawasemi wao ndio walianza kushambulia raia wasiokuwa na silaha.

Katika video ambazo Muliro hakuonyesha mojawapo ni ya yule kijana anaitwa Mahinyila huyu ni wakili na alikuwepo mahakamani ila video yake inaonyesha polisi watatu wasio na sare wamemvamia na wanataka kumkamata anapowahoji wao ni akina nani na wanamkamata kwanini hawajitambulishi bali wanazidisha kutumia nguvu je ni sawa mbona mleta mada analeta double standard?

Iangalie video original hapo angalia hapo polisi walichoanza kukifanya je hapo polisi wanaweza kutueleza huyo jamaa kosa lake ni nini hadi aanze kupigwa ?


View: https://youtu.be/dJG62_0i7Pc?si=WayC7NM0B0jVeBB1

Video ya pili hii hapa ni advocate Mahinyila na polisi wasio na sare mbona hii Muliro haitolei ufafanuzi?

Kosa la huyu wakili kukamatwa ilikuwa ni nini?


View: https://youtu.be/OoFs1hkQT0w?si=ORsNS1oPQLdo7DAI

Nyie mko na wahuni tu.
Huyo wakili kaambiwa mwanzo tu aondoke akawa anabisha, hata Lema kaondoka baada ya kumtetea ye kabisha ndio wakakabana nae huko mbele.
Labda hata sio wakili, kavaa suti tu ya sh 5000 anajileta kimbelembele wakili msomi wakakabana nae.
Ni kosa dogo tu la exposure.
Heshimu kazi za watu utaheshimiwa pia.
Hao jamaa wakabaji hawako secure, wanahisi kudharauliwa, kupuuzwa na watu wasio na elimu.
Ndio mana wanatumia miguvu.
Angeondoka zake asingeguswa
 
Mahilinya alikuwa ana resist kuwa arrested. Hakuna double standard.Mahilinya aliwatusi askari na waliojaribu kumweka chini ya ulinzi akawa ana resist. Lema alijaribu kumuombea kwamba aachwe kwa hiyo ina maana Lema alikuwa anajua ni askari waliovaa kiraia. Alipoona jamaa hataki kuwa arrested akajiondokea zake. Mwisho akasarenda na kupelekwa Polisi.
Yeah, Lema alikuwa smart japo wana CDM wanamoinda. Licha ya usela wake lakini jamaa kuna namna yuko civilized. Anajua mipaka yake - nadhani kukaa Canada kumemsaidia. Mahinyila alijaribu kutengeneza un necessary scene. Lema aliuona mkenge akajiondokea....
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Nyie mko na wahuni tu.
Huyo wakili kaambiwa mwanzo tu aondoke akawa anabisha, hata Lema kaondoka baada ya kumtetea ye kabisha ndio wakakabana nae huko mbele.
Labda hata sio wakili, kavaa suti tu ya sh 5000 anajileta kimbelembele wakili msomi wakakabana nae.
Kigezo gani umekitumia kusema kulikuwepo na wahuni?

Huyo kijana aliambiwa aondoke kwa sababu zipi , kumbuka hiyo ni open court , huyo kijana ni wakili pia ni mwanachama na kiongozi wa CHADEMA ambaye alihudhuria kesi sasa polisi waliona anayo threat ipi hadi wamfukuze?

Issue ya Lema kuwepo hapo na kuacha kumsaidia haina uhusiano wowote na ushenzi waliokuwa wanafanya hapo polisi.

Na ndio alichokisema Mello namna hiyo hiyo ndio waliingia ofisi za JF wanazuiliwa na mlinzi getini watoe maelezo wao wanalazimisha na kutumia nguvu kuingia Mello muda huo anawaona kwenye CCTV nadhani siku za usoni ushahidi kama huu itabidi utumike ili watu waache kutumia nguvu pasipo na uhitaji.



Ni kosa dogo tu la exposure.
Heshimu kazi za watu utaheshimiwa pia.
Hao jamaa wakabaji hawako secure, wanahisi kudharauliwa, kupuuzwa na watu wasio na elimu.
Ndio mana wanatumia miguvu.
Angeondoka zake asingeguswa
Huyo kijana amewadharau wapi polisi?

Ukimsikiliza kwenye hiyo video anawauliza nyie ni akina nani na mnataka nini?

Kama ingekuwa tangu mwanzo wanalazimisha kumtaka atoke mahakamani na wangezingatia taratibu sidhani kama asingewakubalia.

Pia serikali kuingilia mahakama ndio imewafikisha hapo , hii kesi ingekuwa inarushwa live ingepunguza msongamano wa watu hapo ila wanaogopa kesi isiwe live maana copy zitabaki YouTube na hata ambao hawakuona muda inaendelea jioni wataangalia hiyo itambeba Lissu huku watu wakipuuzia matamasha ya wasanii yaliyopewa jina la kampeni anayoendelea nayo Samia.
 
Huyo amelipa kisasi anakuaje sio raia mwema kwani raia wanakatazwa self defense hii itufundishe haya mambo yana mwisho watu walipopigwa Kisutu wale walikua Polisi wema? Hizo ni hisia zakuchoshwa nanuonevu nakuona liwalo na liwe tu
 
Huyo amelipa kisasi anakuaje sio raia mwema kwani raia wanakatazwa self defense hii itufundishe haya mambo yana mwisho watu walipopigwa Kisutu wale walikua Polisi wema? Hizo ni hisia zakuchoshwa nanuonevu nakuona liwalo na liwe tu
Sasa kama alikuwa kwenye so called defence malalamiko ya nini?Ukimpiga Askari utapigwa.
 
Back
Top Bottom