Huyu mdada nampenda nimetumia njia zote kanikataa sasa imebaki njia moja tu

Huyu mdada nampenda nimetumia njia zote kanikataa sasa imebaki njia moja tu

Nimesoma nae kuanzia form1 hadi form4 pia tukakutana chuo, kipindi chote hicho nilikuwa namtongoza kwa njia mbalimbali kama kumpa zawadi na hongo mbalimbali cha ajabu nilipo muambia ukweli kuwa namtaka akanikataa

Wakati tupo o-level nilijua kwakuwa bado tupo na safari ya masomo lakini tulivyokutana chuo mambo yakawa yale yale. Boom langu kala la kutosha na mambo mengi nimemfanyia lakini malipo yake ni kunikataa hii sitakubali wala kukata tamaa

Sasa mbinu iliyobaki ni kwenda kwa mtaalam nikamloge najua ni hard way but the only way
1755538422275.jpeg
 
Kwanini anapokea kumbe hanitaki na wakati mwingine akiwa na shida ananiomba ila mimi kiroho safi nampa ila malipo yake ni kunikataa siku zote huku ni kuchezea hisia zangu sitakubali
Ok, endelea boss
 
Ving'ang'anizi kama nyie mwisho wa siku mnapigwa matukio ya kutosha mnaishia kujiua
 
Huna haja ya kwenda kwa mtalaamu mkuu kuendelea kupoteza tu gharama
Chukua hii upate tu ukucha wa kunguru mvizie anakojoa akimaliza we nenda weka ukucha huo kwenye mkojo niamini mimi huyo atakuwa wa kwako milele
Si anakojolea chooni mkuu nitauwekaje ukucha au humohumo kwenye sink
 
Ving'ang'anizi kama nyie mwisho wa siku mnapigwa matukio ya kutosha mnaishia kujiua
Siwezi kujiua ila hii mbinu nakuhakikishia atakuja mwenyewe na itakuwa zamu yangu kulinga
 
Mkuu, jaribu mbinu hii:
Mtafute au mchombeze demu mwingine na ujimwambafai naye mbele ya huyo dada anayekutesaga- Halafu uje utoe majibu baadae.
Ni mbinu isiyo shindwa. Nimeitumia sana Kwa mafanikio makubwa- haijalishi ni mwanamke wa nchi gani-
Atakutafuta mwenyewe na kukutunuku kimasihara. Wing lady - wanakusaidiaga sana kuwalamba hawa kichwa ngumu.
Wanawake wengi kwa asilimia kubwa sana wana kitu kinaitwa FOMO- fear of Missing out na ukiijua kuitumia, utawachakata hadi uwakinai
 
Back
Top Bottom