Huyu mhalifu wa Selander alipaswa kukamatwa, siyo kuuawa
Mtu ana silaha na anaua watu .Kwa nini mmuache ?By the way huwa hawasemi hawa wala kutoa ushirikiano kwa polisi. Wanakula yamini hawa magaidi. Bora wameliua tu.
Thank you 👏
Mtu ameua askari wawili na mlinzi, anaendelea kurusha risasi ovyo na kuhatarisha maisha ya watu wengine, wewe unasema wamkamate? Fikra nyingine ni za kijinga kabisa. Tena wangemuua kwa silaha kubwa ya kuharibia vifaru vitani ili asibakie hata kidole!
 
Upelelezi wa Moto pale msamvu mpaka leo kimya

Upelelezi wa Moto pale k'koo mpaka leo kimya

Upelelezi gani tunnaousubiri Zaid ya kutupotezea muda

Kweli na hili litapita tu
Basi acha tubuni na kuamini mahakama yetu ya humu
Wao waache wale hela zaupelelezi
 
Hahahaaa nimecheka adi najishtukia siyo kwamba kilichotokea ni kizuri ila tumezidi ujuaji usio na maana kwa kweli,kweli kila mmoja Ana haki ya kutoa maoni yake kwa umma ila jamani hebu hata tufikirie kidogo basiii kuhusu hili tukio siyo kuandika ugoro jamani eti asingeuawa hiiii watu Wana masihara sanaaaa...kilichofanyika ni sahihi kabisa pia tukio hili liwe ni funzo na salamu kwa polisi nchi nzima kuwa Mambo yanabadilika wasikariri na kujisahau kabisa pia vilevile wachague vijana sahihi ijapokua tunajua ni ngumu...
 
Polisi walipaswa kumtia nguvuni huyu mtu aliyekuwa na bunduki huko Kinondoni maeneo ya Selander. Lakini kwa kukosa weledi na kwa vile polisi Wana uoga uliokithiri wakamfyatulia risasi na kumuua.

Sasa watakosa taarifa muhimu kutoka kwa mhalifu huyu mfano:
  • Ni nani?
  • Katumwa na nani?
  • Yuko na akina nani (wako wangapi)?
  • Nini dhamira yao?
  • Nini chanzo cha wao kufanya hivi?

Kwa kumuua hawajatatua tatizo.

Polisi wetu Wana ujasiri wa kuwakamata CHADEMA tu.

Kanda maalumu ya polisi jijini Dar imeshindwa vipi kumkamata mtu huyu mmoja tu??
Sina utaalamu wa kijeshi lakini uzoefu unaonesha kwenye tukio kama lile dawa huwa ni kumfyeka mhusika. Hata Marekani ambako wanaongoza kwa visa vya aina hii, wadunguaji hummaliza kabisa mhusika. Ninadhani kuna sababu za msingi kufanya hivyo. Jamaa anakuwa na mashine heavy kama huyu wa leo hapa Tz,mkijidai mnamvunja mguu, bado ana mashine ,ataendelea kuachia mchekeche maana hamjua ana uwezo wa aina gani.
 
Huyo jamaa alikuwa Chizi asiekuwa na mafunzo yeyote huwezi kukaa peupe vile huku umeibagala manati hadharani

Hata kama ikija kujulikana kuwa ni Gaidi lakini ana uchizi vilevile.
Hawezi akawa chizi akawa na uwezo wa kuwaambia wapita njia wengine nyie piteni, tu mimi nawataka polisi tu?!!angekuwa chizi kweli maafa ambayo angesababisha yangekuwa makubwa sana, !!kuna kitu tu, tena dhidi ya polisi!!
 
Hawezi akawa chizi akawa na uwezo wa kuwaambia wapita njia wengine nyie piteni, tu mimi nawataka polisi tu?!!angekuwa chizi kweli maafa ambayo angesababisha yangekuwa makubwa sana, !!kuna kitu tu, tena dhidi ya polisi!!
Uchizi uko wa aina nyingi sana Bro,unaweza ukawa na Paranoid dhidi ya watu waliovaa uniform.
 
Behind the scenes.
FB_IMG_16299278772992628.jpg
 
Hii ni failure kwa jeshi la polisi,jambazi au kama wanvyotaka wengi tuamini kuwa ni gaidi ,inakuwaje jamaa amesimama na walikuwa na uwezo wa kumchapa risasi za miguu na kumkalisha chini,huenda wangemkamata wangejua mengi sana ,iliyobaki sasa ni kubambikiza tu.
 
Ni punguani peke yake ndiye anaweza kuamini kuwa Tanzania ina Polisi.Kile ni kikundi cha vichwa vya wendawazimu ambao kazi yao ni kudhulumu,kupora mali za uma na kuhakikisha kuwa CCM inaendelea kubakia madarakani.
 
Ni punguani peke yake ndiye anaweza kuamini kuwa Tanzania ina Polisi.Kile ni kikundi cha vichwa vya wendawazimu ambao kazi yao ni kudhulumu,kupora mali za uma na kuhakikisha kuwa CCM inaendelea kubakia madarakani.
Tuache mihemko! Hii inaonesha kuwa kurudisha polisi katika mafunzo ya shabaha hakuepukiki
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Point. Au hata angepigwa za miguu tu. Na aliyemuua ametumia risasi kama 5-8 hivi kupatia shabaha! Wakati jamaa mwenyewe alikuwa amesimama kama mti tu.
Kimsingi hata ile lisasi iliyo muangusha ilikua ni bahatiii tuuu.na jamaa asingetoka katika kile kibanda basi naaamini makontena yoote ya police tanganyika yangeisha bila kumpiga hata moja[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Ukisikia mikwara yao kwenye vyombo vya habari utadhani watuu kweli. Ndio maana hata kwa lissu walipiga risasi elfu moja kwenye gari.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Mtu ana silaha na anaua watu .Kwa nini mmuache ?By the way huwa hawasemi hawa wala kutoa ushirikiano kwa polisi. Wanakula yamini hawa magaidi. Bora wameliua tu.
Huyu jamaa aliishiwa risasi akatoka kwenye kibanda akajisalimisha kwa kunyoosha mikono juu . Alipaswa kukamatwa Kwanza ahojiwe ndo auawe.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Tuache mihemko! Hii inaonesha kuwa kurudisha polisi katika mafunzo ya shabaha hakuepukiki
Warudishwe katika mafunzo ya shabaa au katika mafunzo ya kuikimbia dhuluma na kuiba mali za uma?Unaelewa kuwa hawa polisi wameuawa baada ya kupora madini ya Bwana Hamza?Unaelewa kuwa hawa ambao unawaita kuwa ni Polisi hapa Tanzania ni vibaka na majambazi?
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Back
Top Bottom