Huyu mhalifu wa Selander alipaswa kukamatwa, siyo kuuawa
Achana na hizo stori za ufaransa... Tukio hilo la ufaransa lilikuwa na mazingira yake, tuzungumzie hili la leo!. Jamaa licha ya pistol aliyokuwa nayo bado alikuwa na SMG mbili, moja inaning'inia shingoni nyingine anaitumia kulenga kila anachokiona.... kumbuka SMG ina risasi thelathini na ameishaua watu wanne wewe unasema aachwe aue watu wapatao 30, aishiwe risasi wewe ndio ukamkamate?..... Wewe utakuwa askari kweli au askofu??.
Askari wenye akili wangepiga risasi sehemu muhimu za yule mhalifu ili kumdhoofisha kama mikono, miguu ama mabega. Mwenyewe angenyoosha mikono.

Walichofanya hawa polisi wetu ni uzwazwa
 
Uwezekano wa kuvaa tisheti ya vilipuzi huwezi kuurule out. Hili utaliona kwa wale askari walioenda kuchukua silaha zile baada ya jambazi kuanguka chini walikuwa katika tahadhari kubwa.
Walikuwa wana-dramatize tu ili waonekane wanajua kitu halafu kqmera za tv ziwachukue. Hakuna kitu pale.

Polisi wetu ni wachovu
 
Wamemuua kifo chepesi sana huyu bwana walitakiwa wamkamate akiwa hai wapate taarifa kutoka kwake kupeleleza anaishi wapi ndugu jamaa na maraiki asingetia ushirikiano wanammaliza huko huko tunapewa taarifa kauawa akipatiwa matibabu. 24 season iliniharibu saba😂😂😂
kitendo cha kumuona tu....kama kweli ni gaidi maiti yake itazungumza...hivi sasa nina uhakika kuna watu wanazungumza nae huyo maiti...maiti huwa zinaongea na hii itaongea na kutapika nyongo yote...!
 
Jamaa wa Uvccm
IMG-20210825-WA0032.jpg
 
Polisi walipaswa kumtia nguvuni huyu mtu aliyekuwa na bunduki huko Kinondoni maeneo ya Selander. Lakini kwa kukosa weledi na kwa vile polisi Wana uoga uliokithiri wakamfyatulia risasi na kumuua.

Sasa watakosa taarifa muhimu kutoka kwa mhalifu huyu mfano:
  • Ni nani?
  • Katumwa na nani?
  • Yuko na akina nani (wako wangapi)?
  • Nini dhamira yao?
  • Nini chanzo cha wao kufanya hivi?

Kwa kumuua hawajatatua tatizo.

Polisi wetu Wana ujasiri wa kuwakamata CHADEMA tu.

Kanda maalumu ya polisi jijini Dar imeshindwa vipi kumkamata mtu huyu mmoja tu??
Mbona nasikia alikuwa ni Mwendawazimu? Je, kwa Uwendawazimu wake huo Ukimhoji unaweza kupata Majibu ya Kutosha?
 
Mbona nasikia alikuwa ni Mwendawazimu? Je, kwa Uwendawazimu wake huo Ukimhoji unaweza kupata Majibu ya Kutosha?
Hicho ni kichaka tu kimeundwa na polisi ili kuuficha ujinga wao waliofanya wa kumpiga risasi na kumuua mhalifu kabla ya kumhoji.
 
Point. Au hata angepigwa za miguu tu. Na aliyemuua ametumia risasi kama 5-8 hivi kupatia shabaha! Wakati jamaa mwenyewe alikuwa amesimama kama mti tu.

Halafu anatokea mtu anasema polisi wa Tanzania hawakosei. Wanapiga 2 au 3 tu! Leo sasa tumejionea. Na ni jambazi mmoja tu yule, ila mirisasi imewatokaaa. Sasa tuamini nini kwenye issue ya Lissu!
 
Waswahili tunapewa picha na habari tunaitangaza sisi kama kweli vile
Kwa kutengeneza story hatujambo
Tumeambiwa tusubiri upelelezi ila tayari tunajua kila kitu na hata movie tunaweza kutengeneza ila baadae tukafanya editing kidogo
 
Vita ni vita mbona hufikilii askari wawili waliofariki
Askari kufa kwenye pambano is not a choice rather is a part and outcomes of their job. Na kwamba kama ikilazimika kufa na ikatokea hivyo, basi hiyo si ajabu....

Lakini kuua mtu ambaye anesababisha vifo vya askari badala ya kutumia kila njia salama kumkamata ili kujua sababu zake za kuua na aseme waliko wenzake, ni kukosa professionalism katika jukumu la kazi yako..!!

Kazi ya polisi ya kwanza ni kumkamata mhalifu. Kumuua mhalifu au jambazi hutokea tu under very special circumstances. Huyu ilikuwa ni rahisi mno kumkamata hata kama alishaua watu kadhaa wakiwemo askari...!!

Sasa cheki hii. Kama huyu mtu ni gaidi au jambazi kweli na ana wenzake (back up) si hawa waliobaki na hawajulikani walipo wataendelea kuua watu na askari wengine tena...?
 
Nafikiri polisi hawa wako well trained kwenye mambo mengine kama kubambikia wapinzani vyesi na kuwatesa, kusomba kura za wizi au kuvuruga mikutano ya Chadema.

Hata intelijensia tu hawana kabisa, wanauaje mtu bila kufahamu ni nani na motive yake ilikuwa nini, labda hata alikuwa kichaa. Ndio shida ya kuwa na polisi waliopigwa tu msasa wa kisiasa ili kulinda maslahi ya chama fulani. Bure kabisa.
 
umeanza vizuri umekuja kuharibu tu hapo kwenye chadema
hivi ungelikuwa ni wewe unaona kabisa mtu anafyatua ana ua watu uanze kuchagua tena sehemu ya kumdhibiti kweli? you not serious
Hujui usemalo au ni mwenzako nini? Ameua halafu akamatwe na kupelekwa kula bure? Who told you kumbaff?
 
Polisi walipaswa kumtia nguvuni huyu mtu aliyekuwa na bunduki huko Kinondoni maeneo ya Selander. Lakini kwa kukosa weledi na kwa vile polisi Wana uoga uliokithiri wakamfyatulia risasi na kumuua.

Sasa watakosa taarifa muhimu kutoka kwa mhalifu huyu mfano:
  • Ni nani?
  • Katumwa na nani?
  • Yuko na akina nani (wako wangapi)?
  • Nini dhamira yao?
  • Nini chanzo cha wao kufanya hivi?

Kwa kumuua hawajatatua tatizo.

Polisi wetu Wana ujasiri wa kuwakamata CHADEMA tu.

Kanda maalumu ya polisi jijini Dar imeshindwa vipi kumkamata mtu huyu mmoja tu??
Ina semekana aliwapiga risasi askari wawili mwanzo kwa kutumia bastola na kuwa pokonya hizo silaha nzito.
Alikuwa akitembea njiani kwa mwendo wa pole huku akipiga risasi ovyo.
Baadae alijificha kwenye kibanda na alipotoka alikuwa na bunduki moja maana ya kwanza iliisha risasi.
Naile yapili ange piga tuu ovyo nayo ingeisha risasi na wengeweza ku mshika kirahisi.
Kungekuwa na sniper akampiga kwenye bega au miguuni bado wangeqweza kumshika.
Lakini inaonyesha polisi wetu walikuwa hawana shabaha na wawo walikuwa wakipiga ovyo. Maana risasi unazionz hazilengi.

Najamaa alipoanguka walizimimina kamawapo kwenye mazoezi.

Kafa na ushahidi umekufa.
Sasa serikasli tuepushe kuwapa p-olisi wadoria silaha nzito maana zipo exposed na mhalifu ni rahisi kuzipata.

Maelezo haya nimeyatoa baada kuangalia clips zilizoko mtandaoni.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Waswahili tunapewa picha na habari tunaitangaza sisi kama kweli vile
Kwa kutengeneza story hatujambo
Tumeambiwa tusubiri upelelezi ila tayari tunajua kila kitu na hata movie tunaweza kutengeneza ila baadae tukafanya editing kidogo
Upelelezi wa Moto pale msamvu mpaka leo kimya

Upelelezi wa Moto pale k'koo mpaka leo kimya

Upelelezi gani tunnaousubiri Zaid ya kutupotezea muda
 
Walikuwa wana-dramatize tu ili waonekane wanajua kitu halafu kqmera za tv ziwachukue. Hakuna kitu pale.

Polisi wetu ni wachovu


Yeyote aliye shusha ushuru wa simu janja kongole kwake. Zimesaidia ushirikishwaji wa taarifa za kichunguzi. Faida nyengine hii.
 
Inategemea na situation mkuu, that was the right choice ukiangalia alikua anashoot hovyo
Mimi ndiyo maana nasema Afrika inahitaji walimu asilia wa maswala ya uchunguzi hasa polisi.

Mimi kama mwalimu binafsi kwa tukio hili ningewafundisha kuharass adui ili atumie silaha zake ziishe pamoja na kutumia mbwa kukamata adui kama huyo au teaser gun then anakamtwa kilaini bila madhara makubwa labda wangekifa askari wawili na mbwa mmoja tu na adui akasalimika ili kutupa taarifa muhimu,bas!!
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Police wa kitz wadhulumaji sana
Huyo kijana hawezi kuwehuka ghafla
Ichunguzwe kuna nini maana jamaa wanasema ni mfanyabiashara wa madini
 
Achana na hizo stori za ufaransa... Tukio hilo la ufaransa lilikuwa na mazingira yake, tuzungumzie hili la leo!. Jamaa licha ya pistol aliyokuwa nayo bado alikuwa na SMG mbili, moja inaning'inia shingoni nyingine anaitumia kulenga kila anachokiona...
Hizo SMG mbili kazipoka kwa maaskari na hakuwa akizipiga ovyo. Alikuwa akivizia polisi tu tena alikuwa akitembea sehemu ya wazi (exposed) kabisa. Kapisahana njiani na wananchi kibao watembea kwa miguu na walio kwenye magari; hakuwafanya kitu.

Sawa, kazi ya askari ni ya hatari sana, lakini askari wenye mafunzo makini wangeweza kumtengua viungo fulani kwa risasi kiasi cha kumlegeza asiweze kufanya chochote na kumzoa kama bata hata angekuwa na silaha gani labda kama walifikiri anaweza kuwa na mabomu ya kutegeshwa (suicide explosives).

Tukubali askari wetu wako nyuma katika mambo haya. Wamezoea kuua tu kwa vile hatua ya mahakama haitiliwi maanani nchini na hivyo hawaoni sababu ya kusotea kazi hiyo. Mtuhumiwa awe hai au maiti husingiziwa chochote na shauri kufungwa kwa maelezo ya polisi pekee.

Hata tukio hili la leo lisingeshuhudiwa live na kurekodiwa na watu wengi, Polisi wangetupiga riwaya yenye kamba kibao kama walivyojaribu kufanya kwenye habari ya mwangosi kabla picha na ushuhuda wa walioona live kutolewa hapa JF.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Back
Top Bottom