Haya ni maoni yako ila tambua kuwa huyo jamaa alikuwa mobile siyo kuwa alikuwa kasimama tu. Ni lazima atakuwa na weledi mkubwa wa kutumia silaha hivyo lazima atakuwa na ana mafunzo kiasi ya kijeshi
 

Ulisha koswa koswa na AK 47 hata siku moja? Kama hujawahi, bora utulie, usiandike haya. Ww unaandika wakati akili yako ya kibinadamu. Ukiwa pale kwenye tukio na risasi zinakukosa kosa, haya wala huwezi fikiri, unakuwa mnyama.
 
Hata angekuwa kaweka silaha chini mimi binafsi nisingemwamini kabisa. Ningemchapa risasi kumwaahisha peponi. Akapokelewa na mabikra saba.
Kwa mauaji aliyofanya hakupaswa kuwa hai.
 
Kwa tukio la jana la Hamza kuua Police, ni dhahiri kuwa jeshi letu la polisi linawekeza zaidi kudhibiti wapinzani kuliko kudhibiti wahalifu.

Kwanza kabisa, ni bahati kubwa sana hamza hakuwa na nia ya kuua raia,angekuwa na nia hiyo angeua wengi sana ikizingatiwa kuwa kwa muda wote ule aliokaa pale na bunduki zile na hakuna police waliofika eneo husika angetaka kuua raia angekula vichwa vingi sana.

Pili,polisi hawakupaswa kumuua. Walipaswa kumdhibiti na kumkamata ili waweze kumhoji na kupata taarifa zaidi.

Jamaa hakuwa eneo la kificho, alikuwa eneo la wazi kabisaa, hivyo ilikuwa ni rahisi sana kwa 'sniper' kumpiga eneo la miguu kisa polisi wamdhibiti na wamkamate akiwa hai ili waweze kupata taarifa nyingi kutoka kwake.

Lakini, kitendo cha kumuua mtu ambaye kwanza yuko mwenyewe, pili eneo la wazi ni ishara kuwa polisi wetu hawana ujuzi wa hali ya juu ya kudhibiti wahalifu zaidi ya kuwaua.

Mwisho, natoa pole kwa familia zilizofia na wapendwa wao, Mungu awape moyo wa ustahimilifu katika kipindi hiki cha majonzi.

 
Kumuacha hai kungerahibu mengi sana ...na pengine mambo yangekuwa tofauti kabisa na kinachosemwa sasa...MAREHEMU HANA HAKI
 
Kwa tukio la jana la Hamza kuua Police, ni dhahiri kuwa jeshi letu la polisi linawekeza zaidi kudhibiti wapinzani kuliko kudhibiti wahalifu.

Kwanza kabisa, ni bahati kubwa sana hamza hakuwa na nia ya kuua raia, angekuwa na nia hiyo angeua wengi sana ikizingatiwa kuwa kwa muda wote ule aliokaa pale na bunduki zile na hakuna police waliofika eneo husika angetaka kuua raia angekula vichwa vingi sana.

Pili, polisi hawakupaswa kumuua. Walipaswa kumdhibiti na kumkamata ili waweze kumhoji na kupata taarifa zaidi.

Jamaa hakuwa eneo la kificho, alikuwa eneo la wazi kabisaa, hivyo ilikuwa ni rahisi sana kwa 'snaiper' kumpiga eneo la miguu kisa polisi wamdhibiti na wamkamate akiwa hai ili waweze kupata taarifa nyingi kutoka kwake.

Lakini, kitendo cha kumuua mtu ambaye kwanza yuko mwenyewe, pili eneo la wazi ni ishara kuwa polisi wetu hawana ujuzi wa hali ya juu ya kudhibiti wahalifu zaidi ya kuwaua.

Mwisho, Natoa pole kwa familia zilizofia na wapendwa wao, Mungu awape moyo wa ustahimilifu katika kipindi hiki cha majonzi.
View attachment 1909080View attachment 1909081View attachment 1909082View attachment 1909083
 
usijitoe ufahamu kwani hao askari hawajaenda shule ? wanajua kila mbinu za kushambulia na kuuwa pale ilikuwa sio kuuwa ni kuhakikisha anapatikana akiwa hai labda iwe haiwezekani kupatikana hivyo. je kwa mazingira yale kulikuwa hakuna uwezekano wa kumkamata mzima? kwani walikuwepo askari wangapi kwenye tukio ? na je maadui walikuwa wangapi? lkn adui alikuwa mmoja na ameweza kuuwa watu wa4 na baadae akawa anatamba njia yote tena kweupeeeeee bila miwani... askari walikuwa wanaweza kwa asilimia 1000 kumkamata bila kumuuwa.
WAMEPOTEZA USHAHIDI NA KESI ITABAKIA KUSUMBUA TU FAMILIA YA HUYO KIJANA MUUWAJI.
 
Alivyoishiwa risasi ndiyo wametoka ufichoni kuja kummalizia risasi, Polisi wetu na IGP Sirro hawana weledi, kama ameishiwa risasi na amenyanyua mikono juu wanampiga risasi ya nini? Wangemkamata wangepata taarifa zaidi kwanini kafanya vile na kama kuna wengine wapo nyuma yake. Utajua polisi wote walifeli form IV, hata ile akili ndogo hawana, wanachojua ni kupiga na kuua tu. Jamaa kawazidi ndiyo maana game ilikuwa 4 kwa moja, na pia 6 waliojeruhiwa. Sirro jiuzulu, jeshi la polisi lifumuliwe, halina weledi.
 
Tukio 1 tu limegeuza matukio mazuri maelfu na maelfu kuwa hakuna kitu na Askari kuonekana hawana maana.

Wapumzisheni Askari wetu jamani, siasa zenu za kipumbavu zisiwatoe hata ufahamu wa kuvukia barabara.
 
Matukio kama haya yanapotokea huwa ndio yanatuonyesha tuna vikosi gani, lakini ukiwakuta eti kwenye mazoezi ya UTAYARI, utasema hata kile kikosi hatari cha SWAT cha US, hakitufikii!!mikwala kibao!!kumbe ni ya kutisha waandamanaji tu!!!yule wala alikuwa hata sio wa kumuua, kutokana na eneo lilivyokuwa wazi vile, kuna silaha ambazo anapigwa anakuwa kama vile ame palalaizi , anakamatwa, sasa sijui kama hizo tunazo, sisi akili yote ni kwenye magari ya washawashana mabomu ya machozi tu!!
 
Nani alikuambia ukipigwa risasi miguuni hufi?
Ila pia anaweza asife,akishadhibitiwa anapatiwa matibabu sahihi na angeliwasaidia sana kupata taarifa muhimu na kuweka jinsi bora ya kukinga yasijirudie huko mbeleni.Hivyo ndivyo ilivyotakiwa kwenye like tukio.Walishafahamu anazo silaha za aina gani,walijiandaaje kumkabili bila kumuua?
 

tatizo jeshi la polisi limejaa viraza
 
Haya ni maoni yako ila tambua kuwa huyo jamaa alikuwa mobile siyo kuwa alikuwa kasimama tu. Ni lazima atakuwa na weledi mkubwa wa kutumia silaha hivyo lazima atakuwa na ana mafunzo kiasi ya kijeshi

Kikosi maalumu kwa ugaidi cha polisi kijumuishwe na askari wa wanyama pori wazoefu. Sababu wao wakati mengine hulazimika kudungua swala wakiwa speed aka mobile.
 
Kufa kwake inawezekana kabisa ni faida kubwa kwa wengine...marehemu always hana haki....
Kwa sasa kilichopo ni kusubiri kelele za mitandaoni zipoe na pengine inaweza kuundwa tume ya kiaina itakayokuja na mapendekezo kadha namna ya kuboresha utendaji wa jeshi letu!
 
TZ tuko wapumbavu wengi sana.

Askari wetu wale 14 waliofia vitani Sudan ktk kulinda amani walitukanwa mwanzo mwisho.

Polisi wa3 waliofia kwenye msafara wa viongozi kusini mwa TZ hivi karibuni waliogeshwa matusi mwanzo mwisho.

TRA wa5 waliofariki hivi karibuni halikadhalika walitukanwa kuwa ni waovu hata shetani anawaogopa.

TZ tupimwe akili maana siasa uchwara za mitandaoni zimetufanya tumekuwa wajinga hata hatuna mshikamano ktk mambo ya kitaifa.
 
Polisi wetu hawa inhiii!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…