Kwa tukio la jana la Hamza kuua Police, ni dhahiri kuwa jeshi letu la polisi linawekeza zaidi kudhibiti wapinzani kuliko kudhibiti wahalifu.
Kwanza kabisa, ni bahati kubwa sana hamza hakuwa na nia ya kuua raia,angekuwa na nia hiyo angeua wengi sana ikizingatiwa kuwa kwa muda wote ule aliokaa pale na bunduki zile na hakuna police waliofika eneo husika angetaka kuua raia angekula vichwa vingi sana.
Pili,polisi hawakupaswa kumuua. Walipaswa kumdhibiti na kumkamata ili waweze kumhoji na kupata taarifa zaidi.
Jamaa hakuwa eneo la kificho, alikuwa eneo la wazi kabisaa, hivyo ilikuwa ni rahisi sana kwa
'sniper' kumpiga eneo la miguu kisa polisi wamdhibiti na wamkamate akiwa hai ili waweze kupata taarifa nyingi kutoka kwake.
Lakini, kitendo cha kumuua mtu ambaye kwanza yuko mwenyewe, pili eneo la wazi ni ishara kuwa polisi wetu hawana ujuzi wa hali ya juu ya kudhibiti wahalifu zaidi ya kuwaua.
Mwisho, natoa pole kwa familia zilizofia na wapendwa wao, Mungu awape moyo wa ustahimilifu katika kipindi hiki cha majonzi.