Huyu mhalifu wa Selander alipaswa kukamatwa, siyo kuuawa
Nanukuu maelezo ya mmoja wa Mashuhuda:

"Akatoka Askari mmoja huku Benki wakaanza kupambana nae..wamepambana wamepambana na huyo Askari wa Benki wamepambana wamepambana, akishuti nae anapiga, akipiga nae anapiga. Yule Mbaba alipomaliza risasi zake, akakaa hivi akasimama, akapiga magoti akaongea kiislamu, akanyanyua mikono yake juu. Alivyonyanyua ile mikono juu yule Mkaka inabidi afanyaje, ampige. Alivyofikia ya hapa (anaonesha kwa ishara) moja sijui ilifikia kwa hapa (anaonesa kwa ishara) ndio akadondoka yule baba chali. Mguu mmoja akaukunja hivi, akadondoka chali Maaskari wengine ndio wakafika"

Kuna wakati nilikuja na uzi nikihoji Askari kupiga risasi zaidi ya 40 wakiikosa tageti na baadae Msemaji akaishia kuhusisha tukio na imani zisizo na maana.

Kikubwa hapa ni WELEDI. Sijui kwa hapa kwetu, ila huko kwa wengine huwa ni kwamba lengo kubwa ya Askari anapofika eneo la tukio ni kuisitisha/kuzuia hatari iliyopo na pindi tu hatari ikishakwisha Askari hana haja ya kuendelea kushambulia.

Na pia inasemekana 'alimiminiwa' risasi. Sidhani kama hapa kuna maelezo ya maana ya kuelezea sababu za msingi za kufanya hivi.

Kwa Wenzetu huko shambulio lolote la ziada baada ya kuimaliza hatari Muhusika anashtakiwa, awe ni raia aliyekuwa anajihami dhidi ya Jambazi, au Askari.

WELEDI, WELEDI.
 
Huwezi kunyanyua mkono juu una silaha mkono mwingine. Alikuwa anataka wafariki askari wengi zaidi?

Kama alitaka yaishe angeweka silaha chini na kunyanyua mikoni yote juu na kutoka eneo iliyopo silaha hata mita kadhaa ambazo kweli kila mtu angeona jamaa hana nia tena na mapambano.
 
Huwezi kunyanyua mkono juu una silaha mkono mwingine. Alikuwa anataka wauwe askari wengi zaidi.

Kama alitaka yaishe angeweka silaha chini na kunyanyua mikoni yote juu na kutoka eneo iliyopo silaha hata mita kadhaa ambazo kweli kila mtu angeona jamaa hana nia tena na mapambano.
Bado sioni room ya kufanya tofauti kwa Askari kwani sidhani kama hata huwa wanawajibishwa kwa kufanya ndivyo sivyo.

Lakini huwa kupiga risasi kunakuja baada ya wito wa kuamuamuru aweke silaha chini na kulala kifudifudi..je hayo yalifanyika?

Na vipi kuhusu kuendelea kumiminia risasi ili hali ameshatoka kwenye hatari? Mtu aliyelala chini mna muda wa kujiridhisha kama si hatari tena.

Refer tukio lililopita la Jambazi aliyetolewa Morogoro 'akaruka kwenye Gari' ....nadhani ni muendelezo tu wa Polisi kudhani wao wana mamlaka ya kufanya wanavyotaka.
 
Mtu ana silaha na anaua watu .Kwa nini mmuache ?By the way huwa hawasemi hawa wala kutoa ushirikiano kwa polisi. Wanakula yamini hawa magaidi. Bora wameliua tu.
Kama Mbowe - naye hajasema kitu ananyoosha vidole viwili tu
 
Yule alishaua askari kufa ilikuwa lazima ushahidi utapatikana kupitia simu na ndugu zake km na ndugu zake ni magaidi watangulizwe
Bado sio sababu.

Weledi wa Kipolisi unapaswa kuwa zaidi ya raia wa kawaida, ndio maana wanaandaliwa kufanya hizo kazi na hawabebwi tu na kupewa silaha.
 
Hapa unachofanya ni hadithi za kufikirika tu. Hapo ukute hata jirani akivamiwa na kundi la vibaka wenye masime huna weledi wa kunyanyua simu kwa mtetemo na woga.
 
Bado sioni room ya kufanya tofauti kwa Askari kwani sidhani kama hata huwa wanawajibishwa kwa kufanya ndivyo sivyo.

Lakini huwa kupiga risasi kunakuja baada ya wito wa kuamuamuru aweke silaha chini na kulala kifudifudi..je hayo yalifanyika?

Na vipi kuhusu kuendelea kumiminia risasi ili hali ameshatoka kwenye hatari? Mtu aliyelala chini mna muda wa kujiridhisha kama si hatari tena.

Refer tukio lililopita la Jambazi aliyetolewa Morogoro akaruka kwenye Gari .
Jamaa unataka kunitia HASIRA sasa.

Mtu kaua askari wawili na anapambana na wengine unataka apewe wito wa kuweka silaha chini au kulala kifudifudi?

Kama alitaka kujisalimisha angeweka silaha chini kusonga mbele akiwa kaweka mikono juu.

Serikali sisitizeni matumizi na kilimo cha mbogamboga wananchi wenu wanawehuka huku.
 
What do you mean wako wangapi? Have you sat and wonder [emoji189] to realize kwamba hili tukio linaonekana kwa kila namna kwamba ni self motivated na halina interest yeyote na chama cha siasa wala dini?
Hili tukio amelifanya yeye kwa maslahi yake, ndo maana baada ya kuona sasa hakuna kilichobaki kupambania akatoka nje. Alitaka kumalizika.
Alitoka nje baada ya kurushiwa gas..alizidiwa mule kwenye kile kibanda.
 
Hujui mbinu zinazotumiwa na magaidi wewe raia wakati wa mapambano..kaa kimya tu.
Hujui mbinu zinazotumiwa na magaidi wewe raia wakati wa mapambano..kaa kimya tu.
Ndio majibu yenu Wananchi hayo.

Eneo la wazi lile bado kulikuwa na nafasi ya kutumia welediwa Kipolisi zaidi ya kuuwa tu.

Kumbuka walishafanikiwa kuisimamisha hatari iliyokuwepo....Mtu ukishamuamrisha akalala chini na kuweka mikono sehemu unayoiona unashindwa nini kumdhibiti kama wewe ni Askari?.
 
Huwezi kunyanyua mkono juu una silaha mkono mwingine. Alikuwa anataka wauwe askari wengi zaidi.

Kama alitaka yaishe angeweka silaha chini na kunyanyua mikoni yote juu na kutoka eneo iliyopo silaha hata mita kadhaa ambazo kweli kila mtu angeona jamaa hana nia tena na mapambano.
Na sijui kwanini aliuwa askari wachache kiasi kile.
 
Hata vitani ukimpiga risasi adui akiwa ame sarenda ni uhalifu wa kivita, utashtakiwa.

Ukiendelea kumpiga risasi adui aliyekufa tayari, ni uhalifu wa kivita pia.

Jana polisi walikua na nafasi ya kumkamata akiwa hai, lakini naona walikwenda kwa lengo kuua tu.
Kabisa Mkuu...sasa nashangaa Watu wanaunga mkono madhaifu ya Jeshi la Polisi.

Ndio maana Raia tunaonewa sana maana hata Polisi wanaamini tupo Wajinga wengi.
 
Point. Au hata angepigwa za miguu tu. Na aliyemuua ametumia risasi kama 5-8 hivi kupatia shabaha! Wakati jamaa mwenyewe alikuwa amesimama kama mti tu.
Kuna haja ya jeshi letu kuunda kikosi cha marksman Mahiri na kuwamotisha!
 
Ndio majibu yenu Wananchi hayo.

Eneo la wazi lile bado kulikuwa na nafasi ya kutumia welediwa Kipolisi zaidi ya kuuwa tu.

Kumbuka walishafanikiwa kuisimamisha hatari iliyokuwepo....Mtu ukishamuamrisha akalala chini na kuweka mikono sehemu unayoiona unashindwa nini kumdhibiti kama wewe ni Askari?.
Nina mashaka na uwezo wako wa uelewa.

Uwanja wa vita kama ule jamaa anakuja na kushoot askari anapora bunduki anaanza kupiga kelele anadeal na askari ulitaka askari amkaribie na kumwambia "Hamza weka silaha chini bby wangu Hamza kibonge"

Ile ilikuwa vita ya niue au nikuue basi na polisi walichofanya si kosa. Unamtetea kuwa alinyosha mikono juu kivipi wakati ametoka kwenye kibanda na silaha yake.

Ulitaka polisi wamkimbilie amwage bongo zao utangaziwe polisi 24 wamefariki ufurahi?
 
Nanukuu maelezo ya mmoja wa Mashuhuda "......akatoka Askari mmoja huku Benki wakaanza kupambana nae..wamepambana wamepambana na huyo Askari wa Benki wamepambana wamepambana..akishuti nae anapiga..akipiga nae anapiga..yule Mbaba alipomaliza risasi zake..akakaa hivi..akasimama..akapiga magoti..akaongea kiislamu..akanyanyua mikono yake juu..alivyonyanyua ile mikono juu..yule Mkaka inabidi afanyaje..ampige..alivyofikia ya hapa (anaonesha kwa ishara)..moja sijui ilifikia kwa hapa(anaonesa kwa ishara)..ndio akadondoka yule baba chali..mguu mmoja akaukunja hivi..akadondoka chali Maaskari wengine ndio wakafika"

Kuna wakati nilikuja na uzi nikihoji Askari kupiga risasi zaidi ya 40 wakiikosa tageti na baadae Msemaji akaishia kuhusisha tukio na imani zisizo na maana.

Kikubwa hapa ni WELEDI...Sijui kwa hapa kwetu, ila huko kwa wengine huwa ni kwamba lengo kubwa ya Askari anapofika eneo la tukio ni kuisitisha/kuzuia hatari iliyopo...na pindi tu hatari ikishakwisha Askari hana haja ya kuendelea kushambulia.

Na pia inasemekana 'alimiminiwa' risasi.....sidhani kama hapa kuna maelezo ya maana ya kuelezea sababu za msingi za kufanya hivi.

Kwa Wenzetu huko shambulio lolote la ziada baada ya kuimaliza hatari Muhusika anashtakiwa, awe ni raia aliyekuwa anajihami dhidi ya Jambazi, au Askari.

WELEDI...WELEDI.
Haya mambo mnayasema kwa sababu hamuijui Bunduki. Haiwezekani na haitatokea mtu kujua kwamba anaepambana nae ameishiwa Risasi. Lakini pia kumbuka asui yule alikuwa akiua askari haiwezeka umuamini kuwa ameishiwa risasi na amesalenda
 
Back
Top Bottom