Huyu mjamzito amenyanyaswa na wahudumu wa mwendokasi hapa Mbezi Mwisho mpaka akazimia

Huyu mjamzito amenyanyaswa na wahudumu wa mwendokasi hapa Mbezi Mwisho mpaka akazimia

Ishu sio kukaa kwenye siti, ishu ni dogo ataongeza uzito wa mzigo.

Siungi mkono huyo mama kufanyiwa hivyo.

Upande mwingine hii inaonyesha jinsi gani bongo life ni gumu. Huyo mama alikosa 200 ya kumlipia dogo nauli.
Ni sawa anaweza kukosa, je hao mapunguani walosimama wakimuangalia na huyu alowahi kupiga picha ili alete umbea humu alishindwa kumsaidia huyo mama?
 
Nilitamani kusikia kuwa, kuna mwanamme mmoja aliguswa hapo akamlipia hiyo sijui shs 700
badala ya kusubiria hadi kelele ziwe nyingi kiasi hicho na kuweza kusababisha madhara kwa mama kijacho
 
Nilitamani kusikia kuwa, kuna mwanamme mmoja aliguswa hapo akamlipa hiyo sijui shs 700
badala ya kusubiria hadi kelele ziwe nyingi kiasi hicho na kuweza kusababisha madhara kwa mama kijacho
Kabisa
 
Kuna Uzi humu unasomeka,"Usimuonee huruma kabisa mwanamke".

Labda bus lile lilikuwa limejaa wadau wa mada ile,ila wangemsaidia huyo mtoto kwa kumlipia nauli.
 
Wote mnaotukana na kulaumu hajasaidiwa nanyi ni wapumbavu tu maana hamjui stori ya upande wa 2.

Sijaja hapa kubrag tumemsaidia 1,2,3.... Tunajaribu kuonesha huduma mbovu zinazotolewa na DART.

Kwa hiyo msidhani watu walikaa tu bila kufanya lolote, mpaka mwendokasi haijaondoka hapo sio bure tu.

Pumbav waheed😡
 
Ila ukweli huyo analipa mama alipaswa Kutumia busara au kauli nzuri ili apate msaada kama hakuwa na nauli Kutumia ujauzito wake na hali yake ya ugonjwa kupata free pass ya mtoto haikuwa sawa
Kuna siku nimefanya kosa linalohitaji fine kwa hao mwendo Kasi nilifanya pasi na kujua maana ndio kwa mara ya kwanza nilikuwa napanda
Abiria na wale jamaa waliwaka hatari binafsi nilikaa kimya safari ikaendelea katikati ya safari mmoja wao akaamua kunisemesha imekuwaje nikamsimulia mazingira yote yalivyo tena kwa utulivu kufika mwisho wa kituo jamaa wakashauriana wakasema unaweza kwenda bro baadhi ya abiria wakashangaa
 
Miaka mitano unalipia nauri.
Hicho ndo kikubwa
Nauli anaanza lipia mtoto wa la kwanza.

Miaka 7 mtu hutakiwa kuanza la kwanza.

Miaka 5 au 6 kuanza la kwanza hii ni trend imevamiwa na wamama wa siku hizi.
 
Hapa conclusion ni kwamba...

UMASIKINI ni fedheha na kitu kibaya sana...
 
Mleta mada Hongera sana kwa kuonesha mambo yalivyo.
Kwa navyojua siku hizi watu wana kitu inaitwa Sheria Mkononi na najua ilitumika kwa asilimia flani hapo.

Kitu kibaya zaidi ni picha aliyojengewa huyo Mtoto wa Miaka mitano inatia huruma sana.

Wanaume tutafute hela Mama Vijacho wasiteseke.

Huu usafiri ukitaka kujua ni wa hatari.Angalia Mwendokasi ya Mbezi jinsi watu wanavyoshonana na mabasi yapo mengi tu yamepaki.
 
Nianze na Swali: Watoto wa kuanzia miaka mingapi wanapaswa kulipa nauli za mwendokasi?

Mida ya hii jioni huyu dada mjamzito alikuwa na mwanaye wakiwa wanasubiri mwendokasi za Kivukoni. Mtoto alikuwa na miaka kama mitano hivi.

Alipoingia kwenye gari cha ajabu mhudumu anayescan ticket akawa analazimisha yule dada amlipie na huyo mtoto nauli, ilhali ni mtoto mdogo anayeweza kupakatwa.

Pamoja na dada kuwaambia atampakata lakini walimgomea, ndipo ikatokea kukusukumana hapa na pale mpaka ikabidi watu wote watoke kwenye mwendokasi.

Haijalishi ni nani alikuwa na kosa hapa, lakini sijapenda namna huyu dada mjamzito alivyokuwa treated, maana wamemuharrass sana mpaka dada wa watu akazimia, huku mwanaye akilia kwa uchungu.

Hili shirika japo ni la umma, lakini staffs wake wana zero customer care, hawana utu na hawajali wateja hata kama ana hali inayohitaji kusaidiwa.

Mtoto waliyekuwa wanafosi alipie👇
View attachment 2960024

Mama mjamzito akiwa ameanguka chini👇
View attachment 2960027

View attachment 2960028

Mwendokasi iliyokuwa inaenda Kivukoni👇

View attachment 2960033

WEWE MPUMBAVU SANA. UNAKIMBILIA HUKU KULETA MASIKITIKO HUYO DADA ANANYANYASWA WEWE UNAFANYA NINI? NYIE MNA AKILI KWELI? WOTE NYIE MMEHUSIKA KUMNYANYASA HUYO DADA NA HUONI AIBU KUJA KUANZISHA UZI.

MITANZANIA NI MINAFIKI NA MIPUUZI SANA. SI WANAWAKE SI WANAUME. MJAMZITO ANANYANYASWA UNAISHIA KUPIGA PICHA NA KULETA MALALAMIKO? WEWE UNA AKILI KWELI? JINSIA GANI?

1. ULISHINDWA MLIPIA NAULI HUYO MTOTO?
2. MLISHINDWA KUMJIA JUU HUYO MHUDUMU?
3. MLISHINDWA MGOMEA ?
 
Nilitamani kusikia kuwa, kuna mwanamme mmoja aliguswa hapo akamlipia hiyo sijui shs 700
badala ya kusubiria hadi kelele ziwe nyingi kiasi hicho na kuweza kusababisha madhara kwa mama kijacho
Kwa hiyo kuwa mwansume ndio kutoatoa pesa hovyo sio?
 
Back
Top Bottom