Nimeangalia kipindi cha Ujenzi EATV nikamuona dada mdogo kiumri akiwa tayari kashajenga nyumba tatu Kubwa jijini Dar.
Anadai yeye huwa hapendi sana starehe ila starehe yake ni kujenga nyumba nzurinzuri. Kisa cha kuja hapa ni umri wake na vitu anavyomiliki.
Bahati mbaya Mtangazaji wa kipindi hicho cha ujenzi Basilisa John hakumuuliza siri ya mafanikio yake ili wanawake wengine wajitume pia. Hakuulizwa jina pia, zaidi ni kuonesha tu mijengo yake.
Japo Sina uhakika, Anaonekana hajaolewa. Aaaaaaaaaahhhhhhh
Kwa maisha yetu ya kibongo,kuweza kumiriki nyumba tatu za thamani ya 60+Milioni,tena ukiwa at 35+,ni wachache sana,umalize shule update ajira yq kukulipa 2.5M+,hizo ajira ni chache sana,
Kwa uzoefu wangu,kwenye industry Moja maarufu,salary zilikua ndogo sana miaka hiyo ya 2000,ila wizi kwenye industry ulikuwa mkubwa sana,vijana walitqjirika sio kwa salary au mikopo Bali wizi!
Magsri,majumba,walijenga wengine waliamua kuwa na totoz TU,mpaka sie tunaingia 2006+,watu walikuwa wameishatsjirika,industry ikawa ngumu 2010+,hapo aliyekuwa hajajenga ndio imetoka hiyo,ikirudi pancha!!wazee wangu wengine ndio ikawa chaliiii kabisa,wamekuwa mafukara,waliosoma alama za nyakati Sasa hv ni madingi 56+,wanamiriki makampuni na wametoa ajira kwa machalii kibao,ila wizi ndio hakuna tena,ni kuishi kwa salary TU,
Mzungu mchawi