Huyu mwanamke ana sonona. Msaada wakuu

Huyu mwanamke ana sonona. Msaada wakuu

Eeeeeeh jibu analo yeye
Anawatoto watano sasa. Mume wake aliondoka miaka 5 iliyopita, akaacha watoto watano: wamwisho (miezi 9), wakati huo mtoto wa pili (3) kutoka mwisho anaumwa (Athma).

Mwanaume akaondoka kachukua mke wa watu kijiji jirani wakaenda Katavi. Hakuwasiliana na familia yake muda wote akiwa Katavi.

Mwanamke aliishi kwa Vibarua vya Shambani na wanae... akajikaza akalima akapata, akaendelea kusomesha wanaye.

Baada ya miaka 5 mume amerudi anaomba asamehewe waendelee na maisha!

Wakuu nini cha kufanya kwa huyu mwanamke?
 
wamwisho (miezi 9), wakati huo mtoto wa pili (3)

Mume wake aliondoka miaka 5 iliyopita,
Elewa mtoto wa mwisho yaani wa 5. Alikuwa na umri wa miez 9.
Wa pili kutoka mwisho: maanisha wa 4 alikuwa na miaka 3.
 
Inategemea hilo kosa la abandon amelifanya mara ngapi, kama ni mara ya kwanza amsamehe, ampe chance ya wao kulea watoto pamoja.

Lakini asiache kupambana na kazi zake kulea watoto wake sababu once mtu akikuabandon pengine akafanya hivyo tena.

Kuna watu wana spirit ya mahangaiko na mizururo. Na anaweza kumsamehe huyo baba akabadilika wakalea watoto wao hadi mwisho wa maisha yao, its a game of chance and uncertainties.
 
Mwambie aachane nae tu

Kama aliweza kulea watoto wake kwa miaka 5, na hawakupungukiwa kitu.. hakuna kitakachomshinda.

Akaze aachane na huyo fala
 
Yeye mwanamke ndio mwamuzi wa mwisho huwez jua alikuwa anakunwaje au ulijimilikisha Jimbo baada ya jamaa kuondoka?
Inaonekana hapa msemaji wa familia,anaona asilimia zake anaenda kurudishiwa.
Mtoto wa mwisho, miezi 9. Anaefuatwa na wa mwisho, miaka 3. Na mme aliondoka miaka 5.
Si kweli huyu mama si mkulima,lakini aliyevamia inaonekana ana vita,sasa kumpisha mwenye mali hataki.
 
Ni mme wake au hawara? Waswahili wengi huwa wanapenda kusema mume, hata kama alimchukua bila kuowana kisha wakazaa lakini bado ataitwa mume. Aleyommba gekke huyo ni mume wake??
 
Kiswahili naona ni kigumu, someni kwa utulivu.

Hapo ndo nyumbani kwao sasa huyo mama atafanya nini,

Sema tu maradhi ndo cha kuofiya.
 
Tunaweza toa maoni tukabinuka hadi kupiga misamba ila maamuzi yapo kwenye moyo wa huyo mama.Kuna Ile kauli"mama nanii tushakuwa sasa tutulie tulee watoto wetu" Hii kauli kina mama wengi huwa hawachomoi.
 
wamwisho (miezi 9),
Watu wote wapo kwenye mfungo, hawataki chaii.

giphy (1).gif

PambanaZaidi/CottonandMore
 
Alikuwa au ana miezi?
rejea para ya 1

Inategemea hilo kosa la abandon amelifanya mara ngapi, kama ni mara ya kwanza amsamehe, ampe chance ya wao kulea watoto pamoja.

Lakini asiache kupambana na kazi zake kulea watoto wake sababu once mtu akikuabandon pengine akafanya hivyo tena.

Kuna watu wana spirit ya mahangaiko na mizururo. Na anaweza kumsamehe huyo baba akabadilika wakalea watoto wao hadi mwisho wa maisha yao, its a game of chance and uncertainties.
Asante
 
Mkiambiwa muache kula sana vyakula vya wanga mnaona mnaonewa, sasa kitu kipo wazi kabisa huyo fedhuli aliondoka miaka mitano iliyopita akaacha watoto watano, wa mwisho akiwa ana miezi 9, wa pili kutoka mwisho alikua ana miaka mitatu na mwenye asthma(pumu) ugumu uko wapi hapo wa kuelewa,

Kurudi kwenye mada, huyo mama kama amekutuma umuombee ushauri basi bado anamtaka mumewe, kwa aliyofanyiwa wala hakua na sababu ya kuomba ushauri.
 
🤝🤝
 
Back
Top Bottom