Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,916
- 43,505
Akimsamehe halafu wakarudiana tena atakuwa hana tofauti na wale wehu….Anawatoto watano sasa. Mume wake aliondoka miaka 5 iliyopita, akaacha watoto watano: wamwisho (miezi 9), wakati huo mtoto wa pili (3) kutoka mwisho anaumwa (Athma).
Mwanaume akaondoka kachukua mke wa watu kijiji jirani wakaenda Katavi. Hakuwasiliana na familia yake muda wote akiwa Katavi.
Mwanamke aliishi kwa Vibarua vya Shambani na wanae... akajikaza akalima akapata, akaendelea kusomesha wanaye.
Baada ya miaka 5 mume amerudi anaomba asamehewe waendelee na maisha!
Wakuu nini cha kufanya kwa huyu mwanamke?
Lakini atakuwa hana tofauti na magaidi ya kule Hamas maana ndio yana roho ngumu!
Mwambie amsamehe lakini wasirudiane tena na wakae mbali kabisa abaki kuwa baba tuu!