Huyu raia Godwin Gondwe amepata wapi ujasiri wa kuvaa sare za JWTZ?

asante kwa kufichua siri
 
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya.
Na salute anapigiwa.
Alihitimu jkt . NI jeshi la akiba. Anaruhusiwa kuvaa combat kwenye shughuli maalum.
Alipass out. Alipiga gwsride. Alikula kiapo kwa Nchi na kwa amiri jeshi.
Anayo force number.
Hata Halima mdee, zitto kabwe wanaruhusiwa kwani walihitimu mafunzo ya jkt program maalum.
Kumbuka wakati wa Vita ya kagera ,baadhi ya jkt kuruta walienda front.
 
Hii nchi ndani ya utawala huu wa awamu ya tano, kila aliye katika madaraka, hata yawe madogo kama vile Katibu Kata, anajiona yupo juu ya sheria!

Na anajiona ni "untouchable" ambaye hawezi kuguswa na Jeshi la Polisi nchini
 
1:Naongea na civilian.
2: Jkt inasimamiwa na jw. Force number Ni number anayotumia Askari kujitambulusha Kama raia kuwa na Personal file number.
Kombat Ni vazi la kijeshi linalovaliwa wakati wa operation( police wanazo magereza wanazo fire wanazo wanyama pori wanazo.) Jw wanazo na jkt wanazo.
Kwa taarifa yako, Mkuu wa wilaya anaweza kukagua gwaride na akawapa Askari vyeo kwa niaba ya Amiri Jeshi Mkuu.( Rais)
 
Kwa taarifa yako Mgambo wanaitwa Jeshi la Akiba.na Ndio maana linasimamiwa na JWTZ. Mshauri wa Mgambo wa mkoa au wilaya Ni wanajeshi wa jw. Mkuu wa Jeshi la akiba kwa Sasa Ni Maj Gen( aliyekuwa anaongoza Jkt kabla my rais hajamteua Afande Charles mbughe)
 
DC ni kamishna (ambae ni mtumishi wa umma) sasa utumishi wa umma na kuvaa mavazi ya vyombo vya ulinzi na usalama wapi na wapi?
Ni tanzania pekee, huwezi kukuta kokote duniani mtumishi wa umma kama huyo.
Ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa wilaya .
 
DC ni kamishna (ambae ni mtumishi wa umma) sasa utumishi wa umma na kuvaa mavazi ya vyombo vya ulinzi na usalama wapi na wapi?
Ni tanzania pekee, huwezi kukuta kokote duniani mtumishi wa umma kama huyo.
Mkuu wa takukuru wa Sasa Ni mjeshi. Na Ni mtumishi wa umma.
RC wa kagera Kaguti Ni mjeshi. Nauliza: rc mtumishi wa umma kupiga combat ofcn Ni kosa?
Usichanganye madesa beberu. Mfumo wa utawala tz upo sawa kwa mahitaji ya Watz. Haikuanza Leo. George mkuchika waziri ( mb) ,Rtd Lt yusuph makamba, Maj Anatory Tarimo, nknk walikuwa civil servants na wajeda pia.
Kuruta( recruits) akisha pass out Ni sehemu ya jeshi. Pakitokea OP na akahusishwa kwenye hiyo OP hazuiwi kuvaa combat Wala kupewa bunduki.
Alifundishwa kupiga salute na kofia, pasipo kofia na akiwa na bunduki.
Huyo Ni sehemu ya jeshi.
Sare wasizoruhusiwa kuvaa Ni dress number one. Lakini combat anavaa( haina crown)
 
Jibu hili hapa limemaliza utata, hakuna cha nini wal nini, mengi yamenenwa ila hili limemaliza. Kuna mwenye swali??

ᴮʸ cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᵈ
 
Tofautisha vyeo vya kisiasa na vyeo rasmi, maana kuna watu umewataja hapo wenye vyeo vya kisiasa kitu ambacho kwasasa hakipo, pia kuna wale majenerali; kikawaida kuna ngazi ya ukifikia utastaafu kuweko kwenye muundo wa utawala wa chombo husika lakini hustaafu kazi kwa maana cheo chako utatambulika nacho hadi kufa kwako na ndio maana simshangai Gaguti wala Kijuu, kwa maana wale ni majenerali.

ᴮʸ cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᵈ
 
Kama unayaelewa usingehoji Dc gondwe kuvaa nguo zenye mabaka sawa na sare za jwtz.
Soma hapo, kila kitu kina muundo wake

ᴮʸ cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᵈ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…