Ifikie hatua tuachiane nafasi

Ifikie hatua tuachiane nafasi

Hivi unajua ukiwa busy kutafuta wa kuishi nae utaangukia pua maana chaguzi zinakua na criteria na kwa kuwa wanadamu hatujakamilika sio rahisi sana kumpata mwenye vigezo vyote,cha kufanya ishi kama hutafuti ila usiache kuanzisha mahusiano,hakika miongoni mwa hayo mahusiano utapata mtu utainjoi nae sana mtu mtakaelewana nae vizuri.
 
Kwa mtazamo wangu, watu wanaopenda kuwafatilia wenzao Kwa kila kitu na kila muda awe mwanamke au mwanaume ni watu ambao naona Kama Wana matatizo ya akili.

Kiufupi sio watu wazuri wa kuwa nao kwenye mahusiano, haya matukio ya kuchinjana na kuuwana Kwa wapenzi ni moja ya matokeo ya kutopeana nafasi.

Mtu unafatiliwa asubuh unapotoka kulala Hadi usiku unapoingia kulala Aisee!

Ninachojua Kama binadamu Kuna wakati utahitaji uwe peke yako, ufanye Mambo yako vizuri na uyatafakari Kwa kina. Na Wala hakuna ulalazima wa hayo Mambo yako umwambie mkeo au mumeo.

Kupeana nafasi kunaboresha mahusiano Kwa watu wanaojitambua kinyume na Hapo ni majanga.
 
Back
Top Bottom