Ignore list on JamiiForums: Maboresho ya mwaka 2020

Ignore list on JamiiForums: Maboresho ya mwaka 2020

Melo to me this is not crucial

Kila mara humu tunalalamika viongozi wetu katika mambo mbalimbali na hata kudai watusikilize na wasipotusikiliza tunandelea kulalama je kumbe wanavyotuignore ni sawa? Pía wakiignore maendeleo kwa umma ni sawa kwani nasi kama binadamu tunapenda kusikia na kuona yanayotupendeza! Basi tusiwakwaze na viongozi wetu ili wasituignore bali watupende kwa kusifia
Binadamu si option kupatwa, kusikia au kuona mabaya au mazuri tu kwani sarafu ya maisha ni pande mbili( uzuri/ubaya)

Kuna watu wanaweza kutumia fursa hii kuniignore pale juu, ni sawa kwa kuwa majumbani mwao watakutana na haya wanayoyakimbia, huwezi kuwa bora bila kupingwa hadharani na sirini( tuko na vivuli lkn bado tunaignore vipi tungekuwa og)

Utakua bia yetu wewe, pole kwa kufungiwa vioo 😂🤣🤣☺️☺️☺️☺️
 
Mkuu Maxence Melo , this improvement is good. Lakini pia hii yaweza kupunguza chachu ya mijadala humu jf.

Mfano jukwaa la Siasa ndiyo jukwaa ambalo nadhani linaongoza kuwa viewed na mijadala mingi. Kupamba moto kwa jukwaa hili ni kutokana na migongano ya hoja za wachangiaji. Migongano ya hoja ni based on political affiliation/belief ya mtu husika.

Na nionavyo mimi binafsi, members wanaonekana 'kuchukiwa' humu ni wale wanaotoa maoni yao kusupport or kufavor utawala huu wa awamu ya tano wa ccm, mfano members kama Bia yetu , USSR , Magonjwa Mtambuka , jingalao , n.k

Hao ni baadhi ya members ambao wao wameamua kuweka wazi political affiliations zao na wanaandika mawazo yao kwa mlengo huo.

Nikiangalia trend kufuatia maboresho haya ya 'ignore' button, member BIA YETU ndiye ataongoza kuwa ignored sana humu jf, sio kwa sababu anatukana sana watu, bali ni kwa sababu tu maoni yake ya kisiasa hayapendwi na mtu wa upande mwingine kisiasa!

Tukianza kutandikana 'ignore' button kwa sababu ya political affiliations/oppion, then tunaelekea pia kutandikana 'ignore' button kwa sababu ya religious affiliations/opinion zetu.

Jf portrays itself as the place "Where We Dare To Talk Openly". Kwa kuzingatia na kuitekeleza kauli mbiu hii, jf is adhering to one of the principles of natural justice ambayo ni Haki ya Kusikilizwa. Yes, mtu unapompa platform ya yeye azungumze openly, impliedly unakuwa umempatia haki ya kusikilizwa (right to be heard).

'Ignore' button ni systematic switch ya kuziba masikio. Right to be heard is meaningless endapo wasikilizaji/wasomaji wameziba masikio na kuvaa miwani ya mbao (ignore button)!

Mtu akiwa ignored sana, itaathiri contribution flow yake ya threads or posts. Ikifanyika kwa yule na yule na yule, in the long run itaathiri chachu ya mijadala hapa Jf. Jukwaa litakosa hoja ama mawazo kinzani, eventually jf will be full of threads za maoni ya mlengo mmoja.

Uwepo wa migongano ya hoja na mijadala kinzani, ni chachu kubwa na pia inaisaidia sana jf kutoonekana ni politically based upande mmoja.

Mimi nashauri 'Ignore Button' iwekwe kwenye Threads tu, not at individual level.

Mfano tu: mkuu Mshana Jr naweza bonyeza Ignore Button kwenye thread yake ya kisiasa, ila nikafaidika maarifa kwenye thread yake nyingine ya mambo ya ulozi.

Au naweza block/ignore Thread ya kisiasa ya mkuu Hornet , ila Thread yake nyingine ya mambo ya biashara ikanipa maarifa.

-Kaveli-
Yote hii imekuja baada ya watu kama kina Mmawia kuzidiwa na hoja za nguvu na zenye ushahidi kutoka kwa baadhi ya rare creatures in JF.
 
Huu ni udikteta!
Ukiona mtu unahangaika eti usiwe unaona maoni ya mtu flani kisa hayuko upnde wako, jua una tatizo la kisaikolojia au una stress.

Binfsi siwezi kujihangaisha na mtu tunaekutana tu mtandaoni.
 
Kubofya ignore list dhidi ya jingalao ni ishara ya kuniogopa na kunikimbia ulingoni.

Kuna wafuasi wa CCM kibao humu mbona mmetajwa nyie wanne sana, mjirekebishe lugha za kuprovoke reactions au lugha mbovu achaneni nazo, or else mtajikuta nyie wanne peke yenu mkijijibu wenyewe hahahaaaa 😂😂😂🤣🤣🤣☺️☺️☺️☺️☺️🙈
 
'Unadhani'... at least you sound fair in your writing.

Well, yawezekana nikawa nimeitafsiri tofauti (not 'vibaya').

Kuna haki na wajibu. Mtu ana haki ya kusikilizwa maoni au mawazo yake, lakini naye ana wajibu wa kutokuvunja Sheria ama kumkwaza mwingine katika utoaji wa mawazo yake. So Mimi huwa nafikiri kwamba mtu aseme au aandike mawazo yake (bila kukwaza mwingine), then ni juu ya msikilizaji/msomaji ku-react anavyoona inafaa.

Mimi binafsi ninachokiona hapa ni kwamba hii 'Ignore Button' itakuwa 'politically driven' zaidi kwasababu tu kuna watu wa kundi moja hawapendi maoni ya upande mwingine.

JF ni majukwaa huru, that means kila member anaandika maoni au mawazo yake kwa mlengo anaouamini yeye.

Ukiwa humu tarajia kupata mawazo ama hoja kinzani.

Humu jf mtu anaweza leo akatoa maoni usiyoyapenda ama usiyokubaliana nayo, lakini kesho mtu huyo huyo akatoa maoni unayokubaliana nayo.

Lakini pia, mtu X anaweza toa maoni usiyounga mkono kwenye mada ya kisiasa, mtu X huyo huyo ukamuunga mkono na kupata maarifa kwenye mchango wake mwingine let say kwenye Jukwaa la Technology.

Kwenye ulimwengu unaofuata rule of law and justice, Haki ya Kusikilizwa hainaga exemption.

Kwenye uwanja wa mijadala huru hauwezi kutaka usome/uone/usikie kile kinachokupendeza tu!

-Kaveli-
Mimi sipendi ku block mtu Mara nyingi hu ignore maana kila mtu anapaswa kusikilizwa Ila mfano jukwaa la siasa Kuna watu wanaharibu makusudi nyuzi badala ya ku discuss wao huanza kuharibu nyuzi yoyote Tena kwa matusi, Sasa wanaotaka kuwa ignore ni Bora uwa ignore tu, Tena ingetakiwa sio ku ignore tu mtu anayetoka nje ya mada pia ku mpa ban ya mda ili kulinda hadhi ya JF before I joined JF nilikuwa napenda kusoma jukwaa la siasa watu wali discuss mada bila ushabiki na walikuwa wanatoa hoja bila matusi hata Yale maoni yaliwasaidia watalawa, Ila nowdays jukwaa limekuwa matahira sehemu ya matusi na ukiendelea kusoma huo upuuzi jukwaa zima linaonakana hamnazo haiwezekani JF idhidiwe na watu wa FB, au Ig kwenye maslay quenn kwenye hoja nzuri.
 
Mmefikia wapi kuweka jukwaa la TANZIA?

Au hamjui kuwa ni heshima kwa jamii kwa JF kuwa na jukwa hili?
Mnakwama wapi?

Hatutaweza kuanzisha jukwaa la misiba kwa sasa. Kumradhi
 
Nyie waoga sana nyie, hii sio sawa, mnapenda kumsikiliza mnachokipenda tu kama wale watu wenu wa tweeter ukiwapinga tu wanakublock, hiyo sio sawa na hata hili hapa linakandamiza freedom of speech and expression, kwa nini haya maboresho yawe katika kipindi hiki Maxence Melo? kuna nini nyuma ya pazia? tujifunze kuvumiliana wapendwa.
Siwezi kuvumilia upumbavu wa uvccm na buku 7 fc
 
Kuna wafuasi wa CCM kibao humu mbona mmetajwa nyie wanne sana, mjirekebishe lugha za kuprovoke reactions au lugha mbovu achaneni nazo, or else mtajikuta nyie wanne peke yenu mkijijibu wenyewe hahahaaaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji3526][emoji3526][emoji3526][emoji3526][emoji3526][emoji85]
Kila mtu ana Uhuru wake Ila jingalao and co company wao ni kuharibu mada na matusi mwanzo mwisho, Sasa wabaki wasome wenyewe huo utopolo wao. Mbona Kuna watu wanazi wa CCM wako critical tu na kikawaida.
 
Naam kiongozi. Naomba usiniweke mimi maana haitafanya kazi [emoji1787]
Melo bhana! Mbona umeharibu sana? Mtu kama anakukera si unajitoa jf?

Yani jf itakuwa ina makundi kama magroup ya whatsap ya vyama vya siasa sasa.
 
Back
Top Bottom