IGP Simon Sirro afanya mabadiliko madogo kwa Makamanda wa Polisi

Rushwa 30M kwa wik ?? Duh kweli noma
 
Sasa mkuu si Kuna vyeo na utawala huyo OCD na RCO wakiwa cheo kimoja si bado bado RCO anakua juu ya OCD kutokana na nguvu ya utawala aliopewa na anaweza kutoa amri ambayo OCD akaitekeleza au wakiwa cheo kimoja huko polis hakuna kuheshimiana hta kma mmoja ndo mtawala? Nisaidie hapo maana bado natoka kapa sijaelewa
 
Kwa jeshini sababu kila kitu ni amri, Cheo Cha kiutawala kinapaswa kuendana na rank ya juu pia.

Ni sawa ujiite baba lakini mkeo ndio anakulisha sijui utampa amri gani, I hope umenielewa.
 
Exactly

Kuna desturi ya kijeshi kuwa junior anapopanda cheo zaidi ya senior senior inatakiwa astaafu

Waitara alikuwa sahihi japo sina na uhakika na zile fununu kuwa alikataa kuongezewa muda
Hii chai hiiii
 
Jkt tuliambiwa anae vaa kofia ndo anapiga salute kwahiyo unamaanisha IGP ndo anakua anawapigia hao makamishna salute huku hao makamishna wakiwa hawapigi salute wanabana mikono tu? Sasa mbona inakua siyo adabu kwa mkulu wao? Au na ww uliskia?
 
Jkt tuliambiwa anae vaa kofia ndo anapiga salute kwahiyo unamaanisha IGP ndo anakua anawapigia hao makamishna salute huku hao makamishna wakiwa hawapigi salute wanabana mikono tu? Sasa mbona inakua siyo adabu kwa mkulu wao? Au na ww uliskia?
Mbona nimeandika kitu kunaeleweka tu. IGP husalimiwa kwa ujumla. Akiwa anatoka kiongozi aliye na cheo cha juu kwanaskari waliopo eneo analopita IGP yeye hutoa ishara kwamba mkuu anapita na kuweka askari wote sawa na yeye pekee atamsalimia mkuu then anatendelea na ishu zake.

Mfano, askari mmekaa au mnafanya mambo yenu na ikawa IGP anapita, fahamu lazima officer wa zamu anakuwepo pale makao kuhakikisha ulinzi na mambo mengine yanaendelea, atakapoona mkuu anatoka yeye atawajibika kusema kwa sauti "wote sawa" then wote mnakauka yeye lazima awe kwenye full uniform atampigia salute then akijibiwa kama hakuna maelekezo atawajambia "mwili legeza" then mnaendelea na ishu zenu.



Kumbuka IGP hazururi kwenye makorido kama askari wa chini kutumwa kila saa na kuzunguka katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

Hata hivyo ili kuepuka salute wao huvua kofia ili ukikutana na boss unakauka tu, kumbuka nae hawezi kukujibu kwa salute hata kama amevaa kofia sababu wewe anayekujibu haipo kwenye uniform kamili ya kupigiwa salute ya mkono Bali ya kukauka tu.

IGP anaweza kuingia ofisini akatoka Mara moja tu.
 
Exactly

Kuna desturi ya kijeshi kuwa junior anapopanda cheo zaidi ya senior senior inatakiwa astaafu

Waitara alikuwa sahihi japo sina na uhakika na zile fununu kuwa alikataa kuongezewa muda
Its ok, lakini kwenye level ya Mkoa huwa RPCs ndio Boss wa RCO.
 
Naunga mkono hoja. MaRCO wako chini ya DCI ambaye ni presidential appointment na mzigo mkubwa wa kazi za kipolisi ni kwenye makosa ya jinai hivyo sababu RCO kuwa chini ya RPC. Wawe kwenye level moja pamoja na rank.
Na ndio inatakiwa hivyo, ili kuwe na uwazi katika utendaji, na kuepusha miingiliano katika majukumu.
 
Kuna watu mmebobea aisee, Hongera zenu.
Nadhan nahitaji kukusoma mara mbili mbili nikuelewe zaidi
 
Kuna watu mmebobea aisee, Hongera zenu.
Nadhan nahitaji kukusoma mara mbili mbili nikuelewe zaidi
Staff officer ndiye hasa nayatakiwa kuwa sawa kicheo na RPC, au ampite cheo kimoja.
 
Mkuu askari hata awe na cheo Cha CDF akikutana na askari alie vaa kiraia na akambania mikono yule CDF ikiwa anamtambua yule alie bana mikono ni askar na anauhakika kuwa ni askari Kama CDF yupo kweny full unform itambidi apige salute huku askar akiwa kabana mikono hata akiwa ni private hana cheo chochote
Hiyo ndo sheria ya salute ilivyo na siyo kweli kuwa IGP akiwa kwenye full unform hatapiga salute akiwa anasalimiwa na mtu ambae hyupo kwenye full unform kwanza askari ukivaa unform mbele ya mkubwa wako huruhusiwi kukaa bila kuvaa kofia ukimuona tu ni lazima uvae kofia hata kama ulikua umevua
Ukipitia JKT hiv vtu utavijua tu huwa wanaelekeza
 
Unazidi kuongelea JKT sisi tupo makazini tunakueleza yanayofanyika achana na nadharia.

Ukikaa makao makuu utaelewa ni utaratibu unaoeleweka sasa we sababu unataka kuleta JKT yako basi sawa.

Tuliofanya kazi muda mrefu wanaelewa. Yani siku nzima hautafanya kazi sababu ya nadharia zako utaishia kupiga saluti maana pale wakubwa kila Idara, utadhangaa wanakuambia askari relax.

Wakikuona unaleta ujkt wako watakusaidia kulainisha maisha yako ili ufanye kazi.

Salute sio kazi mzee, kazi ipo makao ni ofisi tupu mafaili yanazunguka na vikao tupu sasa salute zako zitakupotezea muda na watabaki wanakuangalia tu, acha nidhamu ya uoga wakubwa wanaangaliaga pia mazingira ukileta sana nidhamu za uoga utakuja kuishia kuwa RSM
 
Alafu huko jkt alikaa mwezi mmoja[emoji23]mara nyingine ni bora kukaa kimya na kujifunza tu.
 
Alafu huko jkt alikaa mwezi mmoja[emoji23]mara nyingine ni bora kukaa kimya na kujifunza tu.
Yani amekomaa na saluti as if ni ishu sana. Hili ni tatizo la mitaala ya kozi za kuruta wanaammbiwa saluti kila saa na smart area uwe mkakamavu wakati ukishakuwa askari smart area unakatiza tu sio ishu.

Yani kwa makao wanaopata shida ni walinzi getini na askari kiongozi wa zamu hao muda wote lazima kuwa na silaha na full uniform na Beret iwe kichwani.

Wengine sasa haipo kwenye Vita upo ofisini tu unaanza kuvaa kofia masaa yote aisee πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ hajapata kukutana na ofisi za wakubwa achana na huko vituo vya polisi unakuta mwenye nyota ni mkuu wa kituo pekee au na msaidizi wengine ni NCO tu. Huko juu kukutana na manyota ni kawaida na yapo kibao maana ndio maeneo yao wasomi na watawala wa jeshini.

Kule kuna maofisa huku chini kuna askari. Maofisa hawanaga mambo mengi ya kinoko although wanaona mwenendo wa askari.
 
Its ok, lakini kwenye level ya Mkoa huwa RPCs ndio Boss wa RCO.
Ni dhahiri kwamba polisi kwa sasa wanapaswa kutenganishwa zaidi kama ilivyokuwa zamani kwenye kuendesha mashtaka mpaka walipoondolewa hiyo power.

Hii ya kuchunguza pia waondolewe iwe no Agency inayojitegemea ili haki itendeke.

Mtu anayekukamata ndio anakupeleleza hii sio sawa anaweza kuamua kukuwekea ushahidi wa kubambikia ilimradi akukomeshe tu.

Anayepeleleza jinai watoke kwa DCI na wasiingiliane kiutawala kabisa. Anayekamata alete ushahidi, anayechunguza adhibitishe kama kuna kosa na huo ushahidi ni wa kweli then wapeleke kwa DPP ili apeleke mahakamani.

Hapo kila mmoja atakuwa na sehemu yake ya utendaji na itakuwa rahisi sana kujua nani hafanyi kazi kwa haki.

Hapa karibuni kulikuwa na malalamiko mengi sana kwamba DPP hatendi haki Mahakamani jambo ambalo sio la kweli.

DPP huletewa ushahidi na polisi waliomkamata mtu wanayemtuhumu ni muhalifu. DPP kazi yake ni kwenda mahakamani kusimama kwa niaba ya Jamhuri Ila yeye hahusiki popote zaidi ya kuletewa malalamiko na mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi.

Naelewa itatengeneza gharama katika kufungua ofisi za public investigation kila mkoa na wilaya Ila ili tuweze kutengeneza misingi ya haki ni bora kuwaachia wahalifu 100 kuliko kumfunga mwenye haki mmoja tu kwa uzembe .

Na wakifungua hizi ofisi za public investigation pia waruhusu private investigation ili kuwa na option ya upelelezi sio kutegemea polisi pekee ambao nao wanaweza kukwama kwa sababu mbalimbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…