IGP Sirro: CHADEMA wanamuona Mbowe Malaika hawezi kosea, ushahidi tunao

IGP Sirro: CHADEMA wanamuona Mbowe Malaika hawezi kosea, ushahidi tunao

sasa wakufa ni nani ? ndiyoswali la muhimu watangaze kuwa mnyika atakuwa mbele sehemu fulani wamfuate siyo anawqambia tu watu wakaandamane yeye anawaangalia kwenye tv
Kwani mnyika ulimsikiza jana! Anasem yeye atakuwa mbele kama mbowe ambaye amejitoa sadaka ili wewe upone. Hata mimi nitakuwa mbele ili we mwoga upane
 
Kama kweli una Mungu na wewe ni mfuasi wa dini tueleze umewakamata wangapi hadi leo...yale maboxsi ya kura yalioletwa na akina Mdee vituoni ( kabla hawajaasi) yako wapi?

Ahsante sana IGP kwa maelezo na makatazo, wenye akili tumekuelewa vizuri sana.

Tuache kufuata upepo kamwe tusiburuzwe, tuheshimu sheria pamoja na vyombo vinavyo simamia sheria.

Katibu Mkuu wa Chadema Mnyika na Mrema naamini wamepata ujumbe na watautekeleza.

Kwamba "Uvccm mnamshukuru Sirro kwa makatazo? Kwamba msiburuzwe? Mtaheshimu sheria na kwamba sasa mmeelewa vizuri .....?" --- Na huo utopolo mwingine wote uliojaza hapo.

Kwamba Mnyika na Lema...?

CCM ndiyo wamekutuma kuyasema hayo?

😂😂😂😂😂😂😂!

Hiiiiii bagosha!

Si bora ungekaa kimya tu jombi?
 
Akikujibu niite Mkuu, Niko smoking room one time.
 
View attachment 1877322
IGP Simon Sirro leo Agosti 2, 2021 akizungumza kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe

IGP Simon Sirro leo Agosti 2, 2021 amezungumza haya kuhusu kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe:

Mnakumbuka mnamo tarehe 17 mkoani Mwanza walikamatwa wanachama/wafuasi 15 wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (CHADEMA) Taifa Ndugu Freeman Aikael Mbowe wanachama hao walikamatwa kwa kosa la kutoa Matamshi yenye kuashiria uvunjifu wa amani nchini ikiwemo kuhamasisha/ kushawishi wananchi kwa Vitisho na Sharti kuwa lazima katiba mpya ipatikane la sivyo, yanayoendelea Afrika Kusini yatatokea Tanzania

Baada ya kukamatwa Ndugu Freeman Aikael Mbowe alipelekwa Jijini DSM ambapo kulikuwa na kesi inayopelelezwa dhidi yake kuhusiana na kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi. Watuhumiwa wenzake 6 walikuwa Mahabusu na walishafikishwa Mahakamani. Watuhumiwa wengine waliokamatwa Jijini Mwanza pamoja na Ndugu. Mbowe waliachiwa kwa dhamana. Hata hivyo baada ya upelelezi kukamilika Jalada la kesi litawasilishwa Ofisi ya Mashtaka kwa hatua zaidi

Kuhusu Mtuhumiwa Freeman Mbowe na Wenzake tuhuma dhidi yao kwa sasa iko chini ya Mamlaka ya Mahakama. Suala la dhamana kwa kesi wanayokabiliwa nayo ni la kisheria na linasimamiwa na Mahakama

Hivyo Jeshi la Polisi halitegemei mtu wala kikundi cha watu kwa namna yoyote kutoa shinikizo kwa Mamlaka ya Mahakama ama mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe aachiwa au kupewa dhamana

Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi cha Watu kitakacho jaribu kuhamisisha Mikusanyiko isiyo rasmi au kuandamana au kwa namna yoyote ile ili kutoa shinikizo lolote.
Sawa Broo
 
Tuna madhaifu?

Ni kana kwamba kuwa tunakubali kuwa mwamba ana makosa, ila chargesheet ina mapungufu.

Front page ya gazeti la raia mwema limetoa picha kamili kuwa tunabali kuwa mwamba huenda ana makosa, ila charge sheet ndio inamapungufu.

Kwa ufupi tunatakiwa kubadilika sana, maana bado tunamapungufu.
 
View attachment 1877322
IGP Simon Sirro leo Agosti 2, 2021 akizungumza kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe

IGP Simon Sirro leo Agost 2,2021 amefanya mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amezungumza mbalimbali kuhusu kukamatwa na Mwenyekiti wa Chadema pamoja na vuguvugu la kutaka kufanya maandamano. Akiwa katika mkutano huo SIrro alisema yafuatayo:

“CHADEMA wanaona Mwenyekiti wao (Mbowe) ameonewa na wanasema hawezi kuwa hivyo wanamuona ni Malaika hawezi kufanya kosa”

“Kabla ya Uchaguzi nilisema kuna Watu wamepanga kuhakikisha Uchaguzi haufanyiki, nilisema kuna baadhi ya Watu wamepanga kulipua visima vya mafuta na kufanya mauaji ya Viongozi na nilisema tutawakamata kabla hawajafanya hivyo”

“Tuliwakamata kabla, hayo ya Mwenyekiti wao (Mbowe) sitaki kuzungumzia sana lipo Mahakama ila wajue yeye ni Binadamu kama Binadamu wengine na anaweza kufanya kosa tumempeleka Mahakamani tuache Mahakama itimize wajibu wake”

“Kama kweli ni mkweli Mwenyekiti wao (Mbowe) na anamuamini Mungu waende wamuulize habari hiyo, kuna mambo unaweza kuyafanya kwamba ni siri lakini ndio mana Vyombo vya Habari vipo, niwaombe Watanzania wenzangu usilolijua ni kama usiku wa giza usiingie kwenye mtego ambao hujui aliyeutega ana jambo gani”

“Waende wamuulize huyo Mtu tuliyempeleka Mahakamani (Mbowe) kwamba hili jambo unalijua na kama ni ukweli ana Dini yake na anamjua Yesu Kristo aende aaambiwe, tunamuonea kwa lipi ?, tupate nini?, tuna ushahidi wa kutosha tuache Mahakama iamue, kafanya Yes hakufanya Yes lakini habari ya kikundi cha Watu kusema tunataka kuandamana wewe ni nani Bro!? hiyo nafasi hauna”

Awaonya Wanaotaka kuandamana
“Niwaombe Watanzania tuache wale Watu wachache ambao wanataka kupambana na Serikali wapambane nayo labda wana sababu zake lakini Mtu wenye hekima na busara anielewe, lakini kikubwa kama wameandaa kwenda Canada au Marekani wajiandae ila hatuwezi kuruhusu Watu wachache wavuruge Nchi kwasababu wamekosa madaraka”

“Habari ya kusema mnataka kuandamana mnavunja sheria na ukivunja sheria usilaumu Jeshi, ukivunja sheria umeingia kwenye uhalifu, Sirro hatokuacha na Polisi hawatokuacha na ndio maana wanafanya siasa kwa sababu amani na utulivu upo, Sisi hatufanyi Siasa”

“Niwaombe Watanzania ambao wameambiwa mkusanyike kutoka Mara kutoka wapi sijui na muelewe Mahakamana ni kituo nyeti ni kama Kituo cha Polisi ukitaka kuvamia utakung’utwa kwa mujibu wa sheria sababu umetaka sasa kama kuna Mtu maisha yamemshinda aje ila asije kulalamika, hii kesi iko Mahakamani tuiachie Mahakama iamue”
Hata MAGUFULI alioneka Yuko SAHIHI kwenye Suala la CHANJO
 
IGP amesema kama unaona Mbowe kaonewa nenda kamuulize kama kweli yeye ni mkristu safi atakwambia.

nimeona IGP kaongea kwa kujiamini sana kuwa wanao ushahidi hivyo tusubiri mahakama. huna haja ya kutoka mishipa kwa sasa, Jambo usilo lijua nisawa na usiku wa giza. tusijiingize kwenye mitego ukaja kunasa halafu huna wa kumlaumu.

kwa sasa wacha Mbowe apambane na hali yake.

Jeshi letu la polisi ni taasisi inayoshiriki uhalifu wa kimfumo hapa nchini, na sababu hasa polisi wanatumia nafasi zao kujinufaisha na rushwa. Hivyo wanachofanya jeshi la polisi na ni kulindana na chama tawala, viongozi wa serikali wanawaachia polisi wale rushwa, na viongozi wa ccm na serikali wanawatumia hao polisi kupora chaguzi.

Lakini haya yote yatafikia mwisho kwa machafuko makubwa. Ni suala la muda tu huu uchafu wote utafikia mwisho. Na uzuri tunatunza rekodi za hawa wahalifu wote, Siku kikinuka wote hawa wanaofanya uhalifu sasa kupitia madaraka yao hata wakiwa wazee lazima wawajibike. Katiba mpya ni lazima hata mfanyeje.
 
Katibu Mkuu wa chadema Mnyika anapaswa achunge sana kauli zake za kuhamasisha maandamano yenye lengo la kuvunja amani ya nchi.

Asije akalilaumu Jeshi la Polisi endapo atachukuliwa hatua za kisheria.

Huwezi kuhamasisha maandamano ya kushinikiza mahakama itoe haki!! kitendo hiki ni uvunjaji wa sheria.

Mnyika na Mrema wawe makini sana, watanzania hatuko tayari kuona watu.wachache wanajaribu kuchokonoa amani ya nchi yetu, na tunaliomba Jeshi letu kamwe lisivumilie wala kuwachekea.
Waambie ccm watoke wakae mbele, maana wao ndio wanaowaagiza polisi kubambikia washindani wa ccm kesi
 
Kama kweli una Mungu na wewe ni mfuasi wa dini tueleze umewakamata wangapi hadi leo...yale maboxsi ya kura yalioletwa na akina Mdee vituoni ( kabla hawajaasi) yako wapi?

Hata akija kustaafu, IGP Siro hatokuja kulijibu suali hilo!
 
Ukweli ni kwamba Mbowe ushahidi uwe au usiwepo Mbowe awezi kuwa gaidi kamwe
 
Waambie ccm watoke wakae mbele, maana wao ndio wanaowaagiza polisi kubambikia washindani wa ccm kesi
Jeshi la Polisi limeundwa kwa mujibu wa sheria na moja ya majukumu yake makubwa ni KULINDA RAIA NA MALI ZAO, lkn pia kulinda AMANI na UTULIVU.
haijalishi yeyote atakaye vunja sheria atachukuliwa hatua kali za kisheria bila kujali chama chake awe ccm, chadema au hata kama hana chama atachakazwa vilivyo.
Amani ya nchi yetu ni muhimu zaidi kuliko chama chochote kile.
 
FREE FREEMAN. Kilangila.
 
Kwamba "Uvccm mnamshukuru Sirro kwa makatazo? Kwamba msiburuzwe? Mtaheshimu sheria na kwamba sasa mmeelewa vizuri .....?" --- Na huo utopolo mwingine wote uliojaza hapo.

Kwamba Mnyika na Lema...?

CCM ndiyo wamekutuma kuyasema hayo?

😂😂😂😂😂😂😂!

Hiiiiii bagosha!

Si bora ungekaa kimya tu jombi?
 
View attachment 1877322
IGP Simon Sirro leo Agosti 2, 2021 akizungumza kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe

IGP Simon Sirro leo Agost 2,2021 amefanya mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amezungumza mbalimbali kuhusu kukamatwa na Mwenyekiti wa Chadema pamoja na vuguvugu la kutaka kufanya maandamano. Akiwa katika mkutano huo SIrro alisema yafuatayo:

“CHADEMA wanaona Mwenyekiti wao (Mbowe) ameonewa na wanasema hawezi kuwa hivyo wanamuona ni Malaika hawezi kufanya kosa”

“Kabla ya Uchaguzi nilisema kuna Watu wamepanga kuhakikisha Uchaguzi haufanyiki, nilisema kuna baadhi ya Watu wamepanga kulipua visima vya mafuta na kufanya mauaji ya Viongozi na nilisema tutawakamata kabla hawajafanya hivyo”

“Tuliwakamata kabla, hayo ya Mwenyekiti wao (Mbowe) sitaki kuzungumzia sana lipo Mahakama ila wajue yeye ni Binadamu kama Binadamu wengine na anaweza kufanya kosa tumempeleka Mahakamani tuache Mahakama itimize wajibu wake”

“Kama kweli ni mkweli Mwenyekiti wao (Mbowe) na anamuamini Mungu waende wamuulize habari hiyo, kuna mambo unaweza kuyafanya kwamba ni siri lakini ndio mana Vyombo vya Habari vipo, niwaombe Watanzania wenzangu usilolijua ni kama usiku wa giza usiingie kwenye mtego ambao hujui aliyeutega ana jambo gani”

“Waende wamuulize huyo Mtu tuliyempeleka Mahakamani (Mbowe) kwamba hili jambo unalijua na kama ni ukweli ana Dini yake na anamjua Yesu Kristo aende aaambiwe, tunamuonea kwa lipi ?, tupate nini?, tuna ushahidi wa kutosha tuache Mahakama iamue, kafanya Yes hakufanya Yes lakini habari ya kikundi cha Watu kusema tunataka kuandamana wewe ni nani Bro!? hiyo nafasi hauna”

Awaonya Wanaotaka kuandamana
“Niwaombe Watanzania tuache wale Watu wachache ambao wanataka kupambana na Serikali wapambane nayo labda wana sababu zake lakini Mtu wenye hekima na busara anielewe, lakini kikubwa kama wameandaa kwenda Canada au Marekani wajiandae ila hatuwezi kuruhusu Watu wachache wavuruge Nchi kwasababu wamekosa madaraka”

“Habari ya kusema mnataka kuandamana mnavunja sheria na ukivunja sheria usilaumu Jeshi, ukivunja sheria umeingia kwenye uhalifu, Sirro hatokuacha na Polisi hawatokuacha na ndio maana wanafanya siasa kwa sababu amani na utulivu upo, Sisi hatufanyi Siasa”

“Niwaombe Watanzania ambao wameambiwa mkusanyike kutoka Mara kutoka wapi sijui na muelewe Mahakamana ni kituo nyeti ni kama Kituo cha Polisi ukitaka kuvamia utakung’utwa kwa mujibu wa sheria sababu umetaka sasa kama kuna Mtu maisha yamemshinda aje ila asije kulalamika, hii kesi iko Mahakamani tuiachie Mahakama iamue”
Hivi huyo ziro anajiona ana akili kuliko watu wenye akili zao?
 
Back
Top Bottom