View attachment 1877322
IGP Simon Sirro leo Agosti 2, 2021 akizungumza kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe
IGP Simon Sirro leo Agosti 2, 2021 amezungumza haya kuhusu kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe:
Mnakumbuka mnamo tarehe 17 mkoani Mwanza walikamatwa wanachama/wafuasi 15 wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (CHADEMA) Taifa Ndugu Freeman Aikael Mbowe wanachama hao walikamatwa kwa kosa la kutoa Matamshi yenye kuashiria uvunjifu wa amani nchini ikiwemo kuhamasisha/ kushawishi wananchi kwa Vitisho na Sharti kuwa lazima katiba mpya ipatikane la sivyo, yanayoendelea Afrika Kusini yatatokea Tanzania
Baada ya kukamatwa Ndugu Freeman Aikael Mbowe alipelekwa Jijini DSM ambapo kulikuwa na kesi inayopelelezwa dhidi yake kuhusiana na kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi. Watuhumiwa wenzake 6 walikuwa Mahabusu na walishafikishwa Mahakamani. Watuhumiwa wengine waliokamatwa Jijini Mwanza pamoja na Ndugu. Mbowe waliachiwa kwa dhamana. Hata hivyo baada ya upelelezi kukamilika Jalada la kesi litawasilishwa Ofisi ya Mashtaka kwa hatua zaidi
Kuhusu Mtuhumiwa Freeman Mbowe na Wenzake tuhuma dhidi yao kwa sasa iko chini ya Mamlaka ya Mahakama. Suala la dhamana kwa kesi wanayokabiliwa nayo ni la kisheria na linasimamiwa na Mahakama
Hivyo Jeshi la Polisi halitegemei mtu wala kikundi cha watu kwa namna yoyote kutoa shinikizo kwa Mamlaka ya Mahakama ama mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe aachiwa au kupewa dhamana
Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi cha Watu kitakacho jaribu kuhamisisha Mikusanyiko isiyo rasmi au kuandamana au kwa namna yoyote ile ili kutoa shinikizo lolote.