post yangu inahusu matusi....Hahaha jibu hoja jomba msilopoke hovyo Bila data...mtafungwa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
post yangu inahusu matusi....Hahaha jibu hoja jomba msilopoke hovyo Bila data...mtafungwa
Kuandamana mahakamani. ...???basi tangulia mbele uongoze wengine wakufuateLabdakama hukumsikiliza amesema maandamano ya amani ambayo yanaruhusiwa kisheria sasa achunge nini Kwani kwenye nchi za demokrasia kuandamana sasa limekuwa kosa la jinai nani amewahi kufungwa kwa kosa la kuandamana hebu tusifanywe wajinga.
Kwani sheria gani ya nchi hii inayosema kwamba watu wakiandamana adhabu ni kupigwa na police?We wachuuze tu wenzio wakati wewe utakuwepo mahakamani kwa kutmia mitandao wenzio wakapondwe pondwe wavunjwe miguu keshoyake uje tena kuwapa pole na kulaumu polisi sana
Mimi sio mwanachama wa chama wa chama chochote cha siasa ila sipendi uonevu kwa raia.We wachuuze tu wenzio wakati wewe utakuwepo mahakamani kwa kutmia mitandao wenzio wakapondwe pondwe wavunjwe miguu keshoyake uje tena kuwapa pole na kulaumu polisi sana
Hakika !Hata IGP wa Al Bashir naye alitoa mkwara kama huu huu lakini kilichompata anakijua.
Naomba kueleweshwa kwa mujibu wa sheria ni wapi kuandamana kumepewa jina la uvunjifu wa amani?Ahsante sana IGP kwa maelezo na makatazo, wenye akili tumekuelewa vizuri sana.
Tuache kufuata upepo kamwe tusiburuzwe, tuheshimu sheria pamoja na vyombo vinavyo simamia sheria.
Katibu Mkuu wa Chadema Mnyika na Mrema naamini wamepata ujumbe na watautekeleza.
Utafanya nini kwa mfano!!!Hata IGP wa Al Bashir naye alitoa mkwara kama huu huu lakini kilichompata anakijua.
nyinyi mlimjaza misifa kisha akavimba akajiona kweli yeye ni mwamba sasa ona matokeo yake ameangamia kwa matendo yake.Wewe Siro kama kweli unamjua Yesu tuambie nani alimpiga Lissu risasi na ni kweli askari wako walisimamia haki ktk uchaguzi ulopita?
Kama Mbowe ni gaidi basi we ni gaidi mara alf moja ya Mbowe kwa yale unayoyasimamia.
Huna haki ya kulitaja jina la Yesu katika mambo yako ya kishetani...
Na ushindwee, kwa jina la Yesuuu...
Mwachieni Mbowe nyie waovu...
wewe nenda ukaandamane na familia yako utaonekana jasiri sana.Labda kama hukumsikiliza amesema maandamano ya amani ambayo yanaruhusiwa kisheria sasa achunge nini Kwani kwenye nchi za demokrasia kuandamana sasa limekuwa kosa la jinai nani amewahi kufungwa kwa kosa la kuandamana hebu tusifanywe wajinga.
Katiba mpya tunaitaka,Mbowe MUACHIENI ,tarehe tano lazima nikatimeze takwa langu la kikatiba,maandamano ya amani, mh IGP ni haki YENU kulinda maandamano ya amani,View attachment 1877322
IGP Simon Sirro leo Agosti 2, 2021 akizungumza kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe
IGP Simon Sirro leo Agost 2,2021 amefanya mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amezungumza mbalimbali kuhusu kukamatwa na Mwenyekiti wa Chadema pamoja na vuguvugu la kutaka kufanya maandamano. Akiwa katika mkutano huo SIrro alisema yafuatayo:
“CHADEMA wanaona Mwenyekiti wao (Mbowe) ameonewa na wanasema hawezi kuwa hivyo wanamuona ni Malaika hawezi kufanya kosa”
“Kabla ya Uchaguzi nilisema kuna Watu wamepanga kuhakikisha Uchaguzi haufanyiki, nilisema kuna baadhi ya Watu wamepanga kulipua visima vya mafuta na kufanya mauaji ya Viongozi na nilisema tutawakamata kabla hawajafanya hivyo”
“Tuliwakamata kabla, hayo ya Mwenyekiti wao (Mbowe) sitaki kuzungumzia sana lipo Mahakama ila wajue yeye ni Binadamu kama Binadamu wengine na anaweza kufanya kosa tumempeleka Mahakamani tuache Mahakama itimize wajibu wake”
“Kama kweli ni mkweli Mwenyekiti wao (Mbowe) na anamuamini Mungu waende wamuulize habari hiyo, kuna mambo unaweza kuyafanya kwamba ni siri lakini ndio mana Vyombo vya Habari vipo, niwaombe Watanzania wenzangu usilolijua ni kama usiku wa giza usiingie kwenye mtego ambao hujui aliyeutega ana jambo gani”
“Waende wamuulize huyo Mtu tuliyempeleka Mahakamani (Mbowe) kwamba hili jambo unalijua na kama ni ukweli ana Dini yake na anamjua Yesu Kristo aende aaambiwe, tunamuonea kwa lipi ?, tupate nini?, tuna ushahidi wa kutosha tuache Mahakama iamue, kafanya Yes hakufanya Yes lakini habari ya kikundi cha Watu kusema tunataka kuandamana wewe ni nani Bro!? hiyo nafasi hauna”
Awaonya Wanaotaka kuandamana
“Niwaombe Watanzania tuache wale Watu wachache ambao wanataka kupambana na Serikali wapambane nayo labda wana sababu zake lakini Mtu wenye hekima na busara anielewe, lakini kikubwa kama wameandaa kwenda Canada au Marekani wajiandae ila hatuwezi kuruhusu Watu wachache wavuruge Nchi kwasababu wamekosa madaraka”
“Habari ya kusema mnataka kuandamana mnavunja sheria na ukivunja sheria usilaumu Jeshi, ukivunja sheria umeingia kwenye uhalifu, Sirro hatokuacha na Polisi hawatokuacha na ndio maana wanafanya siasa kwa sababu amani na utulivu upo, Sisi hatufanyi Siasa”
“Niwaombe Watanzania ambao wameambiwa mkusanyike kutoka Mara kutoka wapi sijui na muelewe Mahakamana ni kituo nyeti ni kama Kituo cha Polisi ukitaka kuvamia utakung’utwa kwa mujibu wa sheria sababu umetaka sasa kama kuna Mtu maisha yamemshinda aje ila asije kulalamika, hii kesi iko Mahakamani tuiachie Mahakama iamue”