IGP Sirro: CHADEMA wanamuona Mbowe Malaika hawezi kosea, ushahidi tunao

Labdakama hukumsikiliza amesema maandamano ya amani ambayo yanaruhusiwa kisheria sasa achunge nini Kwani kwenye nchi za demokrasia kuandamana sasa limekuwa kosa la jinai nani amewahi kufungwa kwa kosa la kuandamana hebu tusifanywe wajinga.
Kuandamana mahakamani. ...???basi tangulia mbele uongoze wengine wakufuate
 
We wachuuze tu wenzio wakati wewe utakuwepo mahakamani kwa kutmia mitandao wenzio wakapondwe pondwe wavunjwe miguu keshoyake uje tena kuwapa pole na kulaumu polisi sana
Kwani sheria gani ya nchi hii inayosema kwamba watu wakiandamana adhabu ni kupigwa na police?

Au mmezoea tu kuvunja sheria?

Halafu tangu lini maandamano ya amani yakawa uvunjifu wa sheria? Mbona katiba imeweka wazi haki ya kuandamana?
 
We wachuuze tu wenzio wakati wewe utakuwepo mahakamani kwa kutmia mitandao wenzio wakapondwe pondwe wavunjwe miguu keshoyake uje tena kuwapa pole na kulaumu polisi sana
Mimi sio mwanachama wa chama wa chama chochote cha siasa ila sipendi uonevu kwa raia.

Pia wapo watu waliokuwa wakiongea jeuri wakiwa madarakani wakiamini jeshi lao lipo imara kuwashughulikia raia pasipo makosa ila raia walipochoka kilichofuata hao hao viongozi wa juu walitoroka wakiwa wamevalia mabaibui kukwepa kisasi kutoka kwa wananchi waliochafukwa.
 
Kitu pekee Polisi wa kitanzania hawajawahi kudanganya ni wakisema watakupiga mpaka uchakae.Hakika utachakaa
 
Naomba kueleweshwa kwa mujibu wa sheria ni wapi kuandamana kumepewa jina la uvunjifu wa amani?

Naomba kifungu cha sheria kinachotaja maandamano kama uvunjifu wa sheria.Nijuavyo maandamano ni haki ya raia kueleza masahibu au uungaji mkono jambo fulani.
 
Kwamba Mbowe alipanga kufanya Ugaidi bila kumshirikisha kiongozi yeyote wa Chadema?
 
Hili jeshi naona wamekosa kazi ya kufanya tangu kuisha kwa kagera war

Kama wanajiona wanajimudu kiuwezo, yaani wana mafunzo ya kutosha si angalau hata waende hapo Cabo Delgado au Somalia, wakapimane nguvu na wenye silaha wenzao, sisi CDM hatuna hata panga
 
Wewe Siro kama kweli unamjua Yesu tuambie nani alimpiga Lissu risasi na ni kweli askari wako walisimamia haki ktk uchaguzi ulopita?

Kama Mbowe ni gaidi basi we ni gaidi mara alf moja ya Mbowe kwa yale unayoyasimamia.

Huna haki ya kulitaja jina la Yesu katika mambo yako ya kishetani...

Na ushindwee, kwa jina la Yesu.

Mwachieni Mbowe nyie waovu.
 
Na najiuliza hivi uchaguzi mkuu uko mbele au? Mbona hakuna visima vilivyolipuliwa na wakati uchaguzi umeshaisha?

Ni nini kilimzuia asitimize azma yake? Na nyie kujua mtu ana nia kama hiyo mmuache uraiani toka mwaka jana hadi leo? Kwelii?

Mwachieni Mbowe nyie waovu...
 
nyinyi mlimjaza misifa kisha akavimba akajiona kweli yeye ni mwamba sasa ona matokeo yake ameangamia kwa matendo yake.
 
Mara Nyingine mimi huwa namlaumu Mchonga kwa kuliua Jeshi la Polisi tuliolirithi kutoka kwa Waingereza na kulitengeneza hili jeshi la Polisi ambalo lilifanywa kuwa la TANU na hata baada ya CCM kuzaliwa limekuwa la CCM

Tukiongelea kulivunja watu wanadhani nimetumwa na Mabeberu aisee!! ona sasa Wakoloni weusi wanavyotutesa.
 
Labda kama hukumsikiliza amesema maandamano ya amani ambayo yanaruhusiwa kisheria sasa achunge nini Kwani kwenye nchi za demokrasia kuandamana sasa limekuwa kosa la jinai nani amewahi kufungwa kwa kosa la kuandamana hebu tusifanywe wajinga.
wewe nenda ukaandamane na familia yako utaonekana jasiri sana.
 
Katiba mpya tunaitaka,Mbowe MUACHIENI ,tarehe tano lazima nikatimeze takwa langu la kikatiba,maandamano ya amani, mh IGP ni haki YENU kulinda maandamano ya amani,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…