IGP Sirro: Jeshi la Polisi kukagua yanayofundishwa kwenye nyumba za Ibada

IGP Sirro: Jeshi la Polisi kukagua yanayofundishwa kwenye nyumba za Ibada

Fuatilia vizuri si kuongea tu Jambo ambalo hulijui au hujafanyia utafiti. Hao wapo huko Kila siku wanajua wanachokiongea. Mimi nikiwa chuo mwaka 2012 niliyasikia hayo kwa watu wa mtaani. Wanayajua Sana tu kuwa Kuna mambo yanaendelea huku mtaani si mazuri walisema watoto wa sekondari wanasajiliwa kwenye makundi ya kigaidi

Uliyasikia kumbe, na wala hujashuhudia!!!!! Aise acha kwenda vijiwe vya kahawa.
 
IGP Sirro amesema jeshi lake litaanza kukagua yale yanayofundishwa kwenye nyumba za ibada.

Chanzo: Swahili times

My take; Baadhi ya nyumba za ibada huzalisha magaidi kwa kufundisha kareti.
===
Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa litakuwa likipita katika nyumba za ibada kukagua mafunzo wanayofundishwa watoto katika madrasa na shule za Jumapili (Sunday schools) kufahamu aina ya mafundisho yanayotolewa.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro ameeleza hayo wakati akizungumzia ziara yake ya siku nne nchini Rwanda na kusema wamejifunza hilo kutoka huko, hivyo ni vyema wapite kwenye maneno hayo kujua malengo ya mafunzo yanayotolewa.

“Tumeona wenzetu hizi shule za dini, kwa mfano haya Madrasa, kwa mfano hizo Sunday schools kuna kikosi maalum kuona mafunzo yanayofundishwa. Je! Mafunzo yale yanatolewa kwa ajili ya uzalendo, au ni mafunzo yanayotolewa kwa ajili ya kuharibu nchi,” amesema Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Sirro ameeleza utaratibu huo ni mzuri na kwamba watawashirikisha viongozi wa dini na timu ya kupambana na makosa ya kigaidi kuona namna ya kupitia mafunzo yanayofundishwa kwenye shule za dini na shule za elimu dunia, hadi ngazi ya vyuo vikuu, kuona kama mafunzo yanawajenga au yanawabomoa vijana.

Aidha, ameitaka jamii kutoa taarifa endapo itabaini kuna mtu ana tabia au mwenendo kinyume na jamii husika, na kwamba sio lazima mhusika afungwe, bali wanaweza kumsaidia kuwa mtu mwema na akaendelea na shughuli zake.
Kwa hiyo Rwanda ndio imekuwa role model wetu? Hivi wao hasa wanautulivu, amani na demokrasia nzuri kiasi cha sisi kwenda kwao kusoma na kuiga?
 
IGP fanyeni kiintelligensia msitangaze vinginevyo wata-pretend kuacha kwa muda kisha badae kuendelea!

Fanyeni kisiri siri!

Hilo jambo ni muhimu sana na wala msirudi nyuma ktk kulitekeleza, isipokuwa fanyeni kwa siri na ustadi mkubwa ili kuweze kutimiza lengo !
 
Sambamba na hilo andaeni regular seminars za Viongozi wa dini wakafundishe waamini wao kuhusu namna ya kubaini magaidi, madhara yatokanayo na Ugaidi na jinsi ya kuepuka Ugaidi na usiri ktk kutolea taarifa na mtoa taarifa kulindwa kwa kiapo!
 
Mashuleni mpaka mikoani jipangeni mkawaelimishe Walimu na wanafunzi kuhusu hilo jambo.

Mnakumbuka yule mwanafunzi wa Bihawana kule Dodoma aliyekamatwa kule Chuo cha Gharisa nchini Kenya kwenye tukio la mauaji la kigaidi?

Rashid Mberesero, unaambiwa alikuwa anashinda msikitini darasani haingii mzazi wake(mama) yake alilia sana kumbe mwanae alikuwa anajifunza kuua watu wasio na hatia!

Pateni Picha!
 
IGP Sirro amesema jeshi lake litaanza kukagua yale yanayofundishwa kwenye nyumba za ibada.

Chanzo: Swahili times

My take; Baadhi ya nyumba za ibada huzalisha magaidi kwa kufundisha kareti.
===
Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa litakuwa likipita katika nyumba za ibada kukagua mafunzo wanayofundishwa watoto katika madrasa na shule za Jumapili (Sunday schools) kufahamu aina ya mafundisho yanayotolewa.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro ameeleza hayo wakati akizungumzia ziara yake ya siku nne nchini Rwanda na kusema wamejifunza hilo kutoka huko, hivyo ni vyema wapite kwenye maneno hayo kujua malengo ya mafunzo yanayotolewa.

“Tumeona wenzetu hizi shule za dini, kwa mfano haya Madrasa, kwa mfano hizo Sunday schools kuna kikosi maalum kuona mafunzo yanayofundishwa. Je! Mafunzo yale yanatolewa kwa ajili ya uzalendo, au ni mafunzo yanayotolewa kwa ajili ya kuharibu nchi,” amesema Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Sirro ameeleza utaratibu huo ni mzuri na kwamba watawashirikisha viongozi wa dini na timu ya kupambana na makosa ya kigaidi kuona namna ya kupitia mafunzo yanayofundishwa kwenye shule za dini na shule za elimu dunia, hadi ngazi ya vyuo vikuu, kuona kama mafunzo yanawajenga au yanawabomoa vijana.

Aidha, ameitaka jamii kutoa taarifa endapo itabaini kuna mtu ana tabia au mwenendo kinyume na jamii husika, na kwamba sio lazima mhusika afungwe, bali wanaweza kumsaidia kuwa mtu mwema na akaendelea na shughuli zake.
Kareti haaaa
 
OCDs, Afisa usalama wa Wilaya , wakuu wa vituo wapate semina halafu wahakikishe kwenye kila Wilaya , Tarafa, Kata , vijiji na vitongoji vyao watu wote wa dini zote na wale wasio na dini kupitia wajumbe wa nyumba 50 wote wapate awareness ya jambo hilo la Ugaidi.
 
Ovyo kabisa, Trump aliita africa whole shit akimaanisha kwamba bado tuko zama za ujinga, uncivilized, eti wafahanu mafundisho ya madrasa za kiibada sasa haya mambo wap na wap ni kama vile akili zao zimegonga wameshindwa kubuni mambo ya kitaalamu au hata kujifunza kw nchi wenzetu uko nje sio kama hapo kw kagame.,

Siro mpaka kuja kuzifahamu madrasa za dini itamkosti muda kiasi gani ili apate nini.,
 
mtahangaika sana kama Polisi msipobadilika na kuacha dhulma dhidi ya Raia tutazidi kuwachukia mmoja wao ni mimi mpaka naingia kaburini nina bifu na polisi kwa walionifanyia...

mtasingizia madrasa na sunday school 🏫
 
Lengo lao ni kumfunga mboye then sisi polisccm tuende kwenye nyumba za ibada tukasikilize viongozi wa dini na waumin wao watazungumza nini baada ya kifungo
 
Amesema hizi mbinu za kudeal na nyumba za ibada wamejifunzia Rwanda na watazitumia kweri-kweri hapa Tozonia.
 
Gwajiboy anawafanya waweweseke yaani. Gwajiboy yeye anasoma upepo tu kwamba akasemee kanisani au bungeni. Inawezekana aliutafuta ubunge kwa malengo ambayo hata CCM hawayajui
 
Mtu hafundishwi uzalendo...anajengwa na matendo mema ya watawala kuwa mzalendo
 
Akakague kwanza kile chuo cha polissi Moshi kuweza kujua polisi wanafundishwa nini kule kiasi cha kuwafanya kuwa genge la waovu badala ya kuwa walinzi na watunzaji wa usalama na amani.
Inawezekana huko Moshi CCP polisi wanafundishwa namna ya kutoza ushuru!
 
Ovyo kabisa, Trump aliita africa whole shit akimaanisha kwamba bado tuko zama za ujinga, uncivilized, eti wafahanu mafundisho ya madrasa za kiibada sasa haya mambo wap na wap ni kama vile akili zao zimegonga wameshindwa kubuni mambo ya kitaalamu au hata kujifunza kw nchi wenzetu uko nje sio kama hapo kw kagame.,

Siro mpaka kuja kuzifahamu madrasa za dini itamkosti muda kiasi gani ili apate nini.,

Huyo mzee akae mbali na dini ya Mwenyezi Mungu,, otherwise itamcost yeye na familia yake+watumwa wake/Polisi.
 
Wewe na wauwaji wenzio hamjachoka kuua watu na kuwatupa baharini sio! Basi tafuteni mbinu nyingine sio hizo za kutoa namba za simu umwambie mtu apige kwani umesikia natafuta namba ya mtu,jinga sana.
Pole sana, usilolijua litakusumbua!
 
Back
Top Bottom