IGP Sirro soma alama za nyakati, jiuzulu
Yaani huyo jamaa alipokuwa kitengo cha trafiki dar, aliogopwa mno!!kwani yeye hataki maneno,kama umefanya kosa, kwanza unatiwa ndani, na faini juu, au mahakamani!!na hata polisi wa chini walikuwa wakimuogopa sana!!
Exactly, Mimi nakumbuka mwaka 2004 aling'oa plate number za daladala yangu kosta, kisa dereva sijui alitanua, alikuwa na dada mmoja anaitwa Fatuma,jamaa anapiga kazi haswaa
 
Kwa uozo uliopo ndani ya chombo unachokisimamia Kama mkuu wake huoni kuwa huenda umechoka na kuishiwa mbinu kiasi kwamba imekuwa fedheha kwako Kama kiongozi jitathimini hata ukisimama mbele ya Mh Rais uone aibu jeshi limepoteza WELEDI kwa kasi sana Tangu IGP MAHITA alipokuwepo na wewe ndio umelipeleka porini kabisaa chukua KALAMU NA KARATASI UMSHUKURU MH RAIS ILI MTAANI UHESHIMIWE MUDA NI MWALIMU MZURI UTAKUUMBUA JIUZULU ASANTE
Kinachoshangaza zaidi ni kuwa aliyemteua haoni aibu hii. Sirro anajiaibisha mwenyewe, anamwaibisha aliemteua na analiaibisha taifa. Yanayotokea kwenye kesi ya Mbowe intatia kinyaa. JIUZURU LIEPUSHE TAIFA NA AIBU HII HATA KAMA ALIEKUTEUA HAIONI.
 
Hahaaa!!njaa babaaa, ki ukweli kwa sasa jeshi la polisi limerudi enzi zile za mahita!!Said mwema alijitahidi sana kulirudisha kwenye mstari na akafanikiwa kabisa!!sasa huyu yeye ana amini ktk nguvu na vitisho tu, na sio kwenye weredi!!ila mama kwa kutoa maagizo ya kuundwa kamati ya uchunguzi, na ripoti yake ikafanyiwa kazi inaweza leta mabadiriko, chanzo ni awamu ya 5, kwani jiwe naye aliamini zaidi kwenye utumiaji nguvu na vitisho!!Kama vipi huyo kamishina mpya (Awadhi)wa jeshi la polisi zanzibar apewe u IGP, tu, kwani umakini wake unajulikana sana, wakati akiwa dar, waulize madreva wa daldala habari zake wanazo!!Siro kwa sasa mbinu zimemuishia kabisa, japo huko nyuma alionekana mtu makini sana, kabla hajawa igp!!
Naunga mkono ni wakati muafaka sasa kwa IGP kutokea Zanzibar.
 
Kongole wana JF, kutokana na malalamio ya wananchi juu ya mwenendo wa jeshi la polisi na baadaye matamko ya viongozi wakuu akiwemo rais, waziri mkuu na waziri wa mambo kutilia shaka mwenendo wa jeshi la polisi hadi kufikia PM kuunda tume ya kuchunguza mauaji ya kijana kule Mtwara ambapo polisi wanatuhumiwa kuhusika.

Je, ni busara kwa IGP kuendelea kukalia kiti pasipo kuwajibika, au ndo ile kusubiri kutenguliwa.

Nawasilisha.​
Sio busara lakini Acha ibaki hivyo hivyo!
 
Kongole wana JF, kutokana na malalamio ya wananchi juu ya mwenendo wa jeshi la polisi na baadaye matamko ya viongozi wakuu akiwemo rais, waziri mkuu na waziri wa mambo kutilia shaka mwenendo wa jeshi la polisi hadi kufikia PM kuunda tume ya kuchunguza mauaji ya kijana kule Mtwara ambapo polisi wanatuhumiwa kuhusika.

Je, ni busara kwa IGP kuendelea kukalia kiti pasipo kuwajibika, au ndo ile kusubiri kutenguliwa.

Nawasilisha.​
Hakutakiwa kuwepo kwenye hiyo nafasi tangu mwanzoni mwa mwaka huu
 
Alipaswa aandike barua ya kujiuzulu muda mrefu sana, kuanzia 2017 matukio ya watu kuokotwa kwenye viroba ufukweni na kwenye mito. Askari polisi walivogeuka kuwa TRA kukusanya mapato kwa madereva barabarani na walivokua wakionea madereva barabarani na fine za ajabu.

IGP yupo kwaajili ya kuongozaa ulinzi wa raia na mali zao, ila cha ajaabu nchi hii ni kinyume, yupo kwaajili ya kutetea maovu ya askari wanaofanyia raia.
 
Ikifika next week hajajiuzulu wala kutumbuliwa ...nitabaki na maswali na mshangao wangu moyoni
 
madaraka matu acheni nyie.Mama mwenyewe aliposikia 2025 hato pita alikuwa mkali kama pilipili
 
Kutokuona aibu kwa waswahili mbona kawaida kwa mengi tu

Huyu nae wale wale aone aibu wapi
Yaani mswahili anakuibia unamfukuza kama mbwa halafu baada ya mda anakuja kujikomba na kukusalimia na kukuomba tena hela hata kazi

Hao ndio waswahili bwana
 
Tena Kaza hivyohivyo wala haina haja ya kujiuzuri kuna orodha lakini hatutakubali. Kumbukeni nguvu ya umaa ni nguvu ya Mungu!
 
Back
Top Bottom