IGP Sirro soma alama za nyakati, jiuzulu
Kwa uozo uliopo ndani ya chombo unachokisimamia Kama mkuu wake huoni kuwa huenda umechoka na kuishiwa mbinu kiasi kwamba imekuwa fedheha kwako Kama kiongozi jitathimini hata ukisimama mbele ya Mh Rais uone aibu jeshi limepoteza WELEDI kwa kasi sana Tangu IGP MAHITA alipokuwepo na wewe ndio umelipeleka porini kabisaa chukua KALAMU NA KARATASI UMSHUKURU MH RAIS ILI MTAANI UHESHIMIWE MUDA NI MWALIMU MZURI UTAKUUMBUA JIUZULU ASANTE
Ni wakati sasa jeshi hili liongozwe na utamaduni wa Ki JWTZ ambalo limejizolea uaminifu kwa wananchi tuletee IGP kutoka huko iwapo tunataka mabadiliko serious halafu chini asaidiwe na timu ya akina Awadhi, Suzana Kaganda, RPC dsm na yule bosi wa Takukuru nk. Mabadiliko makubwa ya kimtizamo na kiutendaji yatapatikana. Inahitajika transformation kubwa. Polisi ndiyo kioo cha serikali na Taifa kinahitaji kuongozwa kiweledi, uaminifu na bila upendeleo au uonevu wa aina yoyote. Baada ya hapo wapewe mafunzo yenye mwelekeo wa kulinda haki za binadamu lakini kufanya kazi kisayansi teknolojia na maslahi bora na bila kuacha mbinu zilizowasaidia kukomesha ujambazi na uhalifu sugu uilokuwa tishio miaka ya nyuma.
 
MSAMEHENI AIJIPII....AMEKOSA...AMEKOSA YEYE....AMEKOSA SANA ! NAMSHAURI ASIJIUZULU BALI AOMBE LAZI KWA HANGAYA
 
Hahaaa!!njaa babaaa, ki ukweli kwa sasa jeshi la polisi limerudi enzi zile za mahita!!Said mwema alijitahidi sana kulirudisha kwenye mstari na akafanikiwa kabisa!!sasa huyu yeye ana amini ktk nguvu na vitisho tu, na sio kwenye weredi!!ila mama kwa kutoa maagizo ya kuundwa kamati ya uchunguzi, na ripoti yake ikafanyiwa kazi inaweza leta mabadiriko, chanzo ni awamu ya 5, kwani jiwe naye aliamini zaidi kwenye utumiaji nguvu na vitisho!!Kama vipi huyo kamishina mpya (Awadhi)wa jeshi la polisi zanzibar apewe u IGP, tu, kwani umakini wake unajulikana sana, wakati akiwa dar, waulize madreva wa daldala habari zake wanazo!!Siro kwa sasa mbinu zimemuishia kabisa, japo huko nyuma alionekana mtu makini sana, kabla hajawa igp!!
Askari wasio waadilifu kiboko yao ni Awadhi, wanamjua haswaa,

angepewa Awadhi u-IGP hili alinyooshe jeshi la polisi na kukomesha matukio ya hovyo,au ikishindikana ateuliwa meja general kutoka JW awe IGP
 
Askari wasio waadilifu kiboko yao ni Awadhi, wanamjua haswaa,

angepewa Awadhi u-IGP hili alinyooshe jeshi la polisi na kukomesha matukio ya hovyo,au ikishindikana ateuliwa meja general kutoka JW awe IGP
Yaani huyo jamaa alipokuwa kitengo cha trafiki dar, aliogopwa mno!!kwani yeye hataki maneno,kama umefanya kosa, kwanza unatiwa ndani, na faini juu, au mahakamani!!na hata polisi wa chini walikuwa wakimuogopa sana!!
 
Kongole wana JF, kutokana na malalamio ya wananchi juu ya mwenendo wa jeshi la polisi na baadaye matamko ya viongozi wakuu akiwemo rais, waziri mkuu na waziri wa mambo kutilia shaka mwenendo wa jeshi la polisi hadi kufikia PM kuunda tume ya kuchunguza mauaji ya kijana kule Mtwara ambapo polisi wanatuhumiwa kuhusika.

Je, ni busara kwa IGP kuendelea kukalia kiti pasipo kuwajibika, au ndo ile kusubiri kutenguliwa.

Nawasilisha.​
 
Nyakoro Sirro Simoni tunasubiri ushahidi wake mahakamani hivyo tunataka aje akiwa siyo mstaafu.... HUYU NI MUONGO NA MUHUNI SANA... Anajua walipo Ben Sanane, Azory Gwanda na kilichowakuta Lissu, Kabendera, Roma na Mohamed Dewji Sirro anafahamu vizuri. HUYU INGEKUWA NCHI ZENYE KATIBA MADHUBUTI NI WA KUSHTAKIWA MAHAKAMANI NA AFUNGWE MAISHA.
 
Kama waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani bado wapo ofisini, kwann iwe dhambi kwa IGP kuendelea kuwepo ofisini?

I stand with IGP.

Mfumo wetu wa hovyo Sana. Mabomu yalilipuka yakauwa watu mara mbili waziri wa ulinzi wa wakati huo akakaa kimya na ndiye rais wa Zanzibar hivi sasa.

Only in Tanzania!
 
IGP na waziri wake wa mambo ya ndani na rpc wa mkoa wa mtwara ,wasingesubiri second call kabisa,ilitakiwa wajiweke pembeni kupisha hizi tume to investigate (ingawa binafsi sipendi kabisa hizi tume,kwa kesi hizi za police ilitakiwa tuwe na IPID ,hawa ndio wangefanya uchunguzi wa kesi hii).
 
Na aibu ya mkoa wa Mara
" Nimemuagiza Waziri Mkuu,kuunda tume kuchunguza tuhuma za mauaji yaliyofanywa na Polisi- Mtwara.Polisi hawawezi kujichunguza wenyewe"Rais Samia Suluhu,akiwa njiani kuelekea Mara.
 
"Ingekuwa wewe ni aijipii, halafu hali hii inatokea na unashinikizwa ujiuzulu, ungejisikiaje"? (Sauti ya aijipii)
 
Kamanda Siro usitoke! Atoke kwanza waziri mkuu halafu waziri wa mambo ya ndani ndipo Siro uondoke.

Siro narudia tena usiondoke kizembe kwa kusikiliza maneno ya wadanganyika. Komaa.
 
Kwa uozo uliopo ndani ya chombo unachokisimamia Kama mkuu wake huoni kuwa huenda umechoka na kuishiwa mbinu kiasi kwamba imekuwa fedheha kwako Kama kiongozi jitathimini hata ukisimama mbele ya Mh Rais uone aibu jeshi limepoteza WELEDI kwa kasi sana Tangu IGP MAHITA alipokuwepo na wewe ndio umelipeleka porini kabisaa chukua KALAMU NA KARATASI UMSHUKURU MH RAIS ILI MTAANI UHESHIMIWE MUDA NI MWALIMU MZURI UTAKUUMBUA JIUZULU ASANTE
Tupate IGP mpya kutoka ZANZIBAR, serikali ni ya muungano lakini Ma-IGP wamekuwa wakitoka bara tu., mama alione na hili.
 
Back
Top Bottom