IGP Sirro soma alama za nyakati, jiuzulu
SIRRO na mkuu wa Intellijensia wote wafutwe kazi maana malalamiko, uonevu, mauaji na ubambikiaji kesi watu umeshika kasi kwenye uongozi wa hawa watu wawili.

Hivyo naunga mkono hoja eitha wajiuzuru ama wafutwe kazi kwa ulazima.
 
Toka tupate Uhuru tumekuwana IGP wengi lakini kati ya hao wote haijawahi tokea wakati Jeshi la Polisi limelaumiwa kama ilivyo chini ya uongozi wa Sirro. Enzi ya awamu ya kwanza kulitokea kashfa ya mauaji ya Shinyanga na IGP wa wakati huo ambae kwa bahati mbaya simkumbuki jina pamoja na waziri wake mzee Mwenyi na aliyekuwa mshauri wa masuala ya usalama mzee Paul Sozigwa waliwajibika kwa kujiuzulu.

Vivyo hivyo kwa mauaji ya Kilombero viongozi waliwajibika pamoja na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro hayati Chrisant Majiyatanga Mzindakaya.

Toka tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi vurugu na mauaji yamekuwa yakitokea enzi ya mzee Mahita, Saidi Mwema na wengine lakini si kwa kiwango cha kufikia enzi hizi za IGP Sirro. Maafa ya raia yanaweza kuweka kwenye makundi matatu:

1) Watu kupotea bila ya polisi kutoa maelezo yoyote au watuhumiwa kufikishwa mahakamani. Mifano no Azori Gwamba mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi, Ben Saanane msaidizi wa mwenyekiti CHADEMA, vijana watano waliopotea katika mazingira ya ktatanisha n.k.

2) Kupigwa risasi Tundu Lissu kwenye eneo lenye ulinzi wa polisi 24/7.

3) Watu kutekwa katika mazingira ya kutatanisha kama vile kutekwa kwa Mo Dewji, kutekwa kwa wasanii Nay wa Mitego na Roma Mkatoliki.

4) Watu kuuawa bila polisi kutoa taarifa za uchunguzi mifano ni diwani wa CHADEMA Namawala, maiti zilizookotwa baharini, maiti mto Ruvu nk.

5) Mbaya kuliko zote no watu kuuawa wakiwa mikomoni mwa polisi. Mfano wa karibu kabisa ni mfanyibiashara wa Mtwara na mingine mingi.

Matatizo haya yanatosha kumfanya mfanyikazi yeyote mwenye kuwajibika kuona umuhimu wa kuachia ngazi . Kama yeye haoni umuhu basi aliyemteua aone kuwa huyu mtu ameshindwa kazi na anachofanya ni kumchafua mteuzi wake aonekane anamuunga mkono kwenye masuala yote haya.
 
Nimeona kwa nyakati tofauti huyo IGP Simon Nyakoro Sirro akiongea na wananchi, yupo defensive, amejaa dharau kwa viongozi wake. Kwa mfano akiwa huko mkoani Tanga amesema Police hawapo responsible kwa vifo vingine ila kwa wale wahusika wa moja kwa moja KAMA WALE WALIOMUUA MFANYABIASHARA HUKO MTWARA.
Je ina maana huyo Sirro hajui pia kazi ya police ni kuwa na intelligensia ya kuzuia vitendo viovu? Mbona wakati wa kuzuia mikutano ya CHADEMA wanakuwa tayari wana intelligensia yao? Vipi mbona watu wengi wanaendelea kupotea mikononi mwa police lakini yeye yupo kimya????
IGP Simon Nyakoro Sirro ameshindwa kazi, viatu hivyo ni vikubwa sana kwake, hawezi na hana uwezo wa kuongoza jeshi la polisi! Huyo Masauni pia ni dhaifu kwa Sirro ni kama anamuogopa.
Kuna kipindi alikuzogoa mheshimiwa rais, alikukashifu akisema kwa mafumbo kuwa kila lawama wanatumiwa polisi wakati wao pia wanaumizwa. Ni wakati ule ulivyowaambia polisi wasitumie nguvu za kupita kiasi.
Mheshimiwa rais, mfukuze Sirro, aondoke na hiyo pensheni yake wala hastahili huyo mwizi mkubwa.
 
Habari zenu wakuu.

Kwa hali ya kiusalama ilivo sasa sioni haja ya huyu ndugu yangu Sirro kubakia ofisini...hana maarifa wala ufanisi mwingine wa kutuvusha katika hali ya sasa.

Hali imekuwa mbaya sana, kwa sisi ambao tuna vibiashara vyetu huku mtaani tunaishi kwa wasiwasi sana. Majambazi na vibaka ni kama wako huru sasa kufanya chochote wanachotaka kwa mda wowote.

Matukio ya mauaji yameshakuwa kawaida masikioni mwa wengi sasa..na hakuna jitihada zozote za kukomesha ndio kwanza yanaongezeka.,

Kwa sasa ni vigumu kutofautisha kati ya kibaka, Jambazi na Afisa wa jeshi la polisi, wote wana lengo moja na ukicheza wanakuua.

Sirro umekabidhiwa Ua - GP kutulinda Ila kwa sasa ni kama una bet na maisha yetu. Ni bora uondoke tu uendelee kula keki ya Taifa ukiwa kwako kuliko kuchezea usalama wa maisha ya watanzania
 
Huku mkoani kwetu hali ni shwari tu,lawama zipelekeni kwa RPC wenu Simon Sirro ni wa kitaifa.
 
IGP Sirro alipata hicho cheo kama mkombozi wa jeshi la polisi.

Tunayakumbuka mapambano yake misituni na wahalifu toka Rwanda na Burundi, huko mapori karibu na mpakani. Wakati huo akiwa kamanda wa Fiekd Force Unit, FFU.

Sasa baada ya kuwa IGP, kuna matukio mengi ya kutofuata sheria za uendeshaji jeshi la polisi, GPO, yameibuliwa. Na jua likapatwa wakati wa uongozi wa Awamu ya 5.

Askari polisi wamekuwa wakiteka, kuua, na hata kufanya matukio ya kijambazi kwa kupewa kiburi na wanasiasa.

Sasa idara za uchunguzi za polisi zina underperform, askari inaelekea kupora imekuwa tabia, na kuna hisia wameanza kuuana kuficha ushahidi.

Mbaya zaidi imani ya wananchi kwa polisi inaendelea kushuka, hata Makamu w Rais Dr Mpango wameshaonyesha kukerwa na hali hii.

Hili limeanza kuwa jeshi la mamluki. Serikali ilifikirie sana suala la kulijenga upya jeshi hili.

Lakini Sirro yeye astaafu tu haraka, kwa heshima, kabla halijatokea tukio jingine baya.

=======

Huu ni mmojawapo kati ya mijadala inayomtaka IGP Sirro aidha kuwajibika au awajibishwe. Mingine hii hapa 👇🏾

1) IGP Sirro ama astaafu au afukuzwe kazi

2) Kwa haya yanayolikumba Taifa letu, ilitakiwa Rais Samia amfute kazi IGP Sirro

3) IGP Sirro jiuzulu ulinde heshima yako

4) IGP Simon Sirro unasubiri nini kujiuzulu kwa kashfa hizi za Jeshi la Polisi?
anasubiri afukuzwe sio ajifukuzishe kwani unadhani yeyeZIRO haijui NJAA?
1643801498375.png
 
Wenzetu Kenya nafasi kama hiyo ya IGP inatangazwa kwa uwazi wenye Sifa wanaomba,

Kunakuwa na usaili wa uwazi hadi anapatikana
Mtu mahili wa kufaa kutimiza majukumu kwa manufaa ya wananchi.

Lakini huku bado mambo yanafanyika kienyeji enyeji kwa kujuana tu kujikomba kama sio kujipendekeza.
 
IGP Sirro alipata hicho cheo kama mkombozi wa jeshi la polisi.

Tunayakumbuka mapambano yake misituni na wahalifu toka Rwanda na Burundi, huko mapori karibu na mpakani. Wakati huo akiwa kamanda wa Fiekd Force Unit, FFU.

Sasa baada ya kuwa IGP, kuna matukio mengi ya kutofuata sheria za uendeshaji jeshi la polisi, GPO, yameibuliwa. Na jua likapatwa wakati wa uongozi wa Awamu ya 5.

Askari polisi wamekuwa wakiteka, kuua, na hata kufanya matukio ya kijambazi kwa kupewa kiburi na wanasiasa.

Sasa idara za uchunguzi za polisi zina underperform, askari inaelekea kupora imekuwa tabia, na kuna hisia wameanza kuuana kuficha ushahidi.

Mbaya zaidi imani ya wananchi kwa polisi inaendelea kushuka, hata Makamu w Rais Dr Mpango wameshaonyesha kukerwa na hali hii.

Hili limeanza kuwa jeshi la mamluki. Serikali ilifikirie sana suala la kulijenga upya jeshi hili.

Lakini Sirro yeye astaafu tu haraka, kwa heshima, kabla halijatokea tukio jingine baya.

=======

Huu ni mmojawapo kati ya mijadala inayomtaka IGP Sirro aidha kuwajibika au awajibishwe. Mingine hii hapa 👇🏾

1) IGP Sirro ama astaafu au afukuzwe kazi

2) Kwa haya yanayolikumba Taifa letu, ilitakiwa Rais Samia amfute kazi IGP Sirro

3) IGP Sirro jiuzulu ulinde heshima yako

4) IGP Simon Sirro unasubiri nini kujiuzulu kwa kashfa hizi za Jeshi la Polisi?
 
Polisi walibebwa såna na Mwendazake, utaona wanakiburi kabisa na waliweza kuficha lolote.Wakajiona nao ni Jeshi
 
Kwa uozo uliopo ndani ya chombo unachokisimamia Kama mkuu wake huoni kuwa huenda umechoka na kuishiwa mbinu kiasi kwamba imekuwa fedheha kwako Kama kiongozi jitathimini hata ukisimama mbele ya Mh Rais uone aibu jeshi limepoteza WELEDI kwa kasi sana Tangu IGP MAHITA alipokuwepo na wewe ndio umelipeleka porini kabisaa chukua KALAMU NA KARATASI UMSHUKURU MH RAIS ILI MTAANI UHESHIMIWE MUDA NI MWALIMU MZURI UTAKUUMBUA JIUZULU ASANTE
 
Hahaaa!!njaa babaaa, ki ukweli kwa sasa jeshi la polisi limerudi enzi zile za mahita!!Said mwema alijitahidi sana kulirudisha kwenye mstari na akafanikiwa kabisa!!sasa huyu yeye ana amini ktk nguvu na vitisho tu, na sio kwenye weredi!!ila mama kwa kutoa maagizo ya kuundwa kamati ya uchunguzi, na ripoti yake ikafanyiwa kazi inaweza leta mabadiriko, chanzo ni awamu ya 5, kwani jiwe naye aliamini zaidi kwenye utumiaji nguvu na vitisho!!Kama vipi huyo kamishina mpya (Awadhi)wa jeshi la polisi zanzibar apewe u IGP, tu, kwani umakini wake unajulikana sana, wakati akiwa dar, waulize madreva wa daldala habari zake wanazo!!Siro kwa sasa mbinu zimemuishia kabisa, japo huko nyuma alionekana mtu makini sana, kabla hajawa igp!!
 
Back
Top Bottom