Yaani huyo jamaa alipokuwa kitengo cha trafiki dar, aliogopwa mno!!kwani yeye hataki maneno,kama umefanya kosa, kwanza unatiwa ndani, na faini juu, au mahakamani!!na hata polisi wa chini walikuwa wakimuogopa sana!!
Exactly, Mimi nakumbuka mwaka 2004 aling'oa plate number za daladala yangu kosta, kisa dereva sijui alitanua, alikuwa na dada mmoja anaitwa Fatuma,jamaa anapiga kazi haswaa
 
Kinachoshangaza zaidi ni kuwa aliyemteua haoni aibu hii. Sirro anajiaibisha mwenyewe, anamwaibisha aliemteua na analiaibisha taifa. Yanayotokea kwenye kesi ya Mbowe intatia kinyaa. JIUZURU LIEPUSHE TAIFA NA AIBU HII HATA KAMA ALIEKUTEUA HAIONI.
 
Naunga mkono ni wakati muafaka sasa kwa IGP kutokea Zanzibar.
 
Sio busara lakini Acha ibaki hivyo hivyo!
 
Hakutakiwa kuwepo kwenye hiyo nafasi tangu mwanzoni mwa mwaka huu
 
Alipaswa aandike barua ya kujiuzulu muda mrefu sana, kuanzia 2017 matukio ya watu kuokotwa kwenye viroba ufukweni na kwenye mito. Askari polisi walivogeuka kuwa TRA kukusanya mapato kwa madereva barabarani na walivokua wakionea madereva barabarani na fine za ajabu.

IGP yupo kwaajili ya kuongozaa ulinzi wa raia na mali zao, ila cha ajaabu nchi hii ni kinyume, yupo kwaajili ya kutetea maovu ya askari wanaofanyia raia.
 
Ikifika next week hajajiuzulu wala kutumbuliwa ...nitabaki na maswali na mshangao wangu moyoni
 
madaraka matu acheni nyie.Mama mwenyewe aliposikia 2025 hato pita alikuwa mkali kama pilipili
 
Kutokuona aibu kwa waswahili mbona kawaida kwa mengi tu

Huyu nae wale wale aone aibu wapi
Yaani mswahili anakuibia unamfukuza kama mbwa halafu baada ya mda anakuja kujikomba na kukusalimia na kukuomba tena hela hata kazi

Hao ndio waswahili bwana
 
Tena Kaza hivyohivyo wala haina haja ya kujiuzuri kuna orodha lakini hatutakubali. Kumbukeni nguvu ya umaa ni nguvu ya Mungu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…