IGP Sirro: Tunakichunguza Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu baada ya kupokea fedha nyingi takriban Tsh. bilioni 6 kutoka nje

IGP Sirro: Tunakichunguza Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu baada ya kupokea fedha nyingi takriban Tsh. bilioni 6 kutoka nje

Wanaogopa zitatumika kumsaidia kijana mtukutu kufanya kampeni kuna muda nawaza nimezaliwa Tz bahati mbaya au makusudi ila najikuta naichukia tu nchi yangu kwa ujinga mwingi badala ku focus na mambo ya msingi na yenye mantiki siasa tu mda wote
 
Kuna watu humu wanatetea utafikiri wao ndo wanaijua nchi kushinda serikali yenyewe! mbona hilo ni utaratibu yakinifu au mlitaka waachiwe tu kwa kuwa Kuna huu msamiati "watetezi wa haki za binadamu!!"

Serikali hebu kagueni hizo mutu mpk mjiridhishe hakuna cha kuangalia usoni hapa,hayo matetezi kwanza yanavunjaga na mipaka yanatetea mpk ndoa za kinyume na jinsia!
Mkuu si unajua mahaba ya kisiasa, hii nchi wanaume wapo kazini. Hata nami nafarijika sana kwa juhudi zozote zinazochukuliwa na serikali hasa kwa kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
 
Sometime transfers kama hizi hutumika katika utakatishaji pesa na kufund vikundi vya kigaidi.

Siyo jambo baya kuchunguza ila tu kwa nchi yetu ilipofikia itaonekana kama vile kuna rafu inataka kuchezwa.
Kulikuwa kuna haja gani ya kufunga account zao?Yaani unasimamisha shughuli za taasis kwa hisia tu kwamba unataka kujiridhisha na uhalali wa fedha wanazopata na malengo ya fedha hizo!Kipi kilipaswa kutangulia?Uchunguzi au kufunga account zao na kitutangazia?shame
 
Usalama wa Nchi yako kwanza.Siasa Kwenye sanduku la kura, mungu ibariki Tanzania,mungu mbariki Magufuli,Mungu mbariki Membe,Mungu mbariki Lissu.
 
Kulikuwa kuna haja gani ya kufunga account zao?Yaani unasimamisha shughuli za taasis kwa hisia tu kwamba unataka kujiridhisha na uhalali wa fedha wanazopata na malengo ya fedha hizo!Kipi kilipaswa kutangulia?Uchunguzi au kufunga account zao na kitutangazia?shame
Mkuu huenda wana taarifa za uhakika kabisa, sema hizo ni lugha za kiintelijensia na kulinda diplomasia.
Si unajua taifa/serikali sio polisi peke yao.
 
Hivi kwa taasisi kama ile Billioni 6 ni nyingi sana eeeh?
 
Kulikuwa kuna haja gani ya kufunga account zao?Yaani unasimamisha shughuli za taasis kwa hisia tu kwamba unataka kujiridhisha na uhalali wa fedha wanazopata na malengo ya fedha hizo!Kipi kilipaswa kutangulia?Uchunguzi au kufunga account zao na kitutangazia?shame
Process huhusisha akaunti kufungwa
 
Kwahiyo anataka watu wakionewa kituo kisiweze kuwatetea kwa kukosa pesa. Kama ukiukaji wa haki za binadamu unaongezeka alitegemea gharama za kuwatetea zisiongezeke pia wapunguze unyanyasaji wa raia na matumizi ya hicho kituo yatapumgua automatically.
 
Back
Top Bottom