Ijue Historia ya Firauni na uongo aliozushiwa

We jamaa kwa viroja hujambo!!! Mbona unazidi kumbwela mbwela tu hapa! Nimekuuliza hapa taja hapa hayo maendeleo unayosema!!! Mbona swali rahisi sana..... Au ndo huo ufuaji wa chuma kwa kujianika kwenye moto ili hatimae upate kitu cha kuchimbia wakati wengine walikuwa wameshapita hapo na walishafika kwenye kutumia chuma kwenye maendeleo ya viwanda!!!
 
Nilipenda na kukubaliana kwa kiasi kikubwa na maelezo yako umenifukuza mbali kabisa na wewe kwenye eneo la Waafrika hamna cha kujivunia.Tuna vingi vya kujivunia tangu kale hata sasa.
Sasa kama tuna cha kujivunia; shida yote ya nini ya kujinasibisha na watu ambao hata asili yao hatuijui!! Na mimi ningependa sana tuwe na cha kujivunia lakini inaonekana hatuna na ndio maana tumekuwa ni watu wa kujiegemeza egemeza tu!!!!
 
kwa hiyo herode alikuwa Muzungu??? na alikuwa katika nchi ipi maana kuna siku nimesoma kuwa hiyo israel na misri walikuwa wanaishi watu weusi
Ni kweli kuwa waizrael/wayahudi ni weusi na wametapakaa dunia nzima, hao wazungu mnao waona Israel ni wahamiaji tu
 
Sasa kama tuna cha kujivunia; shida yote ya nini ya kujinasibisha na watu ambao hata asili yao hatuijui!!!

Kujinasabisha na wengine ni upuuzi ila kwamba hatuna cha kujivunia kwa maoni yangu ni upuuzi Zaidi.Nina lundo la maelezo ya maeneo tuliyofanya vizuri kuliko binadamu mwingine yeyote toka kale hata sasa.

Kipindi hicho mnachojadiliana kuhusu filauni uhuni ulikuwa mkubwa huko wengine wanakoona kuna waungwana.Arabuni,Babeli,Rumi na Israeli ya wakati huo kimbilio salama la walionewa lilikuwa Misri.Misri ipo Afrika.

Maandishi ya kwanza ya binadamu yalianzia Misri.Watalii waliomua kwenda wanapotaka kwa gharama zao kushuhudia wanayosimuliwa walikuwa waafrika,rejea ziara ya malkia wa Kushi kumtembelea mfalme wa Israel aliyeitwa Suleiman mwana wa Daudi.

Njaa ilipoikabili Israel kimbilio lao lilikuwa Misri.Misri ni Afrika.

Rejea simulizi za Walter Rodney" How Europe underdeveloped Africa",usiishie tu kusoma habari zake fuatilia sababu/kiini cha kifo chake utajua kiwango cha uwezo wa akili zetu.Huko mbali fuatilia Patrice Lumumba na nmna alivyomalizwa kikatili utajua uwezo wetu wa akili ukoje.Shida ni mamluki na kundi dogo wanaotamani kuwa watumwa milele.

Afrika hatujapungukiwa uwezo wa akili wala raslimali,tumebweteka kwa utajiri uliokithiri( najua unafuata ubishi na matusi mengi),nitatoa kielelezo.Mwajiriwa anayelipwa Tsh.1000,000/=( take home) na mfugaji wa kimasai au kisukuma mwenye ng'ombe 50 anaozurula nao mchna na usiku,jua lake na mvua yake ukikutana nao njiani utamwona nani tajiri aliyefanikiwa? wengi watamwona mopkea 1,000,000/= Kila mwezi tajiri kwa kungalia anavyokula, anavyo vaa, simu aliyo nayo, kagari kamkopo nk.Mfugaji mwenye mgolole ataonekana omba omba. Sitisha ajira mwezi mmoja tu,utajua nani tajiri kati yao.

Ndiyo tofauti yetu na hao ambao miongoni mwao wanatamani kujinasabisha nao.Wana mbwe mbwe hawana kitu Zaidi yetu ila shida zimepanua matumizi ya akili zao.Nitabaki Mwafrika na kujivunia uafrika.

Kwa mada iliyo mezani awe Filauni au Farao maadam alikuwa mtawala wa Misri na kama ngozi yake nyeusi kama yangu huyo ni sehemu yangu,makosa yake ni makosa yetu kinachonitenganisha naye ni maungamo yangu kwenye makosa aliyoyatenda.Damu ya thamani kubwa ilinitenganisha na kila uovu.

Baraka za Ibrahimu zitaambatana name kwa kuwa nilishiriki kuwatunza watumishi wa MUNGU waliofukuzwa na kukataliwa na wakwake.

Ninajua kuwa historia ya kweli Misri ni ya waafrika halisi weusi kama tulivyo.
 
Kuna kitu unakikosea hapa, hoja ya msingi ni utumwa wa kifikra juu ya weusi wetu kutokuweza lolote bila ya weupe. Ndo maana wajuvi wanakwambia tujikomboe, tuuondoe huo utumwa.

Mwaka 1600,ulaya walikuwa na teknolojia ipi ambayo Afrika haikuwepo? Kama wanyama walitumika kwa usafiri vivyo hivyo kwa Afrika. Kama upepo ulitumika kwa usafiri na Afrika pia, kilimo ni kwa jembe la mkono kote, na mengine ni tofauti tu ya kimazingira. Au ulidhani walishakuwa na ndege, umeme magari nk?

Halafu kama unakuwa muwazi kidogo, hapa hatutumii historia ya darasani. Ni ya kimazingira na uhalisia zaidi hapa.

Na teknplojia si lazima mojakwamoja uibuni wewe, unaweza ukaiingiza toka kwa wengine na ndivyo ilivyotokea ulaya.

Afrika ilikutwa iko na mifumo yake ya kisayansi, kisheria, kisiasa,kitabibu na kijamii. Na hadi leo, inaonesha ilikuwa bora kuliko hii mifumo mipya tuloletewa. Kulikuwa na viwanda vyetu, vyenye teknolojia sawa na vya ulaya tofauti labda ni ukubwa tu.

Jinsi nguo ilivyotengenezwa ndivyo tulivyotengeneza sie. Uhunzi ulitumia teknolojia ileile ya kuwasha moto kwa upepo kama kwa wafipa tu.
 
We umeyataja yapi unayoyaita maendeleo ya huko ulaya yaliyo tuzidi huku Afrika kabla ya ujio wao huku, tuanzie hapo. Mi nilikuwa nakupa kanuni za maendeleo, nadhani kwako maendeleo ni vitu si watu.
 
Afrika ndo bara la kwanza kuwa na chuo kikuu ktk dunia hii. Na si Afrika ya waarabu bali weusi, na ni kabla ya muingiliano na weupe wa ulaya. Sijui hapa unasemaje.
 
Chuma kwenye maendeleo ya viwanda? Vilikuwaje hivyo viwanda, havikutumia kuni na makaa kama vile vya wafipa au?
 
Kwani RED INDIANS WA NORTH AMERICA WAKO WAPI? na AUSTRALIA wale watu wa asili wako wapi? MZUNGU NENDA NAE KWA HEKIMA NA BUSARA PAMOJA NA UFAHAMU WA HALI YA JUU. ..
Kidogo afute weusi south.mzungu co mtu kbisaa
 
naomba uniambie u-genius wa wayahudi ni upi??
 
Mkuu kumbuka duniaani kuna matukio mengi kutokana na Muda hivyo si vibaya watu kusoma na kutafuta ukweli juu ya historia husika pia kumbuka kuna vitu vingi duniani vinaficha wa malengo fulani hivyo si vibaya kutafuta ukweli wake.Na ni rahisi pia ni vigumu kujua ukweli,lakini unaweza ukajiuliza kwa nini kitu/historia iliyo sahihi iwe na contridiction ndani yake?? kwa nini kisiwe 100% sure ndipo hapo watu huanza kujifunza zaidi-kwa hiyo lengo sio kujifannanisha na hao mafarao
 
Duh wapi kasema yeye ni mwarabu? Je kuwa mwarabu ni dhambi? Acha ubaguzi haufai
aliyeumba watu akawapa utofauti wa rangi amisha halalisha ubaguzi,hivyo ubaguzi upo na utaendelea kuwepo mpaka mwisho wa dunia
 
 
 
 
Leo tutakuokoa. Kiwiliwili chako baada ya kufa ili uwe ni ukumbusho kwa watu wajao mbele,
Inasemekana alikufa ktk gharika baada ya kukufuru kwa kujiita yeye ni Mungu mkuu
Fuatilia au tafuta filaamu moja inaitwa THE MOSES inaelezea kisa chote ambacho wame act wamisri ,wao wanaijua historia kuliko wewe mnyamwezi wa Tabora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…