Ijue sababu ya marafiki wa DSM kuwakimbia na kuanzisha visingizio pale inapofika mda wa kupokea washkaji zao wa mikoani

Eti mtwara 😅😅😅😅
 
Kiukweli uliyosema yana ukweli kwa asilimia kadhaa na yamewatokea baadhi na taarifa ziko nyingi humu JF.
Binafsi niseme kila mtu na utashi wake na pengine hayo yanawakuta wenye kujikweza katika maisha yao. Kama si mtu wa kujikweza hata kama una chumba kimoja huwezi kukimbia washikaji au ndugu kisa maisha ya kufeki. Binafsi mbali na kukaa kwenye chumba kimoja, nimekaa na wamepita washikaji kibao zaidi ya ndugu na wengine ajira wamepatia kwangu, tena wakiwa dhohofu huko walikotoka na hadi leo baadhi walivyoondoka baada ya kufanikiwa ndio hata salamu ikapotea baada ya siku chache tu za kupata neema. Hivyo kwa namna hiyo unaweza kuwa na nguvu ya kumsaidia mwingine na siyo kwamba ulimtegemea Lah!
Kiufupi tabia ya mtu ndio inahakisi matendo na mambo yake lakini pia washikaji hao hao ndio wakwanza kukuponda wanapofanikiwa.kupanga ni kuchagua, mwishowe tuishi kama wachaga tu.
 
Kiufupi ulimsaidia mtu usitarajie malipo ya fadhila,tenda wema nenda zako.lakini pia kuna mtu anaweza kusafiri toka Mwanza kufika Morogoro ndio ana kwambia umpokee yuko safarini kuja kwako bila taarifa yoyote ya awali,hapo unategemea mwana DSM afanyeje? Anaweza kusema ukweli au Lah! Yupo Dar au hayupo.maisha mtihani.
 
Chumba kimoja,kina kila kitu ndani kama store ya kimaro,usiku joto kama tunachomwa mishikaki,nimezoea asubuhi na kunywa juice yangu ya 500 ya maembe na chapati 2 je yeye ataweza maisha hayo? Mchana makande ya 500,jioni chapati 2 na maharage hapo hata 5000 sijamaliza,asinichoshe bana akalale guest
 
 
Mnaongeaga hivi baada ya kupata,lakini ukute mpaka kufikia hapo kuna watu wamekusaidi pakubwa,na usizani labda umemaliza mwendo bado sana ndugu yangu,labda wewe au wanao nao watakuja itaji tena msaada
Ningekua naongea baada ya kupata basi nidingemkaribisha hata nyumbani kwangu kuishi.
Mim mwenyewe nikienda kweny nyumba za watu lazima niwe na adabu.
 

Kweli kabisa
 
Ila ki ukweli Wana wa mikoani Huwa mna bifu na Wana wa dar sijuwi Kwa nini yaan.Kama vile T.I.D na watoto wadogo.
 
Nyie mkija mkoani(Kwny seminar,'michongo' etc) hua mnakua hamjajipanga kifedha sio?Maana hua hamfikii lodge mnafikia kwa ndg zenu.
Mtu mzima ukiwa na safari iwe mkoani au popote pale hakikisha umejipanga.

Sio unafika sehemu unaanza kusumbua watu
 
Mi napenda mgen anaekuja kisha anaingia jikon ajipikie ,sio nianze kumpikia sijui nihangaike nin huwa nachoka sana mtu anakuja hta kuosha vyombo hakuna anataka kila kitu umfanyie sipendii,wagen wengi wasumbufu mno wachache wastaarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…