Ijue sababu ya marafiki wa DSM kuwakimbia na kuanzisha visingizio pale inapofika mda wa kupokea washkaji zao wa mikoani

Ijue sababu ya marafiki wa DSM kuwakimbia na kuanzisha visingizio pale inapofika mda wa kupokea washkaji zao wa mikoani

Mim nmekaa na mtu hanisaidii chchte ndani hata kufua nguoz ake hawezi alikua analala sebuleni me naondoka namuacha anaamka sa tano. Bills ni kubwa kinyama maji nilipe 25 umeme elf 15.
Muda huo bado nikipika nyama kg moja nyingine nikiweka kweny kafrije kangu nakuta imedokolewa muda mwingine nampakulia mtoto chakula nakuta ety anaonja tena kwa mikono yake imekaa kama spanner.

Mungu anisamehe nlimtimua tu maan alinichosha kabisa nikinunua ety li jitu linakunywa maziwa ya mtoto ety anasema anapenda sana maziwa ya baridi

Ndugu zangu usikaribishe watu ni bora wakae huko huko kwa ndugu zao sijui wapi mim nmejifunza kabisa. Sitak aiseh.
Mim sa hiv sikwepeshi kabisa Bora nikae nadg angu akikosea namuelekeza basi maishae mengine yanasonga.

Mtu ukienda kwa mtu unatakiwa hata siku nyingine unanunua mkate ,unapenda mayai nunua,changia chochote au unapenda maziwa nunua watz wanapenda vya bure na unakuta mtu umeenda kumtembelea mtu hana kazi au anajitafutia na humchangii chochote ni kuongeza mzigo
 
Baba zima linalala kwenye kochi sebuleni, eti nipo dar mjini bwana basi tu
 
Mnaongeaga hivi baada ya kupata,lakini ukute mpaka kufikia hapo kuna watu wamekusaidi pakubwa,na usizani labda umemaliza mwendo bado sana ndugu yangu,labda wewe au wanao nao watakuja itaji tena msaada
Usiendekeze upumbavu.

Nchi ishaachana na mfumo wa kijamaa
 
Mtu ukienda kwa mtu unatakiwa hata siku nyingine unanunua mkate ,unapenda mayai nunua,changia chochote au unapenda maziwa nunua watz wanapenda vya bure na unakuta mtu umeenda kumtembelea mtu hana kazi au anajitafutia na humchangii chochote ni kuongeza mzigo
Acha alaf kibaya zaid hadi maziwa ya mtoto anakunywa khekhekhe khaaa. Mungu atunusuru
 
Sasa mimi imenikuta ila wa mkoani alinikimbia. Iko hivi

Mwaka 2012 mwishoni alikuja jamaa yangu tuliesoma nae chuo kimoja mpaka kumaliza . Yule mwamba kwa madai yake alisema kaja kufuata mzigo kkoo kipindi hicho mimi nilikua muajiriwa ofisi fulani, basi mwamba alifika mpaka kigamboni akakaa kwangu nikampa huduma zote anazopewa mgeni mpaka demu wa kumpooza nikampa. Mwamba alifurahi sana ila cha ajabu alikaa kama mwezi hivi mwanzo alikua ananiambia tutoke wote uniache kkoo nikacheki mzigo na mm sikuuliza namuacha nasepa jioni namkuta ferry tunasepa home.

Baada ya mwezi nikamuuliza vipi mzigo kwa kutojiamini akanijibu nishautuma mkoani, ah basi nikamshauri arudi sasa maana sikuona nn anafanya na ananiwekea usiku tu siwi huru kufanya mambo yangu.

Mwamba akasepa tukawa tunawasiliana vizur tu.
Mwaka 2014 nikapata safari ya kwenda wilayani kwake nikamcheki kwa furaha akanikaribisha sana uzuri hiyo wilaya sio mgeni basi nikafika nikachukua chumba kwaku sikutaka kupeleka dem hapo kwake, mida ya jioni kumcheki hakupokea nikamtxt kaka nimefika wilayani hapa alafu nikapiga kimya ebhana sikujibiwa mpka siku ya tano ambapo siku tatu mbele ndio naondoka. Jamaa kanipigia skuhiyo anauliza vipi kaka kwema asee mambo yaliingiliana uko wapi? Nikamjibu nishasepa kaka japo sijakuona jamaa akaanza kujitapa dah umeondoka hata kusema kaka japo nilikua busy na mambo ya hapa na pale ila next time ukija nicheki kaka, nikamjibu poa.

Sasa nikasema nipite mitaa yake nikakuta bar moja kubwa nikazama nikawa nakula msosi pale jioni mara paaaap jamaa huyu hapa akabaki anacheka cheka na kuona aibu nikamualika hakuweza kukaa sana akasepa siku naondoka kumpigia hapokei na mpka leo siwasiliani nae naona miyeyusho tu.
 
Nzuri sana hii, mkumbushane kwa kweli, wasiwe wanakuja huko wanawapiga fix mpaka mkamaliza fedha zenu za akiba , ukijua ukija Dar siku moja mwana atakuhifadhi.Wenzenu huku wanaishi maisha ambayo sio, wanaona aibu kuwaambia ndugu zenu wanaosoma ili wasikate tamaa ya shule.Msitiriane kama Ndugu tu, yanapita tu.
 
Acha alaf kibaya zaid hadi maziwa ya mtoto anakunywa khekhekhe khaaa. Mungu atunusuru
Mbona mkija Mwanza mnataka samaki kila siku. Na mnalala miguu juu ila nyie mkitembelewa huko kwenu matesoni (DSM ) Mnakwepa ! Poleni sana
 
Jambo hili lipo hata kwa wafanyakazi..yaani wafanyakazi wa Dar wakija mikoani unawatafutia sehemu ya kulala japo atalipa mwenyewe..utakuwa nae kwenye mizunguko baada ya kazi nk.
Nenda wewe Dar..mtakutana kwenye kikao/mkutano na baada ya hapo kila mtu kivyake vyake.
 
Huwajui wanadamu kwa kuroga🤣 anakuja kwako anakukuta una kochi mbili na ka tv ka inch 32 anakuona una maisha unaringa. Anataka na yeye awe kama wewe, anapiga simu kwao anasema yani flani tumesoma nae ila saizi maisha yake mazuri anatembelea gari. Wa kwao wanamwambia usijali tutamuweka sawa huyo🤣

Aah hapana kama ndugu tu anaweza kukufanyia hivyo sembuse rafiki. Michongo ntakupa ila kwangu sina pa kukulaza sio kwa ubaya ila tunapunguza risk
 
Jambo hili lipo hata kwa wafanyakazi..yaani wafanyakazi wa Dar wakija mikoani unawatafutia sehemu ya kulala japo atalipa mwenyewe..utakuwa nae kwenye mizunguko baada ya kazi nk.
Nenda wewe Dar..mtakutana kwenye kikao/mkutano na baada ya hapo kila mtu kivyake vyake.
Na hicho ndicho hasa nlichokuwa namaanisha..huo ukweli kabsaaa ila wengi wemejadili mambo ya vyakula hii inaonyesha hali ya maisha dhoofu bin taaban kwa wa Watanzania..
 
Na hicho ndicho hasa nlichokuwa namaanisha..huo ukweli kabsaaa ila wengi wemejadili mambo ya vyakula hii inaonyesha hali ya maisha dhoofu bin taaban kwa wa Watanzania..
Kweli kabisa...suala siyo chakula bali ni ile hali ya kuonyesha kujali..yaani haina uwiano mzuri.
 
Mbona mkija Mwanza mnataka samaki kila siku. Na mnalala miguu juu ila nyie mkitembelewa huko kwenu matesoni (DSM ) Mnakwepa ! Poleni sana
Mim siishi DSM naish Mwanza na Sina roho mbaya hadi nishindwe kuish na mtu Ila usipofuata taratibu za nyumba yangu lazima nkuondoe.
 
Nilisolve hiyo ishu kibave ila jasho lilinitoka,unakuwaje Cab drivee kwenye jiji lile barabara zina lane 8 na ni mgeni haiwezekani
Ndio maana mwanzoni nilikuita mjinga mjinga now umethibitisha.

NY inaongozwa kwa mifumo unashindwa vipi kusurvive? Huyo boya aliyekutelekeza naye alikuona we mbwiga akaamua akuteme.

Haya hiyo Queens unayodai ulifikia ni Jamaica Avenue au?
 
Back
Top Bottom