Ikitokea ukapewa fursa ya kukutana na wewe mwenyewe wa miaka 10 nyuma. Je, utajishauri nini?

Ikitokea ukapewa fursa ya kukutana na wewe mwenyewe wa miaka 10 nyuma. Je, utajishauri nini?

Miaka 10 iloyopita hata chuo nilishamaliza, hakuna nlichokosea. Mi nlikosea kusoma Advance tu.
Sema ningejishauri kumuoa demu wangu wa utoto, huyu mwanamke alinipenda sana. Kiufupi mimi ndio nilimkataa, baada ya kumess up, mpaka leo bado anipenda ila ndio basi tena sitaweza kumuoa na sijutii.
 
Ningeanza kusoma Sana Vitabu na kukusanya nguvu za kiroho .

Nimegundua kutokusoma Vitabu ndo kulinifanya kuchelewa kujitambua maana nimekulia katika mikono migumu.

Nguvu za koroho kutokuwa na spiritual power imefanya kuchelewa kuwa na nguvu ya kuongoza mambo yangu mengi ya msingi.
 
Ningejiambia kijana punguza umalaya..
Miaka ingezidi hiyo 10, ikawa 15 hivi, ningejiambia Ugenious wako hauendani na utoro wako, ingia darasani utafanya vizuri maradufu. Matokeo yako ni mazuri ila unapaswa kuingia darasani na sio kwa kubagua vipindi.
Kisha nisingekubali kusoma A level baada ya O level ningeenda chuo moja kwa moja.
Nyie ambao hamuoni umuhimu wa Advance labda ni combinations za arts sidhani kuna mtu wa science asione umuhimu wa Advance
 
Tumia vizuri muda ulionao sasa hivi,fanya unachokipenda na kinachokufurahisha nafsi yako,
Yaliyopita yameshapita hayawezi kurudi tena,

Baada ya miaka 10 kupita kuanzia leo, utakuja tena kujiuliza swali hili hili,

Sometimes u will never know the value of a moment until it becomes a memory.
 
Ebu kwanza tupige calculation kidogo
2024-10 = 2014
Daaah 2014 hapa Najishauri nini aiseeeeeeee..
🤔 🤔 🤔 Kidogo ningekua nayajua mashangazi ila wapi....
 
Ningemfuata Halima nimwambie Sasa nimekuwa naomba uwe wangu daima .
Ujana ulinipotezea binti aliyenipenda kweli na Leo najua ndiye mwanamke wa ndoto zangu ila hawa wengine ni ngujiro tu
Note:Niliowahi kudate na nyie kutoka humu jamvini msijisikie vibaya .🙏
Hilo Jina hilo huwa ni la wanawake safi sana....
 
Habari za Jumatatu wanajamii.Pia hongereni kwa pirika za kutafuta pesa za mahitaji yako.

Ninajua mpaka kufika katika umri ulionao kuna makosa kadhaa ushafanya na pengine ukawa unajutia.

Hapa nina swali fikirishi...
Eti,kama ikatokea ukapewa fursa ya kurudi miaka 10 au 15 nyuma na kukutana na wewe mwenyewe wa miaka hiyo kumi nyuma na ujipe ushauri, Je,utajishauri nini....?

Kwangu binafsi ,ningejishauri...
  • Kuangaika kupata fursa na kujitutumia katika kuzitekeleza hata kama zitafeli.
  • Kuondoa uoga kabisa katika kuanza maisha.
  • Fursa haziishii Dar,nitoke na kwenda mikoani na hata ikitokea nje ya Tanzania.
  • Kuwa karibu na watu wenye kuwaza maendeleo.
Kuacha pombe na uzinifu.....
 
Back
Top Bottom