Ikitokea ukapewa fursa ya kukutana na wewe mwenyewe wa miaka 10 nyuma. Je, utajishauri nini?

Ikitokea ukapewa fursa ya kukutana na wewe mwenyewe wa miaka 10 nyuma. Je, utajishauri nini?

Advance education ningeiruka haraka sana. Hata ukiangalia nyakati hizi za sasa wahitimu wengi hawana mwelekeo pamoja na kuwa na miaka miiiingi ya kukaa darasani. Tuliowaacha darasani LA saba ndio majasiri wa maisha HATA KUOA HAWAOGOPI ILA SIO KIJANA WA CHUO KIKUU.
 
Hilo Jina hilo huwa ni la wanawake safi sana....
Haukosei huyo mdada alinipenda sana tena sana Ila Sasa masikini yangu Mimi basi nilikuwa naambilika ni kujiona Mimi ndiye aluwatani kalipokuja kusema imetosha nililia mpaka kamasi Sasa ameolewa na wanapendana na kijamaa chake Kina kipara Kama Gamondi🙊😃
 
Haukosei huyo mdada alinipenda sana tena sana Ila Sasa masikini yangu Mimi basi nilikuwa naambilika ni kujiona Mimi ndiye aluwatani kalipokuja kusema imetosha nililia mpaka kamasi Sasa ameolewa na wanapendana na kijamaa chake Kina kipara Kama Gamondi🙊😃
Umenikumbusha mbali mno, dah....😭😭😭😭
Halima wangu mie....dah.
Ila mi sikujimwambafai....
 
Umenikumbusha mbali mno, dah....😭😭😭😭
Halima wangu mie....dah.
Ila mi sikujimwambafai....
Pole ndugu ,ukimpata dada wa kuitwa Halima akashoboka oa hata Kama ni mke wa pili hawanaga baya hawa .
Nimebembeleza sana Ila nimeishia kuambiwa nitashitakiwa kwa bwana ake kipara ngoto🙊
 
nimesoma PCM azania hapo, naongea nikijuacho, kijana akienda diploma DIT hapo si sawa na advance.

Binafsi nilisoma advance na ndio maana nikaona nisingeenda advance.
Advance anakuwa na analytical skills kubwa diploma anafanya vitu kwa mazoea hao ni watu wawili tofauti

Wewe chuo umesoma kozi gani? (be honesty)
 
Mimi binafsi, ningejishauri yafuatayo
1. Kusoma had chuo kikuu ni muhimu ila muhimu ni kuwa na hela kwanza.

2. Maisha ni kutafta cha kwangu sio kutegemea cha mtu


3. Ubahili kwenye suala la pesa ni siri ya kuwa na uhuru wa fedha


 
Habari za Jumatatu wanajamii.Pia hongereni kwa pirika za kutafuta pesa za mahitaji yako.

Ninajua mpaka kufika katika umri ulionao kuna makosa kadhaa ushafanya na pengine ukawa unajutia.

Hapa nina swali fikirishi...
Eti,kama ikatokea ukapewa fursa ya kurudi miaka 10 au 15 nyuma na kukutana na wewe mwenyewe wa miaka hiyo kumi nyuma na ujipe ushauri, Je,utajishauri nini....?

Kwangu binafsi ,ningejishauri...
  • Kuangaika kupata fursa na kujitutumia katika kuzitekeleza hata kama zitafeli.
  • Kuondoa uoga kabisa katika kuanza maisha.
  • Fursa haziishii Dar,nitoke na kwenda mikoani na hata ikitokea nje ya Tanzania.
  • Kuwa karibu na watu wenye kuwaza maendeleo.
Binafsi, ningejishauri;
1. Kutooa kabla ya kumaliza chuo.
2. Kuendelea na soka coz naamini ningefanikiwa.
3. Kuendelea na biashara licha ya changamoto zilizokuwa zikijitokeza.
 
Mambo kadhaa nimejifunza ambayo natamani ningeyafanyia kazi miaka 10 nyuma lakini kwa sasa nayafanyia kazi

1. Watu wengi wanaotuomba msaada ukweli nikwamba hawahitaji misaada yetu zaidi ya kutumia upendo wetu kama udhaifu nakisha kutamani kunyang'anya tulichonacho (Sio wote lakini wengi)

2. Kuishi huru na mawazo huru (kutokuwa guided with any book of law) zinazotupa restriction limit katika kufanya mambo mengi.
eg. Bila elimu huwez kutoboa
Bila kutoa zaka huwez toboa

3. Moja ya factor zakuwa brave ni pamoja na kutake risk maana nothing can substitute expirience.

4. Mafanikio ya mtu hayapo katika bidii sana bali katika nyakati na bahati na yamejificha katika tabia.
eg. Saving, frugality and taking risk and all are based on behavioral characters

5. Ningejenga hobie ya kusoma vitabu compared na hizi nyingine zilizozoeleka kwa ajili ya self help na financial matters.

6. Mwalimu pekee atakayekufundisha game ni Mr Game pekee. Hawa mentor sijui teacher n commentators tu.
Ndio maana unaambiwa expirience is a best teacher wengine wanatumia neno consistence. Hivyo ushindi upo katika uvumilivu, kujifunza na kutokata tamaa.

NB. Yote niliyoyaandika based on true story nayafanyia kazi kwa sasa na ninaona matokeo Chanya.

Regards
Miguel wa II
 
Back
Top Bottom