Ikiwa wewe ndiye Masikini zaidi kati ya ndugu zako, epuka mikusanyiko ya Kifamilia

Ikiwa wewe ndiye Masikini zaidi kati ya ndugu zako, epuka mikusanyiko ya Kifamilia

Na hawana muda wa kukuuliza unatumia kinywaji gan utashangaa tuu unatupiwa li mo energy uhangaike nalo na usijandanye useme hutumii utaambiwa unaleta fujo
Mo energy? Unapewa hii 😂
17-44-55-1617894480_fanta20black20current20bottle2030020ml.jpg
 
Ukiona familia inabaguana ujue tatizo ni wazazi. Watu wanafanya jinsi walivyokuzwa. Kama mzazi anaabudu pesa lazima shida itokee kwenye familia. Mimi nimezaliwa familia ya kawaida ila ninawashukuru sana wazazi wangu kwa kuhimiza watoto tupendane. Baba yangu ilikuwa kama wimbo kila siku kutuambia pendaneni. Huku ukubwani akisikia mtoto flani ana shida atapigia watoto wake wote tuelekeze nguvu kusaidia yule mwenye shida. Mimi kwa baba sitegemei kurithi mali yoyote ila kaniachia urithi mkubwa sana wa malezi bora.

Huko uchagani ile December huwa ni mwezi maalum wa kwenda kudharauliana. Kama huna hela utapewa sana kazi za kupasua kuni, usafi na shughuli nyingi za kitumwa. Hata kwenye vinywaji utapewa zaidi mbege. Fred Saganda kaeleza vizuri kwenye huu wimbo.
 
Attachments

No wonder mwanaume anawahi kufa! Maana hapa anasemwa mwanaume asiye na pesa, atasemwa na wanawake atasemwa na ndugu. Wanaume wenzangu tujikite kuukataa umasikini ikiwemo wanawake na ndugu maana wote Hao ukijinasibu nao hakika utakuwa masikini.
 
nakumbuka siku nilihuduria kikao cha msiba kanda ya kaskazini mimi kama mkwe wife kanitambulisha kwa mjomba wake kila dakika mjomba ananiuliza umekuja na gari gani
ikabidi tu nimpotezee wao wanadhani kila anayemwoa binti yao ni tajiri
Ndio maana wanakodi magari hao ,huku mjini kila njia inatumika wapate pesa...Wengi sasa hawaendi sio kama zamani ,mtu akijiona hana pesa akanyagi.

Kuna jamaa nilimkopesha akaenda kwao akanitapeli ..Acha tu.
 
Nachukia watu washamba na malimbukeni wanaotweza utu wa mtu kisa pesa
Ni jambo la kipuuzi sana na hufanywa na watu wasio na akili wala exposure na wengi wana insecurities zao nyingi sasa huwa wanaona kuficha hizo insecurities zao ni kutweza utu wa mtu
Na wengi ni hawa kajambanani unakuta ana vichenji vya kubadilisha mboga nae ana treat watu kama Jalala na kujiona multibillionaire , ni ukosefu wa akili
 
Ukikaa na wenzetu hasa hawa wazungu kuna kitu utajifunza ,
Watu weusi tuna matatizo sana
 
Back
Top Bottom