IKULU-DAR: Rais Samia Suluhu akutana na Mjumbe Maalumu wa Rais Uhuru Kenyatta. Rais Samia aalikwa rasmi kuzuru Kenya ili kukuza ushirikiano

IKULU-DAR: Rais Samia Suluhu akutana na Mjumbe Maalumu wa Rais Uhuru Kenyatta. Rais Samia aalikwa rasmi kuzuru Kenya ili kukuza ushirikiano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo 10 Aprili, 2021 amekutana na Dkt. Amina Mohammed, ambaye ni Waziri wa Michezo, Utamaduni na Urithi wa KenyaMjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta Ikulu Jijini Dar es Salaam.

View attachment 1748346

View attachment 1748347

View attachment 1748348 Take care mama! Isije kuwa ni wito Wa mabeberu via kenya! Ila Rais Kenyatta ni mtu mzuri! Ila wasimlazimishe mama kwenda huko akiwa amevaa barakoa!
 
I don't trust Uhuru Kenyatta, anatumiwa vibaya sana na nchi za Magharibi.Na siajabu huyo mjumbe kaleta ujumbe maalum kutoka kwa mabeberu.
Anitumie aje??? Mabeberu ndo kina Nani???

Kama mwendazake aliweza kuwabrainwash kwa fikra zake za miaka 1960 huko basi jueni kuwa nchi sasaivi iko mikononi mwa watu wenye akili na wanaojitambua na wanaojua dunia iko wapi na inaenda wapi?
 
I don't trust Uhuru Kenyatta, anatumiwa vibaya sana na nchi za Magharibi.Na siajabu huyo mjumbe kaleta ujumbe maalum kutoka kwa mabeberu.
Wasimshinikize kuvaa barakoa ni hilo tu! Atakuja kuvaa mwenyewe atakapoona ni vyema wala si kwa shinikizo na vitisho
 
Hamna kitu kama hicho.

Odhis *
You are too uninformed. So you believe there will never be a Global Goverment?So what is the United Nations and it's affiliated bodies for.The UN= The Global Government and it's affiliated bodies if you wish Ministries! Why this talk about globalization,global village etcetera. Can't you connect the dots?What is the World Economic Forum for,do you really folow it and see what it says about the One World Government? And how about the Bildeberg Group do you know what it is all about?Umelela sana mkuu,wake up.The talk about the Global Government is all over,and is being implanted right in front of our very eyes.
 
Hii vaccination ni shida huko ndugu zetu wa DRC wanalia, hebu msikilizeni huyu ndugu yetu.
Haifunguki mkuu,jaribu tena kuileta.

Ndio ni shida mkuu,ndio maana tunajaribu kutoa elimu,anayekubali kudungwa hiyo sindano akubali kwa ujinga wake,asije akasema sikujua.
 
Samia ameamua kurudisha makao makuu ya serikali Dar? Maana siku za karibuni shughuli nyingi za Ikulu zinafanyikia Dar badala ya Dom.
Nani akae sehemu haina upepo wa bahari?
 
Anitumie aje??? Mabeberu ndo kina Nani???

Kama mwendazake aliweza kuwabrainwash kwa fikra zake za miaka 1960 huko basi jueni kuwa nchi sasaivi iko mikononi mwa watu wenye akili na wanaojitambua na wanaojua dunia iko wapi na inaenda wapi?
Ila msitambe sana,kwa kuwa Taifa lina brake zake,na ninyi mafisadi msisahau kwamba Samia hajateuliwa na wananchi na Chama,kwa hivyo si chaguo la Watanzania.
 
Tunapenda sana kuboresha mahisiano ila yasiwe ya kinyonyaji...kwa miaka mingi wakenya wamekuwa wakiyuhujumu katika tasnia ya utalii hata madini.

Wao ndio wamekuwa wanasoko kubwa la uuzaji wa Tanzanite kinyemela mpka ilifikia hatua..mataifa ya nje yakajua Tanzanite.

Ila kipindi cha JPM walinyooka...Hawa watu ni majirani ila umakini unahitajika sana.

Hata kipindi cha Nyerere tumewahi kuwafungia mipaka...hawa ni ndumilakuwili.

Hata kufa kwa EAC ya kwanza...hawa ndio waliochota raslimali nyingi. Sijui sisi tunakwama wapi.

Tanzania kwa ajili ya Watanzania; Waafrika na Walimwengu wote watakaofata taratibu zetu.
Urafiki zetu na hawa wajamaa ni Urafiki wa mashaka. Ukizubaa umeliwa, tukizubaa tumeliwa.
 
Serikali itafanya shughuli zake ikulu ya magogoni hadi pale Ikulu ya Dodoma itakapokamilika kujengwa...

Hehehe awamu ya tano walikurupuka sana kupeleka serikali dodoma.
 
Na Mimi namualika nyumbani kwangu bagamoyo.aje afanye ziara
 
Anitumie aje??? Mabeberu ndo kina Nani???

Kama mwendazake aliweza kuwabrainwash kwa fikra zake za miaka 1960 huko basi jueni kuwa nchi sasaivi iko mikononi mwa watu wenye akili na wanaojitambua na wanaojua dunia iko wapi na inaenda wapi?
Kabisa mkuu sasa hivi nchi imeshatoka kwenye mikono ya ccm sasa ipo mikononi mwa chadema!
 
Safi sana, kawahi kabla ya hajaenda kwa Mu7.
Naona ndio maana yake.

Natumaini mama anauzoefu wa kutosha na kujua njia nzuri za kuhusika na nchi kama Kenya na viongozi wake. Vinginevyo, atafute washauri wazuri sana wa kumsaidia juu ya jambo hilo.
 
Mama aekekezwe kuvaa barakoa jamani asijiamini sana. Anakutana na watu kutoka makundi na maeneo mbali mbali. Hayuko salama kiasi anavyofikiri
 
sasa tunataka kuona Mahusiano mazuri, sio tu ya kutembeleana na kusalimiana lkn wananchi wanataka kuona wanafanya biashara zao bila kizuizi au kikwazo.

Tunaomba tuwe marafiki, majirani na ndugu wa kweli sio ulaghai, na Udugu wa kweli uta thibitishwa na matendo yetu sio maneno peke yake.

Tanzania na Kenya ni ndugu hakuna haja ya kutunishiana misuli.
 
Back
Top Bottom