IKULU: Rais Magufuli amteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

Juzi kanisani St. Peters alisema siku moja ina masaa 48.

Tena si kwa kukosea mara moja tu. Kapiga hesabu ndefu kwamba barakoa moja inavaliwa kwa masaa manne, siku moja ina masaa 48, kwa siku mtu anahitaji barakoa 12.

Sasa huyo mtu mzima kweli?
 
Kumbe ukiwa katibu mkuu wa ccm una qualify kuwa KMK, sidhani hata chuo kikuu amewahi kukamata wadhifa wa juu kwenye utawala, mfano vice-chancellor au deputy vice chancellor....naona uchama chama umehamia kwenye utumishi wa umma, watumishi jiandaeni kununua mashati ya kijani, au nasema uongo...
 
Nafasi yoyote ya chama cha kisiasa ni nafasi ya kisiasa by definition. Hata nafasi ya utendaji ndani ya chama ni nafasi ya utendaji katika muktadha wa kisiasa.

Maana yake, Katibu Mkuu wa Chama atakuwa mtendaji katika kueneza itikadi ya Chama, hivyo hiyo ni nafasi ya kisiasa.

Katibu Mkuu Kiongozi ni mtu anayeongoza watumishi wa umma ambao hawana open affiliation na chama chochote.Na yeye anaongoza kwa maadili ya utumishi wa umma yanayokataza ushabiki wa vyama.

Sasa Bashiru aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM aende kuongoza utumishi wa umma na kukataza ushabiki wa vyama?

Kumfanya Katibu Mkuu wa CCM kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ni kama kumfanya Kocha wa Yanga ajiuzulu ukocha wa Yanga, halafu aende kuwa refa katika mechi ya Simba na Yanga!
 
Hakuna lolote hapo Katibu Mkuu Kiongozi ni mwenyewe mteuzi Iwish i could be IGP
 
Upuuzi wote wa siasa za ujamaa uchwara, sasa rasmi Unahamia serekalini.
 
El Chapo ni muuza madawa ya kulevya.

El Chapo si Mtanzania. Ni raia wa Mexico..
You are missing the context with regards to El Chapo.

Nimekuuliza hivi, kwa kuwa hakuna mtu ambaye anakubalika na watu wote, basi ni sawa Rais amteue El Chapo, muuza madawa ya kulevya, raia wa Mexico, mfungwa aliye gerezani Marekani?

Nimemchagua El Chapo kama mfano to make a very specific point hapa.

Please do not miss the point.
 
We ulitaka ateuliwe nani?

..nadhani watu wanashangaa kwamba Raisi amekwenda kinyume na utamaduni wa kuteua ma-chief secretary.

..kilichotokea naweza kukifananisha na mtu is not an academic halafu ateuliwe kuwa VC ktk chuo kikuu.

..iliwahi kutokea huko nyuma lakini kwa muda mrefu ma-VC wamekuwa na watu waliolelewa kama wahadhiri ktk vyuo vikuu.
 
Kuna kipindi nilikuwa nafikiri Magufuli anaharibu mambo kwa ushamba tu, kwa ujinga, kwa kutojua, kwa ubishi, na kwa kutosikiliza watu...
Jiwe anataka kudistabilize system ili afanye lolote atakalo maana system itakua vulnerable.

Miiko na taratibu zinavunjwa makusudi hakuna wa kuhoji. Anateua watu wasio na taaluma husiki kushika nafasi nyeti ili awe na nguvu ya kuamua kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…