IKULU: Utiaji saini mkataba wa ujenzi wa Stiegler's Gorge

IKULU: Utiaji saini mkataba wa ujenzi wa Stiegler's Gorge

Kijana unajua maana ya stake?
Unajua vigezo vya kushinda zabuni?
Eti mradi umeuzwa, unatia huruma ujue!
Jaribu kuuliza maana ya stake ukishajua maana ya hilo neno utaelewa content nzima.
Wewe ndye hujui maana ya stake. Huu mradi tulitakiwa tuwe na 100% stake. Sasa Egypt kuchukua 55% maana yake who is the majority owner? Hapa Egypt ndye anafanya maamuzi yote. Yan hapa ni sawa na kuuza. Yan umeiza asilimia 55 za mradi wako wewe umebakiza 45. Na miradi ming ya tz huanza hiz. Mwisho wa siku serkal unakuta imebakiza hata 20%.
 
Nafikiri hii ni habari njema, siku zote TANESCO iligeuzwa sehemu ya kupigia hela wakubwa, Mungu atusaidie huu muujiza uwe halisi.
 
Tunategemea Na Mbunge mmoja aliepo matibabuni Ughaibuni nae atajiunga Na Jeshi la Wazalendo chini ya Jemedari Daktari Mahiri
Ila tukiacha unafiki wa kisiasa
Wewe,Ritz,Faiza,chama,Big show,mkandara,rejao,nk huwa mnaongozwa na mahaba ya kidini.
Mnakuwa ccm anapokuwepo mtu kama mwinyi na jakaya.
Mnarudi CUF akiingia mtu Julius,Benyamini na John.
Akiingia Januari wote mnamuacha leproffesseri na Maalim wenyewe.
Hata Maembe akiingia mtampenda kwa kuwa ni rimoti kutokea Msoga.
Nyie bana hamuipendi ccm wala mnaipenda dini.
Na hili linanikumbusha moja ya hutuba za almarhum ustaadh Ilunga Mwanza aliyewaambia wafuasi wake kuwa hakipendwi chama bali anapendwa muislamu yoyote anayewakilisha chama chochote kupampana na mgalatia
 
Tanzania agrees to construct $3 billion dam in wildlife park

14 hrs ago

Tanzania agrees to construct $3 billion dam in wildlife park

14 hrs ago
https://www.linkedin.com/shareArtic...rce=http://a.msn.com/0G/en-xl/BBQQPvD?ocid=sl

http://a.msn.com/0G/en-xl/BBQQPvD?ocid=sf

https://twitter.com/share?url=http:...rer=http://a.msn.com/0G/en-xl/BBQQPvD?ocid=st

https://web.skype.com/share?url=htt...99772a-8e80-44c5-873b-50bc7d375321&source=msn


BBQQG12.img
© Magdalene Mukami/Anadolu Agency/Getty Images File picture of Tanzania President John Magufuli in a press conference.
DAR ES SALAAM, Tanzania — Tanzania on Wednesday signed a $3 billion agreement with two Egyptian companies to construct a huge hydroelectric plant in a game reserve that is a UNESCO World Heritage site.
President John Magufuli witnessed the signing of the agreement with Egyptian Prime Minister Mostafa Madbouly. The companies involved are Arab Contractors and el-Sewedy Electric, an engineering services company.
Conservationists have opposed the construction of the 2,115-megawatt hydroelectric plant along the Rufiji River in the Selous Game Reserve. The reserve is renowned for its animal populations and variety of wildlife habitats.
Conservationists say the project would destroy the environment, which also is key tourist draw and source of revenue for the East African nation. Conservation group WWF, which has openly opposed the project, was not immediately available for comment.
The plan was formulated in the 1980s but Tanzania did not have the capital to put it into effect until recently. Magufuli now says his government is financing the project itself.
Egypt's state news agency said the dam is expected to produce 5,920 gigawatts of power annually.
 
These people are alarmist! Hivi kweli tushindwe kutumia resources zetu kujipatia umeme wa uhakika kwa sababu tunatunza urithi wa dunia (kitu ambacho tumekitekeleza kwa miaka na miaka)? Mbona Mzee Trump amejitoa kwenye Paris Climate Agreement, anapambana na uzalishaji wa coal na mengineyo? Hawapigi kelele?


Watuache tupambane na hali zetu bwana..Umasikini huna heshima!
 
Watunze hivyo vyingine vilivyobaki hiii tunakazi nayo!hawawazungu wapuuzi sana
 
Mbona waliokuwa na licence ya uchimbaji uranium mkuju river walikubaliwa kumegewa kipande cha Selous iweje kwetu iwe ajabu
 
Naona tuko bega kwa bega na Misri katika mradi huu
Tunaomba tuelezwe Concenssions zetu kwa wamisri juu ya Ziwa Victoria baada ya hii ishu, Usije ukakuta wametuwezesha kujenga Stieglers halafu huku behind the scene tumeridhia mkataba wa maji wa kikoloni unaowapa haki Wamisri juu ya ziwa victoria kuliko sisi wenye maji!
 
Mradi wa umeme wa Stieglers Gorge utaipaisha Tanzania ya viwanda kwa kiwango ambacho si rahisi kuona hivi sasa.
Lakini ni kwa kiwango kikubwa.

Mradi ukikamilika Tanzaniabutakuwa imeongeza 2100MW katika gridi ya Taifa.
Hapa na mimi nitatembea kifua mbele, kama atuhimizavyo mh. Magufuli.

Sasa miradi kama ya kuchenjua madini itawezekana kutekelezwa nchini.

Mfano tu, Akosombo Dam huko Ghana ina installed capacity ya 1038MW(NUSU ya stiegler), lakini Ghana ilifanikiwa kuwa na moja ya smelter kubwa Afrika ya kuchenjua Aluminium.

Hapa nasema, Mh John Pombe Magufuli kalamba dume.
 
Awamu ya 4 (kikwete) ilituaminisha kuwa umeme wa Gas ndio rahisi na utashusha bei ya umeme na bidhaa kwa ujumla! matokeo yake umekuwa na umeme uliotumia mabilioni ya shilingi na tulichoaminishwa hakuna.

Awamu hii ya 5 inatuaminisha kuwa umeme huu wa maji utakuwa ndio rahisi zaidi na utashusha bei ya bidhaa na tutatembea kifua mbele.

Awamu ya 6 huenda tukaja kuambiwa umeme wa majenereta ndio mzuri, wenye unafuu kuliko hiyo mingine!
 
Rais John Magufuli ameshuhudia utiaji saini wa ujenzi wa mradi wa umeme wa Bonde la Mto Rufiji wa Stiegler’s Gorge kati ya Serikali ya Tanzania na Misri, akibainisha kuwa mradi huo utasaidia kutunza mazingira tofauti na baadhi ya wanamazingira wanavyokosoa.

Akizungumza janaJumatano Desemba 12, 2018 Ikulu Dar es Salaam katika utiaji saini huo ulishuhudiwa pia na Waziri Mkuu wa Misri, Mostafa Madbouly, Magufuli amesema mradi ulipigwa vita kwa kisingizio cha kulinda mazingira na kusisitiza kuwa unalenga kutunza hayo mazingira.

"Lazima tujifunze kwa waliotutangulia, sisi tuna megawati 1500 wenzetu wa Misri wana megawati zaidi ya 25,000 na maji wanayotumia yanatoka Kagera, lakini kwetu hata hapo Kagera umeme hakuna.

"Nawaomba watanzania hasa wale wanaopenda kusemasema wasitumiwe na mabeberu, huu mradi hauna dini, si wa chama, huu ni mradi wa watanzania wote na ni kwa faida yetu sote watanzania, naomba wasitumiwe na mabeberu.

"Nawapongeza watanzania kwa kutekeleza mradi huu, ndio maana nasisitiza tulipe kodi. Kuamua ni kitu kigumu, nashukuru wabunge na watanzania kwa kuamua, tungeanza hata kutekeleza kidogo kidogo leo tusingefikia hapa au a kupata matatizo haya ya umeme.

"Mradi huu una baraka nyingi, nimekaa kwenye wizara ya ujenzi kwa miaka 23 na tulisaini miradi mingi lakini sijawahi kuona mradi ambao wakati wa utiaji saini kuwa na idadi ya viongozi wetu wa dini kiasi hiki, ndio maana nasema mradi huu umebarikiwa.

"Tulipoomba watukopeshe kwa ajili ya mradi huu wakakataa lakini tulipowaambia kuhusu kuingia ubia wakakubali, maana yake ubia ni biashara na wao ndio watatupangia bei, ukiona nchi imefikia hatua ya kupangiwa bei ujue tumekwisha, ipo siku watasema hatuwashi kabisa.

"Wakati tunakaribia kutia saini mkataba huu, Mhe. Rais wa Misri niliongea nae alisema atashindwa kuhudhuria tukio hili lakini ameniambia mradi huu ataubeba kama mradi wake.

"Tukikamilisha mradi huu, umeme utapatikana kwa bei rahisi, hata bidhaa za viwanda zitauzwa kwa bei ya chini, uchumi wa nchi utakua lakini pia uchumi wa mwananchi mmoja mmoja utakua.

"Wapo wanaosema kuwa mradi huu utaharibu mazingira, si kweli hata kidogo, Mradi huu ni rafiki wa mazingira kwasababu umeme wa maji ni rafiki wa mazingira, lakini eneo litakalotumika ni 1.8% hadi 2%.

"Mradi huu tuliona unafaa kwa sababu chanzo chake ni cha uhakika, gharama zake si kubwa kulinganisha miradi ya vyanzo vingine, lakini pia mito yake ni kutoka sehemu ambazo hupata kiasi kikubwa cha mvua kwa mwaka.

"Nimefurahi baada ya miaka 40 mradi huu unatakelezwa, ni furahi zaidi unatekelezwa kwa fedha zetu wenyewe, utagharimu shilingi trilioni 6.558, wakati Yesu anawakimbia watesi wake alikimbilia nchi ya Misri, na sisi pia kwenye swala la umeme tumekimbilia Misri."Amesema Rais Magufuli
 
Wakati wa makenikia tuliambiwa kuwa tumelamba dume na tutalipwa zaidi ya sh trion 485 tumeshalipwa au Bado?
 
Awamu ya 4 (kikwete) ilituaminisha kuwa umeme wa Gas ndio rahisi na utashusha bei ya umeme na bidhaa kwa ujumla! matokeo yake umekuwa na umeme uliotumia mabilioni ya shilingi na tulichoaminishwa hakuna.

Awamu hii ya 5 inatuaminisha kuwa umeme huu wa maji utakuwa ndio rahisi zaidi na utashusha bei ya bidhaa na tutatembea kifua mbele.

Awamu ya 6 huenda tukaja kuambiwa umeme wa majenereta ndio mzuri, wenye unafuu kuliko hiyo mingine!
Mkuu, ndo ukweli wenyewe mradi utashusha sana gharama za umeme.
Gharama zutu ni za juu mno wakati huko Ulaya, na hata S Africa gharama zao ni karibia only 10% ya gharama zetu.
 
Back
Top Bottom