Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Huyu jamaa ataleta mambo ya kisheria ataibinua ataifunua ataifunika hiyo hati
 
Lisu amewabana hadi hati imetoka. Sasa kinachofuata ni kuwa makubaliano yaliyopo kwenye hati ndo yafuatwe. Wazanzccm ndo watakiona.
 
Walio omba ni wajumbe wa katiba wapelekewe wao ndio watajua ni feki au Original
 
Eti CCM wamegushi saini za Hayati Mwl J. K. Nyerere na Abeid Aman Karume, wameongeza me kwa Karume (kitu ambacho si kawaida ktk saini ya mtu alfabeti kuachana) kwa kutumia komputa (Scan > edit>print). Hata hapo naona kuna hiyo dalili. Je ni kweli au?

Unayosema ni sahihi! NJIA YA MWONGO NI FUPI!!! Ni wakati wa Mungu kuwaumbua waliozoea kudanganya wananchi, kwamba kuna Al-Shaabab, kwamba eti kuna Mkenya amekamatwa aliyeenda kutubu kwa Gwajima jinsi alivyomtesa Ulimboka kwa lengo la kumuua. MUNGU HADHIHAKIWI!!! Wamechokoza moto mkali zaidi!!!!!!!
 
Kwa nini bavicha mnamatatizo makubwa kiasi hiki kila kinachofanyika kwenu ni hapana basi nadhani kazi ya kuuza bangi inawafaa.
Mtawadanganya haohao mambumbu wenu,hapa mpaka kieleweke ikiwa ikulu hadi biashara za sembe zinafanywa sembuse magumashi ya hati..
 
Sunzu huyu jamaa habahatishi heri slaa awe rais kuliko Tundu lissu KUWA mbunge sasa amrkuwa mbunge duuuu
 
SIamini na wala sikubali kuwa tuna hati 2 ZA muungano. Ile yenye saini feki iliyopelekwa mwanzo na hii ya Sefue aliyowaonyesha wachaguliwa wa waaandishi habari mchana huu. Naomba majibu haya kwa nini walipeleka hati tofauti bungeni? Je Zanzibar wameapprove kuwa hiyo Ndio kweli halisi? Naona sasa suala la muungano lirudi kwa wananchi.
Mkuu nakubaliana na wewe katika hati hii Saini ya Nyerere imeonekana kwa rangi yake lakini hii ya Karume inaringana Rangi na maandishi mengine kwa hiyo panahitaji ufahamu wa hali ya juu kuyaona haya ebu angalia picha hizi hapa chini.

View attachment Saini Nyerere.BMP

View attachment Saini Karume.BMP
 
Haya hoja ya kuto kuwepo kwa hati imepata jibu sasa ngoja tusubili kama ni yenyewe isije ikawa imechakachuliwa maana hawa jamaa wa serikali kwa uchakachuaji wako vizuri.

Kumbuka swali la tatu la Lissu, kama hati ni halali je muungano ni halali?
 
Kwa kuleta hati nyengine ya mungano serikali wamekubali kuwa Ile ya mwanzo ilikuwa feki,je tutaiamini vipi kama hii ndio hati halisi!!walisema hati iko ikulu kwanini katika hati inaonyesha kuwa imekuwa faxed mwaka 2013
 
Juu kabisa kama si macho yangu nasoma yafuatayo;

FAX NO. 2117272

Date April 14 2013

Time 09:55am



Je hii ndiyo maandiko ya 1964?

Kaka!
Kwani ile hati aliyoionesha Sefue si ilikuwa binded, na
aliionesha mchana! na
Waandishi ndo waliipiga picha!

Huoni kuwa hii hati kwenye picha ni kama imetolewa copy na haijawa binded na picha imepigwa usiku na aliyeishika ndo amepiga picha,

Kabla ya kuulizia hiyo fax Jiongeze kwanza mkuu.
 
Hiyo hati ilitumwa kwa njia ya FAX tarehe hiyo toka point A kwenda point B; wewe ulitaka FAX ionyeshe mwaka 1964?
Issue ya msingi hapa ni kwamba, je hati hii ni halali au ni feki.

Ikulu imejichanganya. Tunahitaji original documents kuhakiki. Fax,photocopy, transcripts hazikubaliki!
 
Safi sana Ikulu kwa kukata mzizi wa fitina.

Kwa sasa kelele za hati ya muungano zimekatwa. Tuendelee na mijadala ya msingi yenye maslahi kwa taifa.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itadumu ingawa ina maadui wengi. Pamoja tutashinda.
 
Nakwambia huyu jamaa balaa achokonoi sana anawavuta Kama ulimbo wakikaribia wananasa ngoja zifike yeye alichotaka waitoe tuu ili alipue
 
Hati ya Muungano imetolewa, na imeshapelekwa Bungeni dodoma. Tundu Lissu alisema HATI hiyo haipo hivyo Muungano huu ni feki, na taifa hili ni feki.
Kama kweli hati hiyo aliyoionyesha leo Katibu mkuu Kiongozi ni yenyewe.....Kuna watu wataabika sana kwa hoja za jazba bila kuzifanyia uchunguzi.
Natamani iwe uongo ili huu umaarufu tuliompa leo Tundu Lissu uweze kudumu, kinyume na hapo itakuwa aibu sana.
 
Kuna wakati najiuliza ni nani wa kuwawajibisha hawa viongozi wa hii nchi nashindwa kupata jibu!! Hebu subiri muone kama kuna atakayewajibishwa au hata kuulizwa tu kwa kughusha hiyo iliyopelekwa bungeni!!!!
 
Back
Top Bottom