Uchaguzi 2020 Ikungi: Magufuli amuahidi Lissu kazi, amuambia aachane na Urais ambao hatashinda

Uchaguzi 2020 Ikungi: Magufuli amuahidi Lissu kazi, amuambia aachane na Urais ambao hatashinda

Umepanik sana,JPM kawachapa panapostahili,kwani uongo?hata Tundu anajua anafanya masihara hayupo siriaz
Kuliko udhalilishaji kwa umaskini na maisha yako bora unyanyaswe kwa mambo mengine, Mzee leo kawaambia Singida kuwa atawapa kazi ndogondogo maana hawana nguvu ya kuwa na mgombea wakuingia Ikulu.

Kwanini tumepaniki kiasi hiki? Hatukujipanga kufanya kampeni? Eleza sera zako acha wananchi wachague siyo ueleze Mambo binafsi.
 
Hapa tafakuri inahitajika kiwango Cha Lami, hiyo kauli yake inatafsiri Mengi mbele ya huu uchaguzi.
 
Hili ni tusi kwa wanaikungi na kwa wanasingida wote adhabu yake ni kumfundisha Magufuli kwa kupeleka kura kwa Lissu, kuonyesha dharau kwa Lissu ni kuwadharau wanaikungi na wanasingida kuwa Magufuli akishinda hawana hadhi ya kupewa kazi yoyote labda kazi inayolingana na wahudumu wa Ikulu.
 
Mr President nadhan sasa uwe wakati wa kutuambia unakwenda kutufanyia nini miaka hii mitano? Maana kama ni maneno ya kwenye send-off tushayasikia imetosha sasa.Watumishi wanalia madaraja hayasomeki,incriment yenyewe hakuna,mazingira ya walimu na wanafunzi pia mabovu,wakulima pembejeo gharama zipo juu,miundombinu vijijini Ni mibovu wanavijiji wanasafiri kwa shida hasa kipindi Cha mvua tunatumia mapenzi yao na kutoelewa kwao juu ya serikali mbadala kuendelea kuwageuza mitaji yetu na makarai ambayo hutupwa ghorofa linapokamilika.
Manyimbo ya uchumi wa kati hayatavutii sisi wa vijijini, kwanza hatuyaelewi wala hatujaona tofauti yoyote popote.

Baada ya kucheza muziki tangu alfajili bila kula, kule Dodoma alisema keshajenga viwanda elfu 60. Ingefaa watuonyeshe tuwahi ajira kwanza matumbo yauma wajameni.

Ili atakapoleta hiyo midege mingine mipya, itukute tumeshiba na tuna uwezo wa kuitumia hii iliyopo kwenda kwetu Igulumbilo na kurudi kwenye matamasha hata wakati wa mvua ya kifuku.
 
Hahahah kati ya Lissu na JPm nani aliyepaniki?

Hadi leo Lissu hana hata anayoenda kufanya yeye ni kutukana na kulalamika tu kwa Magufuli hahhahaha bora asubiri hiko kikazi kidogo kuliko kujisumbua na kumaliza mafuta ya gari bure tu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Matusi ya Lissu umeyasikia wapi?
 
We endelea kutoa takwimu za kubumba, ila mjue wapiga kura wana hasira kuu! Na mwaka huu wapinzani walishaonya ule mchezo wa nyuma ya pazia! Hakutakuwa na cha kumwachia Mungu tena! Anaeshinda ashinde kihalali na anaeshindwa kweli ashindwe kihalali na maamuzi ya wapiga kura yaheshimiwe!
SASA BASI
 
Hivi kamanda Tindo unategemea Tundu kuchaguliwa na Watanzania awe Rais?hata yeye mwenyewe anajua anazuga

Suala la yeye kuchaguliwa na watanzania kuwa rais hilo wala halina mjadala, labda uzungumzie idadi ya kura kutokutosha. Na kimsingi Lisu hana tatizo na kutopata kura za kura za kuwa rais, bali ana tatizo na kura za kubumba ili kutangaza mshindi kinyume na kura za wananchi.
 
Majengo zahanati,vituo vya afya, maji.. Eti Sikuwahi kuombwa maji.... Mtaturu miezi michache kaniomba maji... wengine walikuwa hawaombi ( Lissu).. Hivi miradi afya,maji ,barabara ni hisani ya mtawala!?
Huyu jamaa kajisahau kabisa. Anafikiri kodi tunazolipa kugharamia maendeleo yetu anazimilki yeye na ni za kwake.
 
Back
Top Bottom