Ila Bashe! Nchi ina upungufu wa sukari tani 30,000; yeye anaagiza tani 400,000!

Ila Bashe! Nchi ina upungufu wa sukari tani 30,000; yeye anaagiza tani 400,000!

Lakini si sheria, maana hujaeleza hivyo.
Na hata kama ingekuwa ni sheria, sasa sheria hiyo inatumika vibaya; hata kama dharura yenyewe haipo, au kiasi kinacho agizwa kinakuwa hakiendani na ukubwa wa dharura.

Huu ni mwanya tu, unaotumika sasa kufanya upigaji, na katika hili, ni wazi huu siyo upigaji wa Bashe; yeye ametumika tu kwa vile wizara yake ndiyo yenye mamlaka.

Dalili zote tayari zinaonyesha serikali nzima hata Bunge linahusishwa, ndiyo maana huyo Binti Fito anavyomsurubu Luhaga Mpina.

Acha vichekesho 'john', uliona wapi bei ya sukari ikishuka; au hiyo wanayosema ilifika Tsh 10,000/ kwa kilo?
Hizo ni komedi tu zinaeleweka.

Haya weka uwiano hapa: Tani 400,000, kushusha bei ya sukari?
Alichofanya Bashe ni Ujanja mdogo Sana, yeye alijua wazalishaji wameficha sukari Ili kutengeneza scarcity hivyo akawaruhusu waagize nje huku akijua kabisa hawataagiza kwa sababu sukari wanayo

Bashe akaongea Bungeni Kwamba Wazalishaji wakiendelea kudelay atatoa Vibali kwa Watu wengine Ili waagize sukari

Wazalishaji wanashindwa na Bashe akatumia Mwanya huo huo kufanya aliyoyafanya

Kimjinimjini tunasema Bashe alitumia Fursa ipasavyo

Unadhani kwanini Dr Mwakyembe hakwenda kumhoji Lowassa kashfa ya Richmond?!

Mabepari Wana akili Sana tofauti na wakulima wa vitunguu akina Lucas 😂😂😂
 
Sasa ndo unatafuta mtu mwenye mtaji wa mil moja, ccm babu ,mama ,baba, kaka,dada mpaka vitukuu wote wezi , ccm ni ukoo wa panya
Ukiwa na Tenda ya Serikali mkononi iliyo nyeti Bank wanakupa mkopo ndani ya dakika 0 😄😄😄
 
- Kwanini watu wa stationery wasio na ujuzi wowote kuhusu masuala ya uagizaji na usambazaji wa sukari wapewe hiyo kazi? Uko wapi usalama wa mtumiaji wa sukari?

- Inawezekana vipi mtu wa stationery mwenye mtaji wa milioni moja akapewa kazi ya kuagiza sukari ya bilioni 6.6?
Sukari Hata wewe unaweza kuagiza Bwashee 😃

Iko TBS
 
Tena wemeagiza kiasi kidogo huku mtaani mahitaji ya sukari bado ni makubwa sana kilo moja ni zaidi ya TSHS. 3000 halafu mnaleta siasa kwenye mambo serious.
 
Afu bei iko pale pale dadeki[emoji28][emoji28][emoji28]nchi ya kis*nge sana hii
 
Tz kila waziri ni mwizi,yule njaanuari akaona na yeye ashushe mijengo nje ya nchi ili apate pa kuiba,baada ya kuona kwake pa kavu
 
Mafuriko ya mwaka jana na mwaka huu miwa ya wakulima yote imeharibika kwa asilmia 80, kwa hiyo nchi itavuna sukari ya maana mwakani. Iliyopo ni kidogo, kwa hiyo upungufu wa sukari utaendelea kwa muda mrefu mpaka wakulima wavune tena miwa.

Kagera ilifikia muda magari ya kusomba miwa yanashindwa kuingia shambani kutokana na mafuriko, miwa yote ikaharibika. Sasa hilo gepu la miwa iliyoharibika linajazwaje kwa karibu mwaka mzima? Morogoro hivyo hivyo, mafuriko yalitamalaki

Unakikua kilimo au unahadithiwa. Miwa haiharibiwi na mvua nyingi. Mvua inaweza kuathiri tu usafirishaji, na siyo production. Mvua zilizonyesha mwaka huu zilikuwa nyingi kwa muda mfupi tu, hivyo athari yake katika usombaji wa miwa kupeleka viwandani, haupo. Maeneo yote, ya uzalishaji miwa, usafirishaji umekuwa wa kawaida kuanzia mwezi wa 5. Hivyo huo wizi wa Bashe hauna uhusiano wowote na uwepo wa mvua nyingi. Hiyu ni mwizi tu. Maana hata huko kwenye miradi ya kilimo ni wizi mtupu. Hata waliopewa tenda kwenye hizo kazi hewa, wanatamba kuwa Bashe hawezi kuwanyima tenda kwa vile kila wakilipwa, wanamkumbuka. Wanayasema hayo kwa uwazi.

Huyu msomali kiuhalisia anaonekana ana asili ya wizi na tamaa. Usalama wake katika wizi anaoufanya, kuna uwezekano mkubwa anaihusisha ofisi ya iteuzi. Maana hata hayo ya kununua pikipiki nyingi ndiyo mbinu ambayo amekuwa akifanya tangu uchaguzi wa 2010.

Mwaka 2010 alikuwa ndiye mpanga mikakati ya Lowasa na Rostam. Kwa kutumia pesa ya Lowasa na Rostam alinunua pikipiki na baiskeli nyingi kwaajili ya kuwahonga viongozi wa chama. Mabolozi wa nyumba kumi jimbo la Nzega, kila mmoja alipewa baiskeli. Na baadhi ambao yeye aliwaona ni muhimu zaidi, waligawiwa pikipiki.
 
Kijana wa kinana au kijana wa kikwete

Kwenye huu utawala hata wafanyakazi nini hawezi kuadhibiwa

Bashe siyo wa Kikwete. Bashe ni mtu wa karibu na Kinana. Labda kwa sababu ni msomali mwenzake. Lakini pia ni mtu wa karibu sana na Rostam. Na kwa sasa amekuwa karibu sana na mama. Huu wizi wa mabilioni mengi kiasi hiki, lazima hawa wote wanahusika. Bashe ni mtekelezaji tu. Inatafutwa pesa ya kampeni, mpangaji lazima atakuwa ni yule yule, wa EPA na Kagoda, mr. Rostam. Huyu kwenye upigaji mkubwa wa pesa unaoihusisha Serikali, huwa hakosekani. Kwa muda mfupi amekamilisha ufisadi kupitia bandari na sukari. Na kabla ya uchaguzi, lazima atatengeneza dili jingine. Mwakani kwenye uchaguzi kutakuwa na mamia ya mabilioni ya pesa ya kuchezea ili kuwaondoa ufahamu wote wenye tamaa ya pesa, na kuwafanya watekeleze watawala wanachokitaka.
 
Mbona ujuaji ni mwingi waTanzania, sukari ikiadimika mnalalamika ikiwa excess mnalalamika, sasa hamuoni sukari ikiwa nyingi ndio bei inashuka?

Duh hii nchi ngumu sana
Binadamu ni lazima utumie akili. Ufahamu kuwa watu waovu, mara nyingi hujinufaisha kupitia matatizo ya watu. Ndiyo maana kijana anayehangaika kutafuta ajira, na hana namna nyingine ya kuendesha maisha bila ya ajira, ni rahisi sana kukutana na matapeli, wakamwibia hata kidogo alicho nacho, na ndicho alichokifanya Bashe. Upungufu mdogo wa sukari ameutumia kufanya ufisadi mkubwa kupindukia. Huyu ni mwizi na fisadi. Hana jina jingine.
 
Hizo Tani 400,000 Bado hatujawa na sukari ya kutosha nchini Sasa Tani 30,000 Hali ingekuwaje ufipa mna shida sana.
 
Unamteuwaje msomali kuwa waziri tatizo liko kwa Samia

Prof mkenda aliiweza sna wizara ya kilimo

Bashe ni mzuri sana katika kutumika kwenye uovu. Alitumika sana wakati ule Rostam akiwa kwenye peak ya siasa za Tanzania. Kwa kutumia pesa ya Rostam, hakuna mgombea ndani ya CCM aliyeweza kumshinda Bashe kule Nzega. Kwenye kura za maoni Seleli alipigwa chini kwa mbali, Kigwangala alipigwa chini kwa mbali kabisa. Lakini kwa sababu Kikwete alikuwa anajua namna Bashe alivyo mchafu na anavyotumika, pamoja na kuwa na kura nyingi za wajumbe waliohongwa kwenye kura za maoni, walimwondoa, na akakamatwa na askari wa uhamiaji.
 
Watuthibitishie kama sukari hii ilipimwa na kuthibitshwa kwa matumizi ya binadamu.
 
Ameibaje? embu tupe mchanganuo

Ina maana wewe huna akili ya kuelewa jinsi Bashe alivyoiba mabilioni ya pesakupitia uagizaji wa sukari? Upo wapi?

Unaambiwa kuwa waagizaji waliongeza sh 100 kwa kila kilo. Sasa chukua hiyo shilingi 100 tu, zidisha kwa maelefu ya tani zilizoagizwa. Na hiyo pesa yote ndiyo iliyopelekwa kwa Bashe.
 
Mbona ujuaji ni mwingi waTanzania, sukari ikiadimika mnalalamika ikiwa excess mnalalamika, sasa hamuoni sukari ikiwa nyingi ndio bei inashuka?

Duh hii nchi ngumu sana
Wapi huko sukari imeshuka? Nilitarajia sukari iwe kilo Tsh 1,000 baada ya mafuriko ya sukari.

Mbona mahindi bei imeshuka kisa uzalishaji upo mwingi
 
Mafuriko ya mwaka jana na mwaka huu miwa ya wakulima yote imeharibika kwa asilmia 80, kwa hiyo nchi itavuna sukari ya maana mwakani. Iliyopo ni kidogo, kwa hiyo upungufu wa sukari utaendelea kwa muda mrefu mpaka wakulima wavune tena miwa.

Kagera ilifikia muda magari ya kusomba miwa yanashindwa kuingia shambani kutokana na mafuriko, miwa yote ikaharibika. Sasa hilo gepu la miwa iliyoharibika linajazwaje kwa karibu mwaka mzima? Morogoro hivyo hivyo, mafuriko yalitamalaki
umesoma kilichoandikwa ukaelewa au umejibu kama mwanaccm?
 
Kwani ametumia hela yako au ya Serikali kuagiza sukari? Pili kipi bora sukari iwe nyingi mpaka iteremke bei kutoka Tsh 10,000 hadi Tsh 3,000?

Hata huyo Lowassa (RIP) kwani alikosa nini kwenye kashfa ya Richmond?
1. Sukari haitashuka itaendelea kupanda, sababu tuna inflation
 
Swali la msingi ,na naomba jibu kwa Mwenyekujua, Bashe kama waziri inawezekana kukamilisha hili dili peke yake ndani ya serikali ? Kama sivyo nani wanaweza kuwa nyuma yake ? Kama ndivyo hii jeuri bashe kaitoa wapi?

Nauliza isije kuwa bashe ni kama bahasha tu kumbe kumbe wenye barua wapo
Hii issue ni kubwa sana... Samia is politically weak Ndio maana bungeni wanamtetea sana mwenyekiti wao
 
Mpina alipokuwa Waziri alifanya operation ya kukamata na kuchoma nyavu ambao Wabunge wa CCM walikuwa wanamiliki, hili jambo ni kama liliwauzi Wana CCM wengi sana
 
Back
Top Bottom