Ila kuna namna Wanaume mnapenda sana matatizo

Ila kuna namna Wanaume mnapenda sana matatizo

Labdaa kama umetoa laki 2 ya mahari kwa kila mmoja

Mahari ya 3M huwezi kutoa kwa kila mwanamke Kijana wa hovyo wewe😅😅
Hiyo kawaida tu , mwenyewe nimelipa mahari kwa wazazi wa mabinti watatu tofauti na kila mmoja anajua baada ya mwaka ataolewa ,ila kiukwel sina mpango wa hata mmoja.
 
Wakuu nadhani mko salama,.

Ntajaribu kutumia codes isijekua wahusika wako humu nikawa nimechomoa betriii,.

Ni hivi,.
Kuna last born wa bibi yetu ambaye mwaka huu mwezi9 anatarajia kufunga ndoa,. Yaani process zote za uchumba na mahari zishafanyika na kamati zishaundwa watu tunaendelea tu kukumbushana michango kwenye group la harusi yake,...

Mambo yote yanafanyika ikiwa Muolewaji bado yuko nje ya nchi alirudi mwaka jana kuja kutambulishwa na alivyovikwa pete ya uchumba akaondoka tena akakamilishe mambo yake ili arudi moja kwa moja kwajili ya ndoa yake,.( Hii inaweza kuwa sababu maybe ),,.means process zingine kama hivi vikao ni ndugu wa pande zote mbili ndio wanahusika,.

Shida ni kwamba huyu Uncle huku kuna mwanamke anaishi nae asa sijui ni mpenzi tu au ni rafiki au sijui imekuwaje lakini ndio hivyo wanaishi wote kinyumbani kabisa,. Nakumbuka tulifanya misa kwajili ya marehemu wa ukoo pamoja na kutengeneza makaburi huyu binti nae alikuja tena aliongozana na dadake kabisa walikuja wote kuungana na sisi,. Na huwa akiwa anapita labda na safari zake lazima apitie kwa bibi amsalimie na kina mama pia ndio hivyohivyo mara vizawadi zawadi ilimradi tu kujipendekeza ukweni,. Hajui kama uncle tayari kashachumbia na anatarajia kuoa mwaka huu,. Na hakuna aliye nyanyua mdomo kumwambia sio Marafiki wa Uncle , Sio ndugu wala mtu yeyote maana Uncle mwenyewe kama anavuta bangi ni mtata balaaa hataki kuambiwa chochote na mtu yeyote,. Kina bibi wameongea nae weee na kina mama ndio kwanza anawaambia yeye mwanaume mambo yake anajua namna ya kushughulika nayo,.

Hivi mtu kama huyu si anatafuta tu matatizo jamani ndugu wa Mume tuonekane hatuna maana?,. Binti wa watu akijakujua kama anachezewa tu na haolewi si tutarogwa ukoo mzima jamani😃😆😅😅,. Maana hadi nyumbani ( ukweni) ameshawahi kuletwa na kuja sio mara moja,. Na Je wakitokea wakuda wakampasha habari muolewaji kuwa huku jamaa yuko na mwanamke mwingine maana ni yuko free anaenda nae kila mahali na trip zake zote wanaenda itakuwaje??,. Mtu si anajiharibia maisha yake mwenyewe jamani?,.

Sometimes wanaume sijui mnakutwaga na nini,. Yaani mnajitafutieni matatizo tu sijui huwa mnawaza nini ??
🤣
Kwani mlishawahi kumuuliza huyo anaeishi nae kwa sasa akasema hajui ikiwa hajui kuwa mwanaume wake anataka kufunga ndoa na mwanamke mwingine?

Ikiwa bado muulizeni.....😎😎😎😎

Inawezekana anajua ninyi tu ndio mnaoteseka.🤣

Hata muoalewaje anaweza kuwa anajua, muulize hivi, UNCLE ANAISHI NA DEMU NA WANAJIACHIA SANA, UNALIJUA HILO?

Halafu utatupatia mrejesho😎
 
Yaani sijui kwanini mnapenda kujiamini kupitiliza,.
Hatakama tamaa za mwili mtu unashindwa kuvumilia kwanza hata jambo tu lipite utaendelea na tabia zako mbele ya safari jamani,.

Me nachukia kweli aisee
Si umwambie huyo anko wako sasa. Sisi hatutaki mambo magumu. Yaan huyo dem ampe hifadhi anko siku zote amtelekeze kisa anaoa. Usikute wameshaelewana. Huyo muolewaji ataitwa wifi kama kawaida 🤣🤣
 
Huyu Uncle kwanza ana karibu miaka 10 na kitu hajawahi kurudi nyumbani wala kuwa na mawasiliano na yeyote,. Amekuja kurudi 2023 kwajili ya suala lake la kuoa ndio wazee wamemvutavuta mpaka mwaka huu maana walikua hawamwamini ,. Tena ndio anafanya mambo kama haya na ni mtata hataki kuambiwa lolote mnamfanyaje??
Inakuwaje wazee wa ukoo wanamuogopa kijana wao?. Kweli jamii zinatofautiana sana. Anyway ila mkimchukulia poa atawasumbua sana baadae na hii ishu yake maana ni kama mnashiriki hichi kikombe.

fikiria wewe ndio ungekuwa huyo dada then unakuja kushtukia mtu anaoa, si unaeza ukalaani ukoo mzima rafiki. Kupitia hayo maumivu ndio namna huyo uncle anaweza waponza wote.

Naelewa unaweza usiwe kwenye nafasi ya kumkanya huyo uncle ila nadhani unaweza kujiepushana hilo janga. Ni bora usishirik hii dhuluma maana hapo ni kumdhulumu mtu future yake. Mbaya sana hiyo.
 
Back
Top Bottom