Ila kuna namna Wanaume mnapenda sana matatizo

Ila kuna namna Wanaume mnapenda sana matatizo

Wakuu nadhani mko salama,.

Ntajaribu kutumia codes isijekua wahusika wako humu nikawa nimechomoa betriii,.

Ni hivi,.
Kuna last born wa bibi yetu ambaye mwaka huu mwezi9 anatarajia kufunga ndoa,. Yaani process zote za uchumba na mahari zishafanyika na kamati zishaundwa watu tunaendelea tu kukumbushana michango kwenye group la harusi yake,...

Mambo yote yanafanyika ikiwa Muolewaji bado yuko nje ya nchi alirudi mwaka jana kuja kutambulishwa na alivyovikwa pete ya uchumba akaondoka tena akakamilishe mambo yake ili arudi moja kwa moja kwajili ya ndoa yake,.( Hii inaweza kuwa sababu maybe ),,.means process zingine kama hivi vikao ni ndugu wa pande zote mbili ndio wanahusika,.

Shida ni kwamba huyu Uncle huku kuna mwanamke anaishi nae asa sijui ni mpenzi tu au ni rafiki au sijui imekuwaje lakini ndio hivyo wanaishi wote kinyumbani kabisa,. Nakumbuka tulifanya misa kwajili ya marehemu wa ukoo pamoja na kutengeneza makaburi huyu binti nae alikuja tena aliongozana na dadake kabisa walikuja wote kuungana na sisi,. Na huwa akiwa anapita labda na safari zake lazima apitie kwa bibi amsalimie na kina mama pia ndio hivyohivyo mara vizawadi zawadi ilimradi tu kujipendekeza ukweni,. Hajui kama uncle tayari kashachumbia na anatarajia kuoa mwaka huu,. Na hakuna aliye nyanyua mdomo kumwambia sio Marafiki wa Uncle , Sio ndugu wala mtu yeyote maana Uncle mwenyewe kama anavuta bangi ni mtata balaaa hataki kuambiwa chochote na mtu yeyote,. Kina bibi wameongea nae weee na kina mama ndio kwanza anawaambia yeye mwanaume mambo yake anajua namna ya kushughulika nayo,.

Hivi mtu kama huyu si anatafuta tu matatizo jamani ndugu wa Mume tuonekane hatuna maana?,. Binti wa watu akijakujua kama anachezewa tu na haolewi si tutarogwa ukoo mzima jamani😃😆😅😅,. Maana hadi nyumbani ( ukweni) ameshawahi kuletwa na kuja sio mara moja,. Na Je wakitokea wakuda wakampasha habari muolewaji kuwa huku jamaa yuko na mwanamke mwingine maana ni yuko free anaenda nae kila mahali na trip zake zote wanaenda itakuwaje??,. Mtu si anajiharibia maisha yake mwenyewe jamani?,.

Sometimes wanaume sijui mnakutwaga na nini,. Yaani mnajitafutieni matatizo tu sijui huwa mnawaza nini ??
Nyie subirini kurogwa tu...🤣
 
Aisee...! Kijana anakuja na hawara bila kificho hadi nyumbani na wote mnafahamu hilo na mnamkenulia meno sababu eti anavuta bangi..!?
Aisee kuna koo ni za hovyo sana yaani kabisa hamjui ya kwamba atakujatia ukoo aibu na wote muonekane ni majuha, hivi watu wazima kabisa mnawezaje kuendelea kuchangishana na kukaa vikao vya kupanga harusi ya kijana asiyejielewa.

Natamani huyo kijana mnikopeshe huku kwenye ukoo wetu naapa kwa miungu na mizimu ya mababu angeacha huo upumbavu.
 
Maumivu ya moyo baada ya kuachwa yanazidi msiba...

Wanawake wakiwa wahanga wakuu

Visasi na malipizi ya kuua kwa nguvu za Giza ila hata wanaomlilia Mungu nao anawalipia kisasi...
Hii ya Mungu kulipa kisasi haipo. Yaani uvunje sheria za Mungu wa kweli, alafu unexpect Mungu alipe kisasi kisa mtu kaachwa bila ndoa, hivi mnamjua kweli Mungu Mtakatifu?
Sheria pekee ni atavuna alichokipanda na pia sheria ya generation curse.

Ila kwa upande wa nguvu za giza ndo inawezekana.
 
Huyu uncle ni mtata mno,. Kwanza wanaweza wakamwambia wengine huko akahisi ni sisi aanze kutunyanyasa 😃😀
Hahahaha

Kaeni kwa kujitahahalisha, siku akiwa anawaangalia kwa jicho la upande upande huku kakunja sura mjue kashasanuliwa😂😂😂
 
Aisee...! Kijana anakuja na hawara bila kificho hadi nyumbani na wote mnafahamu hilo na mnamkenulia meno sababu eti anavuta bangi..!?
Aisee kuna koo ni za hovyo sana yaani kabisa hamjui ya kwamba atakujatia ukoo aibu na wote muonekane ni majuha, hivi watu wazima kabisa mnawezaje kuendelea kuchangishana na kukaa vikao vya kupanga harusi ya kijana asiyejielewa.

Natamani huyo kijana mnikopeshe huku kwenye ukoo wetu naapa kwa miungu na mizimu ya mababu angeacha huo upumbavu.
Ingewezekana tungekupatia tu bure hili jamaa wala sio hadi kukopa,.

Ameshasemwa sana sio na mama yake ( bibi ),. Dada zake na kaka zake lakini hakuna anayemsikia kwanza anasema hataki kufatiliwa maisha yake
 
Back
Top Bottom