Wote tulijua hayo mambo ndio atakayotembea nayo kwa kujidanganya na CCM yake kuwa wametekeleza ilani, Wanasahau kuwa waliahidi wananchi kufanya hivyo, na pia kufanya hivyo haikuwa jambo la hisani bali ni wajibu wao wa msingi kabisa! Lakini wenye akili na uelewa wanachoitaji kujua sio kile alichokwisha kifanya bali nini atakifanya na kitagusa vipi maslshi ya walio wengi! Zaidi ya yote kuna miradi mingine aliyotekeleza kwanza haikuwemo kwenye bajeti ya 2015/2016 wala mpango mkakati wa miaka 5 uliokuwa umeandaliwa na serikali ya awamu ya 4, mfano;-
1. Kuhamisha gafla makao makuu toka DSM kwenda Dodoma, Kwa jinsi serikali zilizopita zilivyowekeza katika miundombinu ya jiji la Dsm kulikuwa na haja gani ya kuhamia Dodoma haraka vile? Je uhamaji ule ulifanya analysis ya athari za kiuchumi kwa wananchi na hasa wawekezaji ambao waliwekeza Dsm kwa kuzingatia makao ya serikali?
2. Kujenga miradi na manunuzi ya vitu kama ndege 11 ambavyo havikutengewa bajeti, kumesababisha serikali kujikuta inafanya matumizi ya fedha bila kufuata kanuni za kupata ridhaa ya bunge. Hali hii ndio iliyosababisha serikali ikakosa uwezo wa kuajiri watumishi wapya na hata walioko maofisini wakashindwa kutimiziwa maslahi yao kwa wakati alafu mtu anarudi tena kwa wananchi na kuanza kuwaeleza habari hizoizo, kwa hakika ni wasiojitambua tu ndio watampa kura!