Hahaha
Mkuu Hakuna Mtu anayechukua Dhambi ya Mtu mwingine!
Hizo ni Hadithi Za Kipagani..
Biblia Yenyewe inakataa..
Agano la Kale..
"Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe; haki yake mwenye haki itakuwa juu yake mwenyewe, na uovu wake mwovu utakuwa juu yake mwenyewe."
"....... Bali kila mtu atakufa kwa uovu wake mwenyewe.....
- Kumbukumbu la Torati 24:16
"Baba wasiuwawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuwawe kwa ajili ya baba zao; kila mtu atauawa kwa dhambi yake mwenyewe."
- 2 Wafalme 14:6 (pia 2 Mambo ya Nyakati 25:4)
"
Lakini watoto wa wale waliomwua baba yake hakuwaua; kama ilivyoandikwa katika kitabu cha torati ya Musa, kama Bwana alivyoagiza, akisema, Baba wasife kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasife kwa ajili ya baba zao; bali kila mtu atakufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe."
haya Tuamie Kwenye Agano Jipya Sasa Linasemaje..
"Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe."
"Msidanganyike; Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna."
Basi Nimelizie Kwa Kukuandikia Nukuu Ya Habari Moja maana Wapo watakuja waanze Kusema Maandiko Haya Sijui Soma na Roho mtakatifu Sasa Nakupa Nukuu ya Kuwajibu..
1 Wakorintho 14:36-38
"Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu? Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana.
Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga."