Ilikuwaje Nyerere akamshinda Sykes?

Ilikuwaje Nyerere akamshinda Sykes?

Wazee ndani ya chama kipindi hicho hawakuwa na mlengo wa kimakundi kama siasa za siku hizi.

Kipindi hicho dhima na mikakati ya chama ilikuwa ni kudai uhuru. Hivyo alihitajika kiongozi mwakilishi msomi na mwenye kuweza kusimamia kile anachotamka kwa hoja zenye nguvu. Kwa muktadha huo, ni wazi Sykes asingetosha kuvaa kiatu na athubutu kama kiongozi msomi Nyerere.

NB; Siioni mantiki ya kuichepusha hii mada kwenye malumbano ya dini.
Halafu ieleweke wazi Nyerere alikuwa na connection kubwa ya wasomi wenzie ambao nauhakika Sykes wengi hakuwa akiwafahamu kiundani ukiachana na motive kubwa iliyokuwa ikitoka kwa wazee wa kiislam kutoka k/koo. Na nnaamini wazee hawa hawakuutanguliza uislam wao mbele kama jinsi anavyo tuaminisha mzee Mohammed Said kwenye machapisho yake.
Kisima,
Thread 'Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya' Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya
 
Huu ni uongo na uzandiki, nyerere na tanzania alisaidiwa na uingereza ndio kumpindua Idi amini, na sote tunajua Amin aliondolewa kwa ajili ya udini tu

Kuzikwa na watu wanne, kumi, elfu, laki sio wema wala ubaya, kuna ambao hawazikwi na miili haionekani kabisa
Ukute alieliwa na simba yupo mbinguni na aliezikwa na maelfu ya watu yupo jehannam
Weka ushahidi wa Uingereza kutusaidia vita dhidi ya Uganda hapa!! Siyo unaropoka ropoka hapa kama bata anayehara
 
Udini gani mnaouongelea? Kwani nyie wenye dini ya Idd Amini mlikuwa wapi kumsaidia? Kinachonisikitisha ni kuamini mambo ya kijinga kijinga kirahisi rahisi tu.

Kuna dhana ya kulipiza rafiki yake Obote kupinduliwa. Hii ina mashiko kuliko ya kuchukia dini ya Idd Amini. Ni ujinga mwingine mkubwa ambao wajinga wengine wameubeba na wanatembea nao.

Kumbuka, hali ya miaka ya sabini sio hali iliyopo leo. Udini gani mnaouongelea leo hii miaka karibu 45 iliyopita?
Na kweli obote alikuwa muislam
 
Bila shaka enzi hizo wakina Nyerere na Sykes walijali kuwa huru tu kutoka kwenye ukoloni.
Hawakujali ukristo wala uislamu au upagani wa mtu.
Ni wazee wa hovyo wenye chuki ndani yao ndiyo wanasambaza udini kwa vijana wapuuzi wa kizazi hiki kwa historia zao uchwara za kuji-victimize.

Udini unasambaa kama kansa ilhali dini zenyewe si hata zetu.

Thuuu!
 
City...
Moja ya sababu ambayo Hamza Mwapachu alitaka harakati za uhuru ziongozwe na Nyerere ni dini yake.

Wakristo wengi walikuwa nje ya harakati za kupambana na Waingereza.

Angalia waasisi wa African Association 1929: Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Humbi Ziota na Ibrahim Hamisi kisha unawakuta Cecil Matola, Raikes Kusi na Rawson Watts.

TAA Political Subcommittee: Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Said Chaurembo, Dr. Vedasto Kyaruzi, Steven Mhando na John Rupia.

Sheikh Hassan bin Ameir akiuza kadi misikitini.

Yako mengi.

Hamza Mwapachu aliamini ikiwa Nyerere ataongoza harakati za kudai uhuru hili vuguvugu litawavutia Wakristo kwa kuona kiongozi ni katika wao.

Hivi ndivyo ilivyokuwa.

Hamza Mwapachu aliogopa Tanganyika isidai uhuru wake ikiwa na vyama viwili vya siasa vilivyojikita katika misingi ya dini kama ilibyokuwa India kati ya Congress Party ya Ghandhi na Nehru dhidi ya Muslim League ya Mohamed Ali Jinah.
 
Kulingana na mahojiano ya Tundu Lissu na mtangazaji wa ITV , Lissu alidai mara ya Mwisho CCM kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti kwa ushindani ilikuwa mwaka 1954 kati ya Julius Nyerere na Abdulwahid Sykes. Ambapo Nyerere alimbwaga Abdulwahid Sykes. Uchaguzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Anatoglou.

Swali la msingi ilikuwa ni kwamba ilikuwaje Nyerere amshinde Sykes ambaye alikuwa ni mtoto wa hapa Dar na baba yake alikuwa kiongozi wa TAA hapo kabla. Yani Nyerere kutoka Musoma aliwezaje kuwashawishi wajumbe wamchague yeye wamuache Sykes wa Dar.

Tusaidiane mbinu alizotumia Nyerere kushinda uchaguzi huo maana haikuwa rahisi.
Sykes na wenzake walitaka nyerere akae hapo,wakajipiga goli la mkono,japo baada ya uchaguzi wakakaa pembeni na kutia shaka masmuzi yao kwa kumpachika mtu wasiyemjua vizuri
 
City...
Moja ya sababu ambayo Hamza Mwapachu alitaka harakati za uhuru ziongozwe na Nyerere ni dini yake.

Wakristo wengi walikuwa nje ya harakati za kupambana na Waingereza.

Angalia waasisi wa African Association 1929: Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Humbi Ziota na Ibrahim Hamisi kisha unawakuta Cecil Matola, Raikes Kusi na Rawson Watts.

TAA Political Subcommittee: Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Said Chaurembo, Dr. Vedasto Kyaruzi, Steven Mhando na John Rupia.

Sheikh Hassan bin Ameir akiuza kadi misikitini.

Yako mengi.

Hamza Mwapachu aliamini ikiwa Nyerere ataongoza harakati za kudai uhuru hili vuguvugu litawavutia Wakristo kwa kuona kiongozi ni katika wao.

Hivi ndivyo ilivyokuwa.

Hamza Mwapachu aliogopa Tanganyika isidai uhuru wake ikiwa na vyama viwili vya siasa vilivyojikita katika misingi ya dini kama ilibyokuwa India kati ya Congress Party ya Ghandhi na Nehru dhidi ya Muslim League ya Mohamed Ali Jinah.
Mzee umetisha sana, unamwaga madini kama yote, ila jamaa ni wadini kweli hawawezi kukubali, ila ukweli ni ukweli tu
 
Bila shaka enzi hizo wakina Nyerere na Sykes walijali kuwa huru tu kutoka kwenye ukoloni.
Hawakujali ukristo wala uislamu au upagani wa mtu.
Ni wazee wa hovyo wenye chuki ndani yao ndiyo wanasambaza udini kwa vijana wapuuzi wa kizazi hiki kwa historia zao uchwara za kuji-victimize.

Udini unasambaa kama kansa ilhali dini zenyewe si hata zetu.

Thuuu!
Sheikh suleiman takadir aliunusa udini akaonya,akatengwa,1968 waislam wakamjua nyerere ni nani,the rest is history
 
Elimu ndo iliyomsaidia ,..na pia ni vatcan city...mzungu alijua wazi angemkabidh uenyekit Muslim basi shule zake na makanisa yangekuwa banned
 
Elimu ndo iliyomsaidia ,..na pia ni vatcan city...mzungu alijua wazi angemkabidh uenyekit Muslim basi shule zake na makanisa yangekuwa banned
Huwa waongo waongo tu mmejaa chuki za kidini,walitaka waache kibaraka mkristu,maana kwao mwafrika mkristu ni bora kuliko asiye mkristu,wakampa na katibu muhtasi mwingereza Ili kimchunga,akateua mawaziri waingereza,wakoloni walewale aliodai wabaya
 
Huwa sikisii:
View attachment 3080206

Hapo nyerere kawachwa kwenye mataa, Malkia anaongea na mtawala wa kweli, Joan Wicken, alipokuja Dar.
1724776399161.png

😂😂😂, Alitema bungo na kumlilia Malkia.
Tatizo humu JF wamejaa mambulula, hawawezi kukuelewa
Na uwezo wa kiakili wa hawa wachangiaji wa JF ndio picha halisi ya Tanzania, ndio maana tuko kwenye giza.
 
Licha ya kwamba Nyerere alikuwa msomi ila ukweli ni kwamba kulikuwa na wasomi wengine, pengine wenye maarifa na upeo kumzidi yeye

Kikubwa ambacho mwalimu aliwazidi wenzake ni manipulation,. Nyerere alikuwa manipulator mzuri sana na hii ilimsaidia katika planning na utekelezaji la malengo yake.

Historia ya Nyerere imejaa mengi ambayo yapo nyuma ya pazia ila yanajulikana.

Uwezo wake mkubwa katika kupandikiza mbegu za anachokiamini ndicho kilichomsaidia.

Nyerere alikuwa smart dictator aliwabana waliompinga na waliokuwa kinyume na itikadi au malengo yake

Vichwa kama vya akina Oscar Kambona, Tuntemeke Sanga na wengineo waliweza kumpa challenge mwalimu Nyerere.

Ni hayo tu, nipo tayari kurekebishwa ila kiukweli isingekuwa rahisi kwake kumshinda mtoto wa mjini Sykes bila kutumia mbinu za ulaghai na manipulation.
Siyo ubingwa wa manipulation bali alikua chaguo la wakoloni, mwenyewe alitaka kuwa padre,askofu mzungu akamkataza,walishaona atawafaa kwenye siasa,wakoloni wakimtumia mwapachu aliyekua afisa kipenyo wao(special branch) kumpenyeza taa kisha tanu
 
Mpasuko wa kidini unaoonekana kutoka kwa wachangia mada ni ishara ya wazi ya tatizo tulilonalo Tanzania kwa sasa. Ukiangalia hapa utaona wanaotukuza ushindi wa nyerere kwenye huo uchaguzi wengi wana msukumo wa kidini wakati upande mwengine pia una hoja zinazoashiria msukumo kama huo ama malalamiko ya udini dhidi ya nyerere na tawala yake.

Swali la msingi la kujiuliza hapa ni kuwa nani ni chanzo cha haya mambo ya hisia za udini? ni wapi tunaenda kama taifa? na nini tunapaswa kufanya kutoka katika hii hali!

Nia thabiti yenye hamu ya kutenda haki kwa wote ndo ufunguo wa kutatua hili balaa linalochipua hapa. Swali la msingi ni je tupo tayari kufanya haki kwa wengine bila kujipendelea wenyewe? (hii ni kwa yeyote mwenye kuchangia kuondoa kadhia hii, ikiwa ni muongeaji tu ama mwenye mamlaka)
Unakua rais,unavunja taasisi ya waislam ya afrika mashariki,serikali yako,kwa miaka 25 haiteui waziri wa elimu muislam ila unateua padre kuwa waziri,na wanaofaulu na kupata elimu za juu ni watu wa dini yako kwa 75+%,mdini nani,nani mpandaji wa mbegu ya udini!?
 
Back
Top Bottom